Hadi sasa nani kaenda mahakamani kumshtaki Dr. Slaa?

BroJay4

JF-Expert Member
Aug 27, 2007
236
16
Waliopania kumshitaki Dk. Slaa waendelea kujiandaa?

na Happiness Katabazi


HADI jana hakuna hata mmoja miongoni mwa watu waliotajwa wakituhumiwa kuwa ni mafisadi, aliyekuwa ametekeleza azima ya kumfungulia mashitaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Watu hao, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, na Patrick Rutabanzibwa, walishatangaza azima yao ya kumfungulia Dk. Slaa mashitaka kwa madai kuwa alikuwa amewakashifu kwa kuwatuhumu kuwa ni mafisadi.

Akihutubia umati uliofurika katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembeyanga, Dk. Slaa alitoa orodha ya watu 11 aliowatuhumu kuwa ni mafisadi na wabadhirifu wa mali ya umma.

Uchunguzi uliofanywa na ‘Tanzania Daima’ kuanzia Septemba 18 hadi jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mahakama za wilaya jijini hapa, umegundua kwamba hakuna hata mmoja aliyekwishatekeleza azma hiyo.

Siku chache baada ya Dk. Slaa kutaja majina hayo, baadhi ya watuhumiwa hao walikana tuhuma hizo na kusema ni za uongo na kuahidi kumfungulia kiongozi huyo kesi ya kashfa kwani amewachafulia majina.

Kwa upande wake, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), alishasema wazi kuwa hatomshitaki Dk Slaa, wakati Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, alisema kwamba tuhuma hizo ni utumbo mtupu na hakusema atamfikisha mahamakani.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Karamagi alisema kuwa atafungua kesi hiyo katika kipindi kisichozidi saa 48, lakini ni zaidi ya wiki sasa na bado hajatekeleza azma yake.

Alipoulizwa na gazeti hili wiki iliyopita, alisema bado dhamira yake ipo pale pale na alikuwa anajiandaa kufungua kesi hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliliambia gazeti hili kuwa suala hilo ni gumu kutokana na mtego uliowekwa na Dk Slaa, ambaye hajaweka bayana aina ya ushahidi alionao dhidi ya watu anaowatuhumu.

“Hata wao waliotuhumiwa wana hofu kuwa iwapo suala hili litafikishwa mahakamani, kuna uwezekano wa mambo mengine mengi kufichuka na kuzidi kuwagandamiza,” alisema mwanasheria mmoja ambaye hakupanda jina lake litajwe gazetini.

Hata hivyo, wakili mwingine, Robert Rugemalila, alisema kitendo cha watuhumiwa hao kushindwa kwenda mahakamani hadi sasa kinaleta hisia kwa wananchi kuwa huenda tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa zina ukweli ndani yake.

“Hawa wana uwezo wa kifedha wa kuweka wanasheria wazuri wa kuendesha kesi zao…sasa ni kitu gani kinachowakwamisha hadi kumfikisha mahakamani Dk.Slaa wanayesema amewachafulia majina yao?

“Haiingii akili kabisa mtu akuvunjie heshima na kukuchafulia jina mbele ya jamii halafu ukae kimya na ushindwe kumpeleka mahakamani, kwa hili serikali na watuhumiwa hao wanawahaada wananchi,” alisema Rugemalila.


Source:Tanzania Daima.
Dr. Slaa alitega bomu,je ni nani wa kulilipua au walikua wanamsubiria Kikwete?
 
Mimi naamini kabisa kwamba hakuna wa kwenda Mahakamani kwa kuwa hata Mkuu wa Kaya hana moto na malalamiko ya wananchi ila kama wazungu watapiga kelele. Issue sasa imesha kuwa diverted Buzwagi haisemwi wote wanaweka matumaini na masikio yao kule BOT ambako wanajua wanaweza kuficha ukweli baada ya matokeo ila la Buzwagi kwa kuwa hata Mkataba uko nje wanali puuzia . Si JK wala Karamagi anaweza kufanya lolote na ndiyo maana JK anakubaliana na ziara za Mawaziri wake mikoani kwa anajua nini wanafanya.

Hapa dawa ni Slaa kuingia Mahakamani awaite na hapa patakuwa patamu sana .

Ila kweli wameshikwa pabaya sana this time .
 
Ngugu yangu Lunyungu,
Dr, Slaa amemwaga mtama hadharani ili kila mtu mwenye njaa adonoe. nadhani si vyema kudhani ni slaa peke yake anaweza kwenda Mahakamani. Slaa akienda vema, lakini mtanzania Yeyote au kikundi chochote kama inaonekana ni vema kwenda mahakamani, I think mlango uko wazi wa kufanya hivyo
 
Waache waende msiwashtue sana! Ila nawaomba mjaribu kutafuta vitengo vya mawakili toka mashirika makubwa yanayopigana na rushwa duniani, haya yapo huru kutoa mawakili wao ktk kesi kama hizi na hasa nchi maskini ambazo wanajaribu sana kupigana na viongozi wanaokula rushwa.
Kuna kimoja ambacho Blair yupo ndani kama mwenyekiti nasikia wanafanya kazi kama Amnesty International kwa hiyo nasi tujiandae upande huu. Hawa jamaa hudai hata nyaraka za mikataba na kama Dr. Slaa atanyimwa haki yake basi kesi hii haitaishia mahakamakuu ya Bongo..
 
Waache waende msiwashtue sana! Ila nawaomba mjaribu kutafuta vitengo vya mawakili toka mashirika makubwa yanayopigana na rushwa duniani, haya yapo huru kutoa mawakili wao ktk kesi kama hizi na hasa nchi maskini ambazo wanajaribu sana kupigana na viongozi wanaokula rushwa.
Kuna kimoja ambacho Blair yupo ndani kama mwenyekiti nasikia wanafanya kazi kama Amnesty International kwa hiyo nasi tujiandae upande huu. Hawa jamaa hudai hata nyaraka za mikataba na kama Dr. Slaa atanyimwa haki yake basi kesi hii haitaishia mahakamakuu ya Bongo..

Hili ni wazo zuri kabisa,Ni vema kujiandaa ili kama haki haitendeki katika mahakama zetu (kama ilivyo shaka ya wengi)mambo yasiishie hapo bali tuipe nafasi hata dunia ya nje nayo itusemee kwa kishindo.
 
Naanza kuona mambo kama ya Lunyungu kwamba hapa ni changa la macho .Wote waujua moto sasa hawawezi kucheza maana wataungua sana .Wacha tuone lakini kwenye hili kuna kuchemka sana kuanzia CCM na Ikulu .
 
Back
Top Bottom