Hadi kifo cha Ruge mnamlaumu Mungu!? Jifunzeni kitu hapa...

Swali langu linauliza ilikuwaje mungu muweza yote alishndwaje kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezi kuwako mpaka kupelekea Adam na Hawa kuirithsha kwa wanadamu wengne mpaka kukawa na kifo.. Kwa maelezo ya mtoa mada!

wakati ukuta.
Swali lako na mtoa mada mtamalizana wenyewe ila langu mie ni hapo uliposema "Mungu kashindwa....." ndiyo maana nikakuuliza kwamba watu wanatenda dhambi kwa sababu Mungu ameshindwa kuumba ulimwengu ambako dhambi hazitendeki? Kwa sababu hii suala la Mungu kushindwa ni jipya kwangu ndio nakusikia wewe.
 
Habari za muda huu wanajamvi.

Poleni ndugu jamaa na marafiki pia kwa msiba mzito wa jamaa/rafiki yetu Ruge Mutahaba. Inauma sana na tutamkumbuka kwa mengi hasa kwenye mapinduzi ya soko la muziki wetu wa kizazi kipya yaani bongo fleva.

Katika ulimwengu huu uliochini ya Shetani Ibilisi kumekuwa na tabia za mazoa mabaya sana ambayo yana mshushia Mungu wetu heshima na kuonekana kama katili, kivipi? Pindi mtu anapokufa utasikia kila mtu wanasiasa,ndugu/jamaa wakisema:-
"TULIMPENDA LAKINI MUNGU KAMPENDA ZAIDI"
"MUNGU KAAMUA KUMCHUKUA"
"KIFO CHAKE KILINGWA HIVYO"
"MUNGU KAMPUNZISHA"
"BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA"
"KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA"

Ukweli ni kwamba Mungu hasababishi kifo cha mtu yeyote yule, Biblia inasema sifa kuu ya Mungu ni upendo 1Yoh 4:8 ikiwa hivyo Mungu anaweza kuuwa?
Biblia inataja wazi kuwa kifo ni adui na baadae Mungu atakiondoa, kifo kinawezaje kuwa pumziko la amani wakati yule aliekufa hayupo tena?

Mungu akimpenda mtu hawezi kumsababishia kifo, huyo mungu atakuwa katili basi, sababu haakuna anaependa kifo.

Ikumbukwe kuwa tunakufa sababu tumerithi dhambi ambayo alifanya Adamu na Hawa pale Eden(Rom 5:12)

Sababu zinazoweza sababisha vifo
tunazaliwa, tunakuaa, tunazeeka na tunarudi mavumbini(kufa), kuna magonjwa, au tukio lisilo tarajiwa na mwisho kabisa kifo cha kizembe au kujitakia.

Inasikitisha lakini tukishajua sababu basi...tutaumia kwa muda tukiwa na tumaini la kufufuliwa kwenye dunia paradiso. (Ndo 24:15)

TUSIPENDE KUFUATA MKUMBO TUCHUNGUZE KILE MUNGU AMESEMA KUPITIA NENO LAKE. SIO KAULI ZA VIONGOZI WA KIDINI NA MAZOEA YA KIPAGANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani akitajwa MUNGU lazima awe huyo unaemwamini,hata Dola,Mabasi mengi yameandikwa "In God we trust".Wewe ukikaa ukafikiri wanamtaja Mungu wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maelezo haya unauliza ilimradi au unataka kujibiwaje..? Nauliza tena ilikuwaje mungu muweza yote akashndwa kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezi kuwako mpaka kupelekea Adam na Hawa kuirithsha kwa watu wengne mpaka kukawa na kifo?

Hauwezi kufika kumi kabla haujapita tisa!

Mpaka hapo nijibiwe ndyo naweza kuelewa mantiki yako inalenga nini!
Swali lako na mtoa mada mtamalizana wenyewe ila langu mie ni hapo uliposema "Mungu kashindwa....." ndiyo maana nikakuuliza kwamba watu wanatenda dhambi kwa sababu Mungu ameshindwa kuumba ulimwengu ambako dhambi hazitendeki? Kwa sababu hii suala la Mungu kushindwa ni jipya kwangu ndio nakusikia wewe.

wakati ukuta.
 
Kwa maelezo haya unauliza ilimradi au unataka kujibiwaje..? Nauliza tena ilikuwaje mungu muweza yote akashndwa kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezi kuwako mpaka kupelekea Adam na Hawa kuirithsha kwa watu wengne mpaka kukawa na kifo?

Hauwezi kufika kumi kabla haujapita tisa!

Mpaka hapo nijibiwe ndyo naweza kuelewa mantiki yako inalenga nini!

wakati ukuta.
Sasa mkuu nimekwambia kabisa kuwa hilo suala la Mungu kushindwa ndio kwanza nimelisikia kwako na ndiyo maana nakuuliza ili nilielewe vizuri ila wewe unataka nijibu tu kwanini Mungu kashindwa wakati mie silifahamu hilo suala la Mungu kushindwa,ni wewe ndiye unasema Mungu kashindwa kuumba ulimwengu ambao hauna kifo wala kufanyika dhambi halafu tena wewe tena unataka watu wakujibu kwanini alishindwa!

Hakuna anayesema kuna kifo na dhambi kwa sababu Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna kifo wala kufanyika dhambi,sasa mie nitaanzaje kujibu kwanini alishindwa wakati sijui hilo suala.
 
Swali langu linauliza ilikuwaje mungu muweza yote alishndwaje kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezi kuwako mpaka kupelekea Adam na Hawa kuirithsha kwa wanadamu wengne mpaka kukawa na kifo.. Kwa maelezo ya mtoa mada!

wakati ukuta.
Labda nikuelekeze kwa mifano ndio uelewe...

Tuseme umekuta gari ya mafuta imeanguka na ukiwa unajua kusoma imeandikwa "hatari usiguse inawaka (inflammable)" wewe umechukua sururu unaenda kutoboa ili upate mafuta,petrol ikilipuka na ukaungua ni nani atalaumiwa? Mwenye gari? Au utalaumiwa mwenyewe kwa tamaa yako na kutotii kwako?

Ukipata jibu linganisha na kilichotokea Eden

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini asife, yy ndo nani ama mliambia Ruge hatakufa ...kifo hakikwepeki na kila mja ataonja mauti
 
Kwani Mungu ndiye alieumba kifo?? Kifo kimesababishwa na wazazi wetu wa kwanza baada ya kutokutii kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila chenye uhai lazima kife, sasa kama Mungu ndie alikuumba na kukuleta duniani kwanini yeye asikuondoe? umesoma science? ni lazima tuumwe ili dawa zinunulike na tufe ili wengine waje, sasa kama kila siku watu wanazaliwa na wengine hawafi hii dunia si ingejaa hata hatua moja tusingepiga?

Nawashangaa watu mnaosema mnaamini Mungu na bado mamlaka mengine mnawapa wengine.
 
Kwani Mungu ndiye alieumba kifo?? Kifo kimesababishwa na wazazi wetu wa kwanza baada ya kutokutii kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu, vinavyoonekana na visivyoonekana, uzima na mauti kaviumba yeye. Ina maana hata miti, wanyama na wadudu wanapokufa ni kwa sababu wamerithi dhambi ya baba yao Adam? Adam alizaa miti, wanyama na wadudu? Hivi si aliviumba yeye mwenyewe kila kimoja kwa jinsi yake?

Kwahiyo ww unafanana na miti? Kama haufanani na miti kwani uwe tofauti na miti wakati wote mnakufa? Mfano wako umekufa wewe yan unajifananidha na mnyama!!aibu yako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo uliyotoa ni sababu ya kifo. Naomba kujua kifo kiliumbwa au hakikuumbwa? Kama kiliumbwa ni nani aliyeumba? Na kama hakikuumbwa inamaana kifo hakipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla sijajibu swali lako nenda kafanye itafiti kwanza kifo ni nn? Jaribu kusoma popote mpaka ujue kifo ni nn. Ukishajua kifo ni kitu gani njoo nikwambie kiliumbwa au hakikuumbwa. Kwa sasa siwez kukupa jibu mana hutaelewa. Mpaka ujue kifo ni nn kwanza

Kuna sababu gani ya kwenda kusoma pengine wakati wewe unayejua upo? Au na wewe hujui? Kama unajua elewesha ili watu waelewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom