Hadi leo sijaelewa faida za utumbuaji wa majipu

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Wanabody habari,

Najua kwa namna moja au nyingine kuna watu watanichukia kutokana na thread yangu hii, kiukweli nampongeza sana raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri ya utumbuaji wa majipu anayofanya, kwasababu taifa lilifikia mahala pabaya sana kwa kutafunwa na mchwa.

Ila pamoja na jitihada za kutumbua hayo majipu lakini mimi bado sijaona wala kupata faida ya moja kwa moja katika maisha, kwanza maisha bado ni magumu na maskini hatujapata ahueni ya maisha kabisa,kwasababu vitu bado bei zipo juu na biashara imekuwa ngumu sana.

Lakini pia hao watu wanaotumbuliwa hayo majipu mi sioni cha maana kwa sababu wao wametutia hasara sana ila adhabu yao eti inakuwa ni kuwasimamisha kazi, sasa kumsimamisha kazi maana yake nini na mtu kakuibia? Hapo nashindwa kuelewa, kwasababu hata ukiwasimamisha kazi bila kuwafirisi haina maana yoyote ile, kwani mi nikiibia kampuni mfano 900 bila, harafu kampuni ikaishia kunifukuza kazi hivi ntapata hasara gani hapo?
 
Kuwa na subra mkuu kumfilisi mtu ni hadi mahakama imkute na hatia, hakuna kesi iliyoamliwa kati ya wote waliosimamishwa kwenye hii awamu ya 5 na hakuna mtu aliyesimamishwa kazi bila kufanyiwa uchunguzi, wengine uchunguzi umemalizika kesi zipo mahakamani wengine uchunguzi unaendelea, just stay tuned ndani ya miezi miwili tu utaona watu wanavofilisiwa wakibainika kufanya ufisadi, JPM hatanii.
 
Kufirisiwa weka ndoto,labda sio kwa tanzania hii
 
Wanabody habari,najua kwa namna moja au nyingine kuna watu watanichukia kutokana na thread yangu hii.kiukweli nampongeza sana raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri ya utumbuaji wa majipu anayofanya.kwa sababu taifa lilifikia mahala pabaya sana kwa kutafunwa na mchwa.ila pamoja na jitihada za kutumbua hayo majipu lakini mimi bado sijaona wala kupata faida ya moja kwa moja katika maisha,kwanza maisha bado ni magumu na maskini hatujapata ahueni ya maisha kabisa.kwa sababu vitu bado bei zipo juu na biashara imekuwa ngumu sana,lakini pia hao watu wanaotumbuliwa hayo majipu mi sioni cha maana kwa sababu wao wametutia hasara sana ila adhabu yao eti inakuwa ni kuwasimamisha kazi,sasa kumsimamisha kazi maana yake nini na mtu kakuibia?hapo nashindwa kuelewa.kwa sababu hata ukiwasimamisha kazi bila kuwafirisi haina maana yoyote ile,kwani mi nikiibia kampuni mfano 900 bil,harafu kampuni ikaishia kunifukuza kazi hivi ntapata hasara gani hapo?
Kwa hiyo ulitaka pepo uione ndani ya siku mia moja!? Get off your butt and do some useful stuff!!
 
Kiukweli inakuwa Hakuna maana kama mtu anasimamishwa afu nyumbani ana mabilioni ya hela
Naskia lakini miongoni mwa waliosimamishwa wanapisha uchunguzi
Ingawaje sio wote
 
Wanabody habari,najua kwa namna moja au nyingine kuna watu watanichukia kutokana na thread yangu hii.kiukweli nampongeza sana raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri ya utumbuaji wa majipu anayofanya.kwa sababu taifa lilifikia mahala pabaya sana kwa kutafunwa na mchwa.ila pamoja na jitihada za kutumbua hayo majipu lakini mimi bado sijaona wala kupata faida ya moja kwa moja katika maisha,kwanza maisha bado ni magumu na maskini hatujapata ahueni ya maisha kabisa.kwa sababu vitu bado bei zipo juu na biashara imekuwa ngumu sana,lakini pia hao watu wanaotumbuliwa hayo majipu mi sioni cha maana kwa sababu wao wametutia hasara sana ila adhabu yao eti inakuwa ni kuwasimamisha kazi,sasa kumsimamisha kazi maana yake nini na mtu kakuibia?hapo nashindwa kuelewa.kwa sababu hata ukiwasimamisha kazi bila kuwafirisi haina maana yoyote ile,kwani mi nikiibia kampuni mfano 900 bil,harafu kampuni ikaishia kunifukuza kazi hivi ntapata hasara gani hapo?
Ulivyoanza tu kwa kujihami kwamba unajua utachukiwa inaonyesha wewe ni JIPU tosha. Pia inawezekana hapo ulipo kuanzia asubuhi haujajishughulisha na chochote hata kwenda kujitolea kung'oa nyasi Muhimbili Ila unatumia computer ya shemeji kuikejeli Serikali...wewe ni JIPU....tena Juvenile JIPU.
 
