Hadhi na matumizi ya nembo ya taifa (Coat of arms)

The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
6,003
3,269
Wakuu
Natumaini sote tunaifahamu nembo ya taifa (Coat of arms). Kuna vitabu vya watoto wa shule ya msingi vimeelezea hiyo nembo na wapi inawekwa. Watoto wetu wanafundishwa jambo jema huu ya hilo.

Pia mimi binafsi nadhani nembo ya taifa ni kitu cha heshima na kipekee; ndio maana utaikuta Ikulu au kwenye magari ya raisi; na sehemu zingine za kidola (state) au serikali.

Lakini kuna siku nilikuwa nasafiri kwa mwendokasi Dar. Nilishtuka kidogo kuiona hii nembo ipo kwenye vituo vya mwendokasi barabara ya Morogoro. Nimejaribu sana kuwaza kama hili ni sawa. Sijui members mnasemaje kuhusu kuiweka alama hii muhimu kwenye vituo vya mwendokasi.
 
Tuna kasi sana na kwa spidi hii kuna siku utakuta Bendera ya Taifa kwenye mitumba huko Kariakoo.
 
Babu, hizi ni symbols tu. Ni alama siovitu vitukufu.
Tunatakiwa kuchukulia serious mambo ya muhimu yanayohusu maendeleo ya "Watu". Mambo ya haya matambara hayamsuidii mtanzania kupata decent job, or decent earning.

Ni sawa na kuhangaika na wimbo chura au mwanaume mashine. Sijui inasaidiaje umasikini, maradhi na ujinga.
 
Kwa hiyo nembo ya taifa ni sacrosanct zaîdi ya bendera? Huwezi kuŵa na bumper sticker ya nembo ya taîfa?
 
Ata bendera ya Taifa kila mtu apewe au anunue tu mbona nchi nyingine wanazo.Mi napenda niwe nayo kwangu sebuleni..sheria nyingine
zinatakiwa zilegezwe..cha msingi ni utiifu na kuijali
 
Hapana mkuu. Maendeleo ya watu yana nafasi yake. Na hizi national symbols zina nafasi yake. Usihamishe context ya mjadala.
Nilikutana na jamaa mmoja, kila nikianzisha mada fulani, utasikia: Itasaidia kupata mlo wa leo? Hii ni akili ya kimaskini.
Tuongelee vitu kadiri ya muktadha (context).
 
Ata bendera ya Taifa kila mtu apewe au anunue tu mbona nchi nyingine wanazo.Mi napenda niwe nayo kwangu sebuleni..sheria nyingine
zinatakiwa zilegezwe..cha msingi ni utiifu na kuijali
Unamkumbuka yule mbwiga aliyeifanya bendera ya taifa kuwa pazia?!..alienda jela
 
Kwa hiyo nembo ya taifa ni sacrosanct zaîdi ya bendera? Huwezi kuŵa na bumper sticker ya nembo ya taîfa?
Sijui kama uko nchini au wapi. Presence ya bendera ya taifa na nembo ya taifa wala havilingani. Labda umewahi kuona nembo ya taifa wapi? Panahesabika.
Na zaidi vitabu viinavyotumika kwenye syllabus kwenye shule za msingi vimeainisha kabisa wapi unaikuta nembo ya taifa.
It will be interesting mtoto akijibu ipo kwenye vituo vya mwendokasi.:D:D:D
 
Wakuu
Natumaini sote tunaifahamu nembo ya taifa (Coat of arms). Kuna vitabu vya watoto wa shule ya msingi vimeelezea hiyo nembo na wapi inawekwa. Watoto wetu wanafundishwa jambo jema huu ya hilo.

Pia mimi binafsi nadhani nembo ya taifa ni kitu cha heshima na kipekee; ndio maana utaikuta Ikulu au kwenye magari ya raisi; na sehemu zingine za kidola (state) au serikali.

Lakini kuna siku nilikuwa nasafiri kwa mwendokasi Dar. Nilishtuka kidogo kuiona hii nembo ipo kwenye vituo vya mwendokasi barabara ya Morogoro. Nimejaribu sana kuwaza kama hili ni sawa. Sijui members mnasemaje kuhusu kuiweka alama hii muhimu kwenye vituo vya mwendokasi.
Nadhani wamedhamiria kuonesha hizo ni ofisi za umma na si mradi wa mtu binafsi
 
Sijui kama uko nchini au wapi. Presence ya bendera ya taifa na nembo ya taifa wala havilingani. Labda umewahi kuona nembo ya taifa wapi? Panahesabika.
Na zaidi vitabu viinavyotumika kwenye syllabus kwenye shule za msingi vimeainisha kabisa wapi unaikuta nembo ya taifa.
It will be interesting mtoto akijibu ipo kwenye vituo vya mwendokasi.:D:D:D
Tuwekee hizo aya hususan za syllabus ya Primary School. Halafu nikuulize hiyo sheria ilietwa mahsusi kwa Wanafunzī wa Shule za Msingi na kushushwa kwenye text- books za Shule ya Msingi, au?
 
Ata bendera ya Taifa kila mtu apewe au anunue tu mbona nchi nyingine wanazo.Mi napenda niwe nayo kwangu sebuleni..sheria nyingine
zinatakiwa zilegezwe..cha msingi ni utiifu na kuijali
Very good.. hii inakumbusha why nchi kama USA utaona wananchi walivyo na "ownership" ya bendera yao na Utaifa..huko kwetu nembo na bendera inaonekana ni mali ya serikali..
 
Mm nimeweka hiyo kitu pqmoja na bendera ya taifa chooni kwangu. Kwani kuna nini?
 
Back
Top Bottom