Habinder Sethi aomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabiri ya Uhujumu Uchumi

Kweli kamanda! Enzi zile kabla CHADEMA haijabadili gia angani na kuanza kuwa mtetezi wa MAFISADI.
Sina chama wala sitakuwa na chama naona kuwa na vyama ni kama mdundiko hapa nchini. No one is serious. Naongea kuangalia data basi.
 
Habinder Seth, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha, wakili wake Michael Ngalo ameieleza Mahakama ya Kisutu leo.

---
Harbinder Sethi anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ameandikia barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukiri makosa yake na kuomba msamaha

Wakili wake, Michael Ngalo amesema hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipotajwa

Sethi, Mwenyekiti Mtendaji wa PAP pamoja na James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa VIP wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar, Afrika Kusini, Kenya na India

Wakili wa Jamhuri, Wankyo Simon ameeleza kuwa wamepokea barua ya Seth wanaifanyia kazi na majibu yatatolewa ila kuhusu upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika

Miongoni mwa mashtaka yao ni kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Tsh. Bilioni 309.

Shetani ndio alikuwa anamtaka huyu na Rugemalila, yaani hapa atakuwa katumia mpaka mateso kumlazimisha duniani hamna siri, itajulikana tu.
 
Njia nzuri ya baraka ilikuwa ni kuharakisha upelelezi wa kesi zao na ushahidi kuwekwa mahakamani. Unawezaje kuwaweka watu mahabusu zaidi ya miaka 3 eti upelelezi haujakamilika! Hii ni "saikolojikol tocha" na makusudi na kuwaumiza binadamu wenzako.

Kama huyo binadamu mwenzangu ni mwizi acha aumizwe tu. Hamna namna. Jino kwa jino
 
Kama huyo binadamu mwenzangu ni mwizi acha aumizwe tu. Hamna namna. Jino kwa jino
Hahahaha. Sawa mkuu. Lakini kama tunasema nchi yetu inafuata utawala wa kisheria sio jambo jema kutokukamilisha upelelezi miaka 3+ wakati kila siku wapelelezi wanakwenda kazini.
 
Njia nzuri ya baraka ilikuwa ni kuharakisha upelelezi wa kesi zao na ushahidi kuwekwa mahakamani. Unawezaje kuwaweka watu mahabusu zaidi ya miaka 3 eti