Usiwe na shaka Juvenile muda ukifika utaona faida ya zoezi la kutumbua majipu linaloendelea hivi sasa. Vuta subira asubuhi yenye matumaini inakaribia.
 
Dah, akili imechoka kutokana na Heka Heka za Leo, wewe unaleta uzi ambao hauna paragraph, Hebu paraphrase basi na sisi wengine tusome.
 
Kumbuka msamaha wa wafungwa uliotolewa na Raisi.. Ilikuwa ni kuongeza nafasi magerezani maana majipu yanakwenda kuzijaza gereza zetu hivi punde.
 
Ulivyoanza tu kwa kujihami kwamba unajua utachukiwa inaonyesha wewe ni JIPU tosha. Pia inawezekana hapo ulipo kuanzia asubuhi haujajishughulisha na chochote hata kwenda kujitolea kung'oa nyasi Muhimbili Ila unatumia computer ya shemeji kuikejeli Serikali...wewe ni JIPU....tena Juvenile JIPU.
Dah kiongozi ulivyomjibu vizuri,,, nilikuwa nataka kumjibu the same lakini nilishikwa na uvivu wa kuandika. Asante kwa jibu mahili mdau!
 
Nenda pale ubungo mataa angalia wingi wa maroli ya ,,makontena na mafuta ,,kwenda mikoani na nchi jirani yalivyopungua,, baada ya MAJIPU ya ,,BANDARINI,,na TRA kutumbuliwa.
 
Wanabody habari,najua kwa namna moja au nyingine kuna watu watanichukia kutokana na thread yangu hii.kiukweli nampongeza sana raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri ya utumbuaji wa majipu anayofanya.kwa sababu taifa lilifikia mahala pabaya sana kwa kutafunwa na mchwa.ila pamoja na jitihada za kutumbua hayo majipu lakini mimi bado sijaona wala kupata faida ya moja kwa moja katika maisha,kwanza maisha bado ni magumu na maskini hatujapata ahueni ya maisha kabisa.kwa sababu vitu bado bei zipo juu na biashara imekuwa ngumu sana,lakini pia hao watu wanaotumbuliwa hayo majipu mi sioni cha maana kwa sababu wao wametutia hasara sana ila adhabu yao eti inakuwa ni kuwasimamisha kazi,sasa kumsimamisha kazi maana yake nini na mtu kakuibia?hapo nashindwa kuelewa.kwa sababu hata ukiwasimamisha kazi bila kuwafirisi haina maana yoyote ile,kwani mi nikiibia kampuni mfano 900 bil,harafu kampuni ikaishia kunifukuza kazi hivi ntapata hasara gani hapo?
Ni vizuri kutoa yako ya moyoni ila hujashughulisha kichwa kupata majibu. Anyways nianze na hoja yako ya kushuka bei vitu. Kusimamishwa mtumishi wa umma haina uhusiano wa papo kwa papo wa kushuka bei ila uhusiano wake utakujaonekana pale litakapokuwa kila mtu anapata kipato chake halali na si kupiga hela nyingi kwa ujanja. Kivipi? Hii itatokana na kutokuwepo watu ambao wanapesa za kuchezea ambazo hawezi nunua kitu kwa bei ghali ukilinganisha na thamani halisi ya kitu anachonunua.
Kuhusu watu kutofikishwa mahakamani wala kufirisiwa ni kwamba; hao watu wanasimamishwa ili kupisha uchunguzi. Uchunguzi ndiyo utakaokuja na ushahidi madhubuti wa kumpeleka mtu mahakamani. Huwezi kumfilisi mtu bila kuonekana na hatia mahakamani. Sheria ya kufilisi ipo na kipindi hiki ndiyo kwa mara ya kwanza nimesikia inatajwa tajwa tena. Hivyo hayo yaweza kutokea kwa wale watakaokutwa na hatia mahakamani.
NB: Aliyefukuzwa mpaka sasa hivi ni yule aliyekuwa katibu tawala Mwanza tena kwa kosa la utovu wa nidhamu.
 
Ilikujua maana halisi ya majip rais anamaanisha nini sikiliza hotuba aliyo hutubia mahakama, anataka maakama wafanye kaz yake, mtu afanyiwe uchunguzi, akikutwa na hatia sheria ifate mkondo wake, let yu wait ma braza soon tutapata positive result ya majip
 
Tumeanza safari ya canaan kwa kishindo ila Nahodha wetu katangulia hatua nyingi mno. Hayo tunayoyaita majipu mengine hayawezi kutumbuliwa.Hivi kweli ni wafanyabiashara pekee ndio wametufikisha hapa tulipo au wako na vigogo kama marais waliotangulia nao? Kuna minong'ono kibao kuwa baadhi ya wanafamilia ya hao marais wameshiriki katika biashara wakifanya ubia na baadhi ya wafanyabiashara na hadi sasa hawamo kwenye list ya kutumbuliwa majipu kwa kosa la kukwepa kodi. Sasa je hao nao ikija kubainika watatumbuliwa majipu? Na kama watatumbuliwa majipu katiba yetu itakuwa imesimama wapi kwa kile kipengere kuwa Rais HATAGUSWA KWA JAMBO LOLOTE AWEPO MADARAKANI AU BAADA YA KUTOKA?
 
Wanabody habari,najua kwa namna moja au nyingine kuna watu watanichukia kutokana na thread yangu hii.kiukweli nampongeza sana raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri ya utumbuaji wa majipu anayofanya.kwa sababu taifa lilifikia mahala pabaya sana kwa kutafunwa na mchwa.ila pamoja na jitihada za kutumbua hayo majipu lakini mimi bado sijaona wala kupata faida ya moja kwa moja katika maisha,kwanza maisha bado ni magumu na maskini hatujapata ahueni ya maisha kabisa.kwa sababu vitu bado bei zipo juu na biashara imekuwa ngumu sana,lakini pia hao watu wanaotumbuliwa hayo majipu mi sioni cha maana kwa sababu wao wametutia hasara sana ila adhabu yao eti inakuwa ni kuwasimamisha kazi,sasa kumsimamisha kazi maana yake nini na mtu kakuibia?hapo nashindwa kuelewa.kwa sababu hata ukiwasimamisha kazi bila kuwafirisi haina maana yoyote ile,kwani mi nikiibia kampuni mfano 900 bil,harafu kampuni ikaishia kunifukuza kazi hivi ntapata hasara gani hapo?
Mkuu mabadiliko na maendeleo ya nchi hayaji kama pesa toka kwenye ATM. Vinginevyo Zimbambwe leo hii ingekuwa nchi tajiri kuliko zote duniani. Kwa kuwafukuza kazi maana yake ni kustopisha ule uzembe na uhujumu wa uchumi pamoja na wizi. Fedha na maendeleo ya nchi itakuwa kwa wote. Kuhusu kuwachukulia hatua nina uhakika kabisa kwamba hawa watu wanao fukuzwa kazi huwa wana fuatwa na PCCB kwa mahojiano zaidi. Magufuli sio mjinga alipo amua kuitengeneza upwa hii PCCB na kuionya Mahakama. Sasa hivi nina wasi wasi sana na ofisi ya DPP kama itaendelea kuwa salama. Tusubiri tuone.
 
kamanda mtoa mada unaonekana unaharaka sana na kuona maendeleo ya wananchi. kwani ni miezi mingapi tangu Magu aingie madarakani. fikiria uozo uliojengeka kwa miaka zaidi ya kumi unadhani unaweza ukaumaliza overnight? ?? subira yavuta heri kamanda. bila haya nchi yetu haitakwenda mbele kamwe. ni lazima kujenga mifumo kabla ya kuanza kazi ati.
 
Wanabody habari,najua kwa namna moja au nyingine kuna watu watanichukia kutokana na thread yangu hii.kiukweli nampongeza sana raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri ya utumbuaji wa majipu anayofanya.kwa sababu taifa lilifikia mahala pabaya sana kwa kutafunwa na mchwa.ila pamoja na jitihada za kutumbua hayo majipu lakini mimi bado sijaona wala kupata faida ya moja kwa moja katika maisha,kwanza maisha bado ni magumu na maskini hatujapata ahueni ya maisha kabisa.kwa sababu vitu bado bei zipo juu na biashara imekuwa ngumu sana,lakini pia hao watu wanaotumbuliwa hayo majipu mi sioni cha maana kwa sababu wao wametutia hasara sana ila adhabu yao eti inakuwa ni kuwasimamisha kazi,sasa kumsimamisha kazi maana yake nini na mtu kakuibia?hapo nashindwa kuelewa.kwa sababu hata ukiwasimamisha kazi bila kuwafirisi haina maana yoyote ile,kwani mi nikiibia kampuni mfano 900 bil,harafu kampuni ikaishia kunifukuza kazi hivi ntapata hasara gani hapo?
Wait after 3 yrs ndo utaanza kuona faida. kwa sasa huwezi ona coz bado mapema sana. but kukusaidia ti ni kwamba hazina kuu ilikuwa tupu, now imeanza kuwa na pesa
 
Back
Top Bottom