Mnyakatari
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 2,027
- 1,791
Mpaka sasa chadema ina viti 23 ukilinganisha na wabunge wa5 wa bunge lililopita.Hii ni baada ya kuchakachua huko kigoma mjini,songea mjini,mbeya vijijini,mbozi magharibi,kilombero,segerea na kwinginepo ambapo pameripotiwa.Bila hivyo vingefika viti zaidi ya 40.Hata hivyo idadi iliyoongezeka ni kubwa,360%.Nawapongeza sana viongozi wote wa chadema kwa kazi kubwa iliyofanyika.Sipati picha bunge lijalo litakavyokuwa baada ya kambi ya upinzani kuongezeka.Sijui chadema itakuwa na viti vingapi maalum anayejua utaratibu naomba anijuze.Kwaiyo wakuu kazi iliyofanyika ni kubwa na sisi wanaharakati twende kinyume na wote wanaobeza,najua wengi wao ni walamba viatu vya kina ki..te.Well done CHADEMA.