Hadhi ya jengo zilimo ofisi za msajili wa makampuni

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,569
Ndugu wana JF kwa aliyewahi kufika ofisi za msajili wa makampuni, mnaonaje hadhi ya lile jengo?

Jee ofisi muhimu kama hii ya msajili wa makampuni inastahili kweli kuwemo katika lile jengo? Hivi kweli kama umempata mbia wako toka nje ya nchi utakuwa tayari kwenda naye kwenye lile jengo au utakwenda peke yako?
 
Vipi wana JF hakuna aliyefika jengo zilipo ofisi za msajili wa makampuni (BRELA)?
 
heheh kitawaka moto siku kipoteze kumbukumbu zoteee watu wanyang'anywe makampuni unachezea CCM!
 
Inaelekea wengi mliomo humu hata sehemu ambayo makampuni au majina ya biashara yanasajiliwa hamjui, mnafanya Internet cafe au?
 
Mimi mwenyewe nilishangaa nilipofika kwenye hilo jengo ,nikashangaa saaana kwani nuiliuwa naona mashangingi yameandikwa BRELA ,na kwa uwingi wa hayo mashangingi nikajua pia hata ofisi zao zina hadhi loh kumbe ni tofauti kwanza sikuamini kwa kuwa sasa Brela ni wakala wa serikali kama ilivyo RITA,EWURA, n.k hata vitendea kazi vyao hapo ofisini vimechoka mbaya ,mafaili yamezagaa chini,kumbukumbu hakuna hata samahani hakuna ,kwa kweli ni ajabu kwani hao Brela wanashindwaje kukarabati ofisi yao ili hali wanaweza kununua mashangingi kibao,ni aibu kubwa hata ukienda na mgeni hapo anajua kama hiyo ni ofisi ya matapeli,kingine hapo ofisini hakuna nidhamu kabisa kwani kwenye vibaraza utakuta wamejaa vishoka a.k.a matapeli kazi yao kuuliza una shida gani, na hujidai wao wanawajuwa wakubwa wa mle mjengoni kwa hiyo toa kitu kidogo shida yako inatatuliwandani ya siku mbili tu badala ya mwezi.Nilipotoka hapo nikapata mafua kutokana na mivumbi na hewa nzito iliyopo hapo ofisini,hawa jamaa inabidi tuwapeleke Ngurdoto wakapate semina endelevu huenda ndio watajua wajibu wao
 
Huo mjengo unalifti ambayo inahitaji rubani kuiendesha. Jamaa sijui kaajiriwa na BLERA kama dereva wa 'lift'. Hureey ajira milioni moja.
 
Ni vizuri kama umejionea hilo, ukiambiwa utoe ushauri utawaambia nini BRELA?
 
Na kweli katika ajira 1,000,000 atakuwa anadaiwa 999,999
 
BRELA wanatakiwa wabadilike kiutendaji na pia wawe computerized mtu akienda kufanya search iwe ni swala tu lakuretrieve information na sio mpaka ukatafute file mara docs nyingine hazipo.........
 
Waliwahi kutangaza tenda ya computerization lakini bado mafaili yamemwagwa kwenye sakafu
 
Waweke kwenye mtandao thubutu,kwani vijisenti vya rushwa watavipataje?mambo yote ana kwa ana kwenye korido chafu pale jengo la Washirika,hapo Brela rushwa ni haki yao toka chini kwa mfagizi hadi juuuu
 
Na vipi kama wange decentralise huduma yao kikanda kama ilivyo idara ya kutoa hati ya ardhi?
 
Ni vizuri kama umejionea hilo, ukiambiwa utoe ushauri utawaambia nini BRELA?

Wawe na mpango wa muda mrefu wa kujenga makao makuu ya ofisi na baadaye kufungua ofisi za kikanda kama ilivyo Idara ya Ardhi ili mwananchi wa kawaida awezi naye kusajili biashara yake bila ya usumbufu wa kusafiri mpaka Dar es Salaam.
 
Jamani naombeni mwenye anwani na namba za simu za EWURA anisaidie maana kwenye website yao hakuna kitu
 
Back
Top Bottom