Shukuru
JF-Expert Member
- Sep 3, 2007
- 748
- 15
Jamani wadau wa elimu hususani hapa Tanzania... hivi huu mtindio wa watoto wadogo ku-graduate from baby-school to pre-primary school then mtoto anavalishwa joho ya rangi ya dam ya mzee na weusi flani hivi au juu katilia kofia ya draft kama mkufunzi wa chuo kikuu..
Akimaliza primary anavaa tena, akifaulu form two anavaa kuingilia form three... mara kufilia form four anavaa tena... form six hali kadhalika... mbaya zaidi naona wanosoma food and hotel management nguo hizo hizo... mmh nasikilizia veta-drivers.m echanics... etc
Jamani huku si kudhalilisha elimu hapa tanzania?
its better kama kila level na type ikawa na mavazi yake...
Akimaliza primary anavaa tena, akifaulu form two anavaa kuingilia form three... mara kufilia form four anavaa tena... form six hali kadhalika... mbaya zaidi naona wanosoma food and hotel management nguo hizo hizo... mmh nasikilizia veta-drivers.m echanics... etc
Jamani huku si kudhalilisha elimu hapa tanzania?
its better kama kila level na type ikawa na mavazi yake...
Habari Wakuu. Mimi naona majoho yanashushwa thamani Tanzania. Haiwezekani mtoto akimaliza nursery, anavaa joho. Akimaliza la saba, anavaa joho. Akimaliza form 4, joho. At least form 6 basi unapoachana na uniform. Kenya majoho ni mpaka diploma au degree kuendelea. Mnaonaje hili?
Salaam wanajamvi...
Tangu kuanzishwa kwa soko huria ktk elimu ya TZ hususan, uanzishwaji wa shule zenye majina luluki, mf. International schools, Academy, English medium schools, St.so and so, etc,etc... Kumezuka uvaaji wa Joho la Mahafali (graduation gown) hata kwa wanafunzi wanaomaliza masomo ya chekechea, au elimu ya msingi au sekondari.
Kwa mtazamo wangu Joho lina hadhi kubwa na livaliwe wakati mwanafunzi amehitimu elimu ya chuo kikuu na anapotunukiwa shahada (Degree, Masters, PhD) ili kuhamasisha watoto wetu kusoma kwa bidii kufikia kiwango cha juu cha elimu. Hivyo, wakati wa kumaliza masomo ya chekechea, au elimu ya msingi au sekondari, wanafunzi wavae sare zao za shule na sio kushonewa majoho.
Nawasilisha........
Nakumbuka miaka ya 90 nilipokua mtoto nilikua nikiona picha ya mtu aliye vaa joho basi moja kwa moja wazo lilikua likinijia ni Je mtu huyo ame graduate degree ya nini.
Joho lilikua ni kwa ajili ya wahitimu wa vyuo vikuu hali iliyokua inalipa heshima Joho, tulikua tunatamani sana kufika huko ili na sisi tuvae Joho.
Lakin sasa hivi nimefuatilia hasa mkoa wa Dar es salaam Joho limekua ni vazi kwa yeyote anaye hitimu bila kujali level yake.
Hata kindergarten graduates nao wana vaa joho, joho limepoteza hadhi yake. Bila kujali aina ya Joho bado sioni kama ni vema kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita kuvaa majoho.
Sijui kama kuna chombo chenye kusimamia hili lakini ni vema Joho likabaki kutumiwa kwa graduates wa Vyuo vya elimu ya juu ili kuleta heshima ya Joho
NAWASILISHA