Elections 2010 Hadi sasa CHADEMA imeshinda

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
2,025
1,791
Mpaka sasa chadema ina viti 23 ukilinganisha na wabunge wa5 wa bunge lililopita.Hii ni baada ya kuchakachua huko kigoma mjini,songea mjini,mbeya vijijini,mbozi magharibi,kilombero,segerea na kwinginepo ambapo pameripotiwa.Bila hivyo vingefika viti zaidi ya 40.Hata hivyo idadi iliyoongezeka ni kubwa,360%.Nawapongeza sana viongozi wote wa chadema kwa kazi kubwa iliyofanyika.Sipati picha bunge lijalo litakavyokuwa baada ya kambi ya upinzani kuongezeka.Sijui chadema itakuwa na viti vingapi maalum anayejua utaratibu naomba anijuze.Kwaiyo wakuu kazi iliyofanyika ni kubwa na sisi wanaharakati twende kinyume na wote wanaobeza,najua wengi wao ni walamba viatu vya kina ki..te.Well done CHADEMA.
 
Mimi naona ni ushindi CHADEMA ila sasa CHADEMA wajipange wafungue ofisi majimboni tayari kwa mapambano ifikapo mwaka 2015..
 
Well done Chadema.
Kinachotakiwa sasa ni kujipanga na kufungua matawi mengi kadri iwezekanavyo.Kuandikisha wanachama wapya,kutangaza sera nk.
Yaani safari ya kuchukua ushindi 2015 tuianze sasa,na sisi wananchi wanamapinduzi na wenye mapenzi ya kweli na nchi hii tuko nyuma yenu.
Daima msikubali kuvurugwa na CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom