Uchaguzi 2020 Hadi sasa kimkakati CHADEMA wameizidi CCM

Huyu Mungu mnayemsemea ni Mungu yupi.
Huyu huyu tunayemwamini? Huyu huyu aliyesema tusihukumu tusije tukahukumiwa? Ni huyu aliyekataza ushoga?

Maana kati ya hao wawili kuna mmoja ni mmumini wa ushoga kwa kigezo cha haki za binadamu
Una ushahidi?
 
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho na isiyoonekana. Kwa inayoonekana ni wazi kuwa....

Pamoja na CCM kuwa na kila kitu kinachotakiwa kwenye kampeni, magari, viwanja, pesa you name it, lkn haina tofauti kubwa na Chadema inayotumia resources chache ilizonazo kwa makini.

Hadi sasa CHADEMA imezindua kampeni katika Kanda kuu zote za Tanzania bara na Zanzibar, huku CCM mgombea wao akizunguka kwenye mikoa michache ya kanda ya kati na Ziwa Victoria tu.

Chama cha Mapinduzi kimehodhi vyombo vyote vya habari TV zote, redio zote, magazeti yote lkn habari zinazo trend zaidi ni za mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu.

Katika kuuza sera CCM wamekuwa wakijitetea zaidi kuliko kutangaza sera zao, mfano juzi mgombea wa CHADEMA alihoji ajira leo serikali imetangaza ajira 13,000 za walimu, Lissu kaongelea bima ya Afya kwa wote Magufuli na Majaliwa nao wanasema watatoa bima bure wakati haipo kwenye ilani yao.

CCM imetandaza mabango ya picha kubwa kubwa za mgombea wao nchi nzima karibu kila ukuta huku Chadema ikionekana kutokuwa na mabango lkn mwitikio wa wahudhuriaji hauna tofauti yoyote.

Pamoja na CCM kuwatumia wasanii wote wa Tanzania na wa nchi jirani ya Kenya bado haijawasaidia kuonyesha nguvu ya chama tawala na kikongwe kwenye kampeni yao.

CCM pesa wanayo vyombo vyote vya dola ni vyao, nini tatizo, inawezekana ni kampeni meneja na timu yake ya kampeni, ni wazito au wamefungwa kutoa maamuzi ya haraka.

Katika tathimini yangu kwa siku hizi za mwanzo wa kampeni CHADEMA imewazidi CCM kwa pointi ingawa siyo nyingi sana.
Mikakati gani?. Labda ya matusi na kebehi. Semeni hoja zenu, mtawasaidia nini watanzania kwenye changamoto zao.
 
Wewe ni mahaba hutaki kusema ukweli.
CCM WAKO KIMKAKATI NCHI NZIMA wanashambulia kila kona ya nchi.

Endeleeni kunifariji tuonane october 28
 
Niliwai sema na nasema tena Tundu Antiphas Lissu ni sawa na Mfalme Daudi na Magufuli ni sawa na Mfalme Sauli.

Sauli alikuwa na majeshi, fitna na fedha za kumshinda Daudi ila Daudi alikuwa na Mungu tu na Mungu aliweza kumshindia vita dhidi ya Sauli!
Amina mkuu
 
Back
Top Bottom