Hadhi na muda muafaka wa kuvaa Joho la Mahafali (graduation gown)

Shukuru

JF-Expert Member
Sep 3, 2007
748
15
Jamani wadau wa elimu hususani hapa Tanzania... hivi huu mtindio wa watoto wadogo ku-graduate from baby-school to pre-primary school then mtoto anavalishwa joho ya rangi ya dam ya mzee na weusi flani hivi au juu katilia kofia ya draft kama mkufunzi wa chuo kikuu..

Akimaliza primary anavaa tena, akifaulu form two anavaa kuingilia form three... mara kufilia form four anavaa tena... form six hali kadhalika... mbaya zaidi naona wanosoma food and hotel management nguo hizo hizo... mmh nasikilizia veta-drivers.m echanics... etc

Jamani huku si kudhalilisha elimu hapa tanzania?

its better kama kila level na type ikawa na mavazi yake...

Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?

Salaam wanajamvi...
Tangu kuanzishwa kwa soko huria ktk elimu ya TZ hususan, uanzishwaji wa shule zenye majina luluki, mf. International schools, Academy, English medium schools, St.so and so, etc,etc... Kumezuka uvaaji wa Joho la Mahafali (graduation gown) hata kwa wanafunzi wanaomaliza masomo ya chekechea, au elimu ya msingi au sekondari.

Kwa mtazamo wangu Joho lina hadhi kubwa na livaliwe wakati mwanafunzi amehitimu elimu ya chuo kikuu na anapotunukiwa shahada (Degree, Masters, PhD) ili kuhamasisha watoto wetu kusoma kwa bidii kufikia kiwango cha juu cha elimu. Hivyo, wakati wa kumaliza masomo ya chekechea, au elimu ya msingi au sekondari, wanafunzi wavae sare zao za shule na sio kushonewa majoho.

Nawasilisha........

Nakumbuka miaka ya 90 nilipokua mtoto nilikua nikiona picha ya mtu aliye vaa joho basi moja kwa moja wazo lilikua likinijia ni Je mtu huyo ame graduate degree ya nini.

Joho lilikua ni kwa ajili ya wahitimu wa vyuo vikuu hali iliyokua inalipa heshima Joho, tulikua tunatamani sana kufika huko ili na sisi tuvae Joho.
Lakin sasa hivi nimefuatilia hasa mkoa wa Dar es salaam Joho limekua ni vazi kwa yeyote anaye hitimu bila kujali level yake.

Hata kindergarten graduates nao wana vaa joho, joho limepoteza hadhi yake. Bila kujali aina ya Joho bado sioni kama ni vema kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita kuvaa majoho.

Sijui kama kuna chombo chenye kusimamia hili lakini ni vema Joho likabaki kutumiwa kwa graduates wa Vyuo vya elimu ya juu ili kuleta heshima ya Joho

NAWASILISHA
 
Hata chekechea wanavaa!!! kweli maana inapungua. Zamani wakati sijaikwaa degree, nilikuwa nasema nasotea gwanda.cjui cku hizi wanasemaje!
 
Jamani wadau wa elimu hususani hapa Tanzania... hivi huu mtindio wa watoto wadogo ku-graduate from baby-school to pre-primary school then mtoto anavalishwa joho ya rangi ya dam ya mzee na weusi flani hivi au juu katilia kofia ya draft kama mkufunzi wa chuo kikuu.. akimaliza primary anavaa tena, akifaulu form two anavaa kuingilia form three... mara kufilia form four anavaa tena... form six hali kadhalika... mbaya zaidi naona wanosoma food and hotel management nguo hizo hizo... mmh nasikilizia veta-drivers.m echanics... etc

Jamani huku si kudhalilisha elimu hapa tanzania?

its better kama kila level na type ikawa na mavazi yake...

Kweli haileti mantiki kutumia majoho kila ngazi ya elimu kwani awali uvaaji joho wakati wa mahafali ilikuwa alama ya kufuzu chuo kikuu. Sasa joho limechakachuliwa na kuwa alama ya kufuzu kiwango chochote cha elimu.

Lakini huku si kudhalilisha elimu bali ni kudhalilisha alama hiyo ya elimu (joho). Kwa bahati nzuri elimu ya mtu inabaki kichwani akivaa au asipovaa hilo joho.
 
Kwani hayo majoho maana yake ni yanavaliwa na watu wanaomaliza chuo tu?
ndiyo maana yake?
lile ni vazi tu kuonyesha umoja na mfanano,kwenye watu wengi hasa katika sherehe za kuhitimu mafunzo. waacheni watoto wafurahie mavazi hayo. acheni hizo bwanaaaa. msifananishe wakati wa zamani na sasa. "wakati ni ukuta ukipambana nao utaumia mwenyewe".
 
Hakuna ubaya wowote kwa watoto kuvaa majoho hiyo inawapa changamoto zaidi ya kuendelea mbele zaidi.
 
Kwa kuwa watu walibuni kuwa mtu akimaliza chuo ndio avae joho.. tena wote wavae sare.. basi mimi naona kuna namna wao walifikiria jinsi ya kuwatenganisha wale waliohitimu na wale ambao bado hawajahitimu.... na kuwapa hamasa zaidi kwa wale walio chini yao kufanya bidii hadi kufikia hatua ya hao ndugu zao wenye majoho... suala la msingi hapa ni demacation inayopatikana kati ya wakufunzai na waru wengine.. so kwa kuwa kulikuwa kuna umuhimu wa kuwatenganisha japo KIMAVAZI na raia wengine.. basi watu wangeheshimu demacation hiyo ili kuendelea kuwapa heshima... ni sawa na sare za polisi.... polisi wana sare tofauti tofauti kwa vitengo tofauti... nafikiri tuige mfano huo...
 
Salaam wanajamvi...
Tangu kuanzishwa kwa soko huria ktk elimu ya TZ hususan, uanzishwaji wa shule zenye majina luluki, mf. International schools, Academy, English medium schools, St.so and so, etc,etc... Kumezuka uvaaji wa Joho la Mahafali (graduation gown) hata kwa wanafunzi wanaomaliza masomo ya chekechea, au elimu ya msingi au sekondari.
Kwa mtazamo wangu Joho lina hadhi kubwa na livaliwe wakati mwanafunzi amehitimu elimu ya chuo kikuu na anapotunukiwa shahada (Degree, Masters, PhD) ili kuhamasisha watoto wetu kusoma kwa bidii kufikia kiwango cha juu cha elimu. Hivyo, wakati wa kumaliza masomo ya chekechea, au elimu ya msingi au sekondari, wanafunzi wavae sare zao za shule na sio kushonewa majoho.

Nawasilisha........
 
Naomba kutofautiana na wewe mkuu! Mie kwa upande wangu sioni kama joho ni motivating factor ya kufanya watoto wetu kutamani kusoma elimu ya juu. Manake tukifikia kukataza majoho tunaweza kwenda mbali zaidi na kusema kuwa shule za chekechekea, msingi na sekondari zisiwe za ghorofa ziendelee kuwa zile zile zisizokuwa na milango wala madirisha na watoto waendelee kukaa chini ili kuwafanya watamani kukalia madawati na kupanda maghorofa watakapokwenda elimu ya juu! Haya ni mawazo mgando!

Nadhani wasomi wenzangu tukiongea na kutenda mambo yetu kisomi basi ata watoto watatamani kusoma elimu ya juu ili watambulike kwa usomi wao. Kwani ata sasa watu wanatamani kuwa kama Prof. Chachage (RIP), Prof. Haroub Othman (RIP), Prof. Shivji na wengineo wengi sio kwa sababu waliona wamevaa majoho bali walijipambanua kwa usomi wao! Nadhani nimesomeka!
 
Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?
 
Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?

Mkuu umefanya vizuri kulileta hili swala kiukweli mimi mwenyewe naumia sana nianapo Elimu ya Tanzania inazidi kuvurgwa kuanzia kwenye vazi la tukio maaalumu hadi ufundishaji, Inasikitisha sana kuona mtoto hata wa kidato cha nne au cha sita amevaa JOHO la watu wanaopewa shahada. Swala kama hili hapa inatakiwa lipigwea marufuku kabisa kwa hawa wamiliki wa shule binafsi kwani ndio wanaoongoza kufanya huu upuuzi wa kuvaa hili vazi kwenye mahafali yao,

Juzi nilisikitika sana kuona mwanataaluma wa UDSM na Mmiliki wa shule ya Perfect Dk Kadeghe akiwa amevaa vazi la graduates kwenye mahafali ya kidato cha 4 pale shuleni kwake, kwa hili huyu jamaa ameaibisha sana chuo kikuu cha DSM nilichokuwa naaamini kina wataaluma bora kutokana na michango yao.

Hivyo basi tuombe serikali yetu kupitia kwa Dk Kawambwa ipige marufuku kuvaa majoho kwenye shule za Vidudu, Msingi, Sekondari pamoja na vyuo vya certificates na dilpoma ili JOHO libaki kuwa special kwa University tuu!!!!
 
Tusubili zama za viongozi ambao wako seriuos ndo watalivalia njuga ili suala
Maana viongozi wengi wa sasa ata elimu zao ni za kughushi ooh Dr fulani kumbe feki.
Personally nashauri iwe kwa level ya chuo tuu ie form 6 mpka vidudu wote MARUFUKU!
 
KindergartenGraduation.jpg

What's the big deal with the grad gowns and hats? Are you trying force us to go back to those days (60s, 70s, and 80s) when these grad gowns and hats were only worn by UDSM grads????
Graduation gowns and hats can be worn by students of any level be it kindergaten grads, high school grads or college grads.
 
Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?
Joho maana yake nini (lina symbolize nini)?
 
Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?

Hosford-Kindergarten-Grad.jpg
 
Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?

Kindergarten-Graduation-2010.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom