Hadi kifo cha Ruge mnamlaumu Mungu!? Jifunzeni kitu hapa...

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Habari za muda huu wanajamvi.

Poleni ndugu jamaa na marafiki pia kwa msiba mzito wa jamaa/rafiki yetu Ruge Mutahaba. Inauma sana na tutamkumbuka kwa mengi hasa kwenye mapinduzi ya soko la muziki wetu wa kizazi kipya yaani bongo fleva.

Katika ulimwengu huu uliochini ya Shetani Ibilisi kumekuwa na tabia za mazoa mabaya sana ambayo yana mshushia Mungu wetu heshima na kuonekana kama katili, kivipi? Pindi mtu anapokufa utasikia kila mtu wanasiasa,ndugu/jamaa wakisema:-
"TULIMPENDA LAKINI MUNGU KAMPENDA ZAIDI"
"MUNGU KAAMUA KUMCHUKUA"
"KIFO CHAKE KILINGWA HIVYO"
"MUNGU KAMPUNZISHA"
"BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA"
"KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA"

Ukweli ni kwamba Mungu hasababishi kifo cha mtu yeyote yule, Biblia inasema sifa kuu ya Mungu ni upendo 1Yoh 4:8 ikiwa hivyo Mungu anaweza kuuwa?
Biblia inataja wazi kuwa kifo ni adui na baadae Mungu atakiondoa, kifo kinawezaje kuwa pumziko la amani wakati yule aliekufa hayupo tena?

Mungu akimpenda mtu hawezi kumsababishia kifo, huyo mungu atakuwa katili basi, sababu haakuna anaependa kifo.

Ikumbukwe kuwa tunakufa sababu tumerithi dhambi ambayo alifanya Adamu na Hawa pale Eden(Rom 5:12)

Sababu zinazoweza sababisha vifo
tunazaliwa, tunakuaa, tunazeeka na tunarudi mavumbini(kufa), kuna magonjwa, au tukio lisilo tarajiwa na mwisho kabisa kifo cha kizembe au kujitakia.

Inasikitisha lakini tukishajua sababu basi...tutaumia kwa muda tukiwa na tumaini la kufufuliwa kwenye dunia paradiso. (Ndo 24:15)

TUSIPENDE KUFUATA MKUMBO TUCHUNGUZE KILE MUNGU AMESEMA KUPITIA NENO LAKE. SIO KAULI ZA VIONGOZI WA KIDINI NA MAZOEA YA KIPAGANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu mwenye uwezo wote alishndwaje kuumba ulimwengx ambao dhambi haiwezi kutendeka mpaka kukatokea kifo?

wakati ukuta.
 
Kifo ni adhabu iliyowekwa na Mungu,mitume na manabii wote walifariki,ila kuna kifo cha mpango wa Mungu na kuna kifo cha mpango wa shetani ambacho hutokea tukimuasi Mungu kama wa Israeli walivyo fanya. ..tusome Isaya 1:18-20

Sent using Jamii Forums mobile app
Kifo cha mpango wa Mungu kipoje? Mungu hakuweka kifo,kifo kilitokea baada ya uasi pale Eden ( Roma 5:12) hata uwe nani lazma ufe tu uwe nabii, mfalme, rais mwadilifu,mtenda dhambi wote kifo ni lazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu wanajamvi... poleni ndugu jamaa na marafiki pia kwa msiba mzito wa jamaa/rafiki yetu Ruge Mutahaba. Inauma sana na tutamkumbuka kwa mengi hasa kwenye mapinduzi ya soko la muziki wetu wa kizazi kipya yaani bongo fleva.

Katika ulimwengu huu uliochini ya Shetani Ibilisi kumekuwa na tabia za mazoa mabaya sana ambayo yana mshushia Mungu wetu heshima na kuonekana kama katili, kivipi? Pindi mtu anapokufa utasikia kila mtu wanasiasa,ndugu/jamaa wakisema:-
"TULIMPENDA LAKINI MUNGU KAMPENDA ZAIDI"
"MUNGU KAAMUA KUMCHUKUA"
"KIFO CHAKE KILINGWA HIVYO"
"MUNGU KAMPUNZISHA"
"BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA"
"KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA"

Ukweli ni kwamba Mungu hasababishi kifo cha mtu yeyote yule, Biblia inasema sifa kuu ya Mungu ni upendo 1Yoh 4:8 ikiwa hivyo Mungu anaweza kuuwa???
Biblia inataja wazi kuwa kifo ni adui na baadae Mungu atakiondoa,kifo kinawezaje kuwa pumziko la amani wakati yule aliekufa hayupo tena?

Mungu akimpenda mtu hawezi kumsababishia kifo,huyo mungu atakuwa katili basi,sababu haakuna anaependa kifo.

Ikumbukwe kuwa tunakufa sababu tumerithi dhambi ambayo alifanya Adamu na Hawa pale Eden(Rom 5:12)

Sababu zinazoweza sababisha vifo
tunazaliwa,tunakuaa,tunazeeka na tunarudi mavumbini(kufa).kuna magonjwa, au tukio lisilo tarajiwa na mwisho kabisa kifo cha kizembe au kujitakia.

Inasikitisha lakini tukishajua sababu basi...tutaumia kwa muda tukiwa na tumaini la kufufuliwa kwenye dunia paradiso. (Ndo 24:15)

TUSIPENDE KUFUATA MKUMBO TUCHUNGUZE KILE MUNGU AMESEMA KUPITIA NENO LAKE. SIO KAULI ZA VIONGOZI WA KIDINI NA MAZOEA YA KIPAGANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku ile pale Tanga kama angejua asingemshika mkono.Kuna sumu alishikishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifo kiliumbwa na Mungu kama alivyoumba kuzaa na kuzaliwa.Sasa kila kifo lazima kiwe na sababu na watu kusema Mungu kampenda zaidi ni maneno tu yakibinadamu yakufarijiana kwasababu swala la kifo liko juu ya uwezo wa binadamu kwaiyo aliyekiumba kifo ndiye ambaye ana mamlaka ya uyo mtu kwakumleta duniani na kumuondoa muda ukifika.
 
Ndio Mungu ndiye aliumba kifo.Alisema hakika kufa tutakufa.Hilo la wazazi wako wa kwanza hiyo ni sababu ya kifo au kufa ila sio kifo.Kifo ni tendo lililoumbwa kama uhai ulivyoumbwa ila ili ufe lazima kuwe na sababu.Kwaiyo usichanganye sababu ya kifo na kifo.
Kwani Mungu ndiye alieumba kifo?? Kifo kimesababishwa na wazazi wetu wa kwanza baada ya kutokutii kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom