Hadi Talk: Nani Anaweza Kumtazama Lowassa Machoni na Amwambie Hufai? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadi Talk: Nani Anaweza Kumtazama Lowassa Machoni na Amwambie Hufai?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Oct 21, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Si siri tena kwamba Lowassa ana mkakati mkubwa wa kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Na wale Thomases wajue kwamba hakuna atakayeweza kumzuia Lowassa kwa sasa. Malecela alikuwa na mikakati kama hii ila Nyerere alimwangalia machoni na kumwambia hafai. Je, ni nani katika CCM leo anaweza kumkemea Lowassa? Mashaka yangu ni kuwa kama alivyosema Mwalimu, mtu anayeitafuta sana ikulu kama alivyo Lowassa, atakuwa anatafuta maslahi binafsi na hivyo hatufai. Ila kwa upande mwingine angashinda Lowassa kwa tiketi ya CCM ningefurahi ili iwe rahisi zaidi kwa CDM kushinda maana itakuwa ngumu sana kumuuza!
   
 2. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Lowassa hauziki na hawezi kuuzika. Kwa taarifa tu Lowassa ameunda mkakati wa kujisafisha unaongozwa na jamaa anaitwa Opulukwa (mpwa wa marehemu Sokoine) hilo kundi limetengeneza mtandao unaotaka rais ajae anatokea Kasikazini. Hiyo kampeni ni kubwa sana inapigwa hadi kwenye bar. Lakini natoa taadhari kwa watanzania wajue kuwa EL ni mbaya sana ni mtu hatari sana. Kule Monduli adui yake anayemtajwa ni Mwakyembe, mmasai yoyote analijua hili. Namtahadharisha EL kuwa hii nchi si yake ni ya watanzania wote na asije akathubutu kuwalaghai watz
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuna mwandishi leo nilikuwa nazungumza nae akasema akijisikia kuishiwa anamwandika vizuri Lowassa na akifanya hivyo anapigiwa simu anapata si chini ya milioni. Hizi hela zinatoka wapi? Usikute wapo freemasons?
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ki ukweli ni mchapa kazi ila ni fisadi FULL STOP.......................HATUFAI.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Is it that easy to fool everybody in Tanzania? Kuna vitu haviwezekani. Time will tell
   
 6. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...mwacheni ang'ang'anie, ila aangalie asije fia mtaroni!
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Inaeza kuwa kweli kwa mujibu wa magazeti ya leo, jamaa kaanza kuonekana mwema
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huu ni uharo huu mie sitaki kujadili kila kitu wacha nisome tu nyie jadili .Mtu hana hata faida kwa Taifa katudidimiza badala tutumie muda kujadili Katiba tunaongelea Lowasa .Usanii huu
   
 9. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  .....mnyonge mnyongeni, sifa zake mpeni.... kwa hali ilivyo hivi sasa tunahitaji rais ajaye awe kama Lowasa (hapa nieleweke, sijasema Lowasa), kama yeye ni gamba, japokuwa mimi sioni tofauti ya wao wanaomwona Lowasa gamba na Lowasa mwenyewe, ukweli tu unabaki kwamba anapigwa vita na wenzake wanaoutaka uras kama yeye au wanaomtaka mtu fulani kwa manufaa binafsi, gamba limelenga watatu tu, ni wajinga tu ndio wataaminishwa hivyo, tusio wavivu kufikiri tunajua huo ni mkakati wa kumtoa Lowasa katika harakati za kuwania urasi....suala linabaki ni URAIS
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Bonge bonge mkuu, kidogo nakupata maana hata mtu mmoja wa ndani alinambia JK hataki tena(amekengeuka) inshu ya kumwachia Lowassa urais anapoondoka as agreed before kati yao hao ambao hawakukutana road,sasa namna ya kumchinjia baharini ndo ikaibuliwa inshu ya kuvua gamba ambayo lengo ilikuwa kuwaondoa katika nafasi za chama za kimamlaka wasiwe na ushawishi u can see hata Igunga anayeitwa gamba na kwamba kaipunguzia mvuto ccm (rostam) ndie alipigiwa magoti aendeshe kampeni. makes sense tatizo ni urais
   
 11. m

  mharakati JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  Huu "uchapa kazi" wa huyu Lowassa ni moja ya mkakati wa kumuingiza magogoni. Mi nafikiri tumefilisika kiungozi kwani mtu akifanya kazi yake kama waziri anaitwa mchapa kazi kwa sababu wengi hawafanyi kazi au nini anachofanya nje ya kazi yake na majukumu yake kama alipokua waziri na waziri mkuu, kuna lolote nje ya majukumu yake? kama anatekeleza majukumu yake kwa kiwango na muda basi ni jukumu lake na huwezi kusema ni mchapa kazi mchapa kazi ni mtu anayeenda hadi nje ya majukumu kufanya yale anayoona yanasadia kazi yake ya kama kiongozi (kumbuka Mrema) na siyo huyu anayefanya kazi yake na kujinufaisha hapo hapo na kakeki ketu kadogo haka.

  Umakini unatakiwa
   
 12. only83

  only83 JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mimi..........
   
Loading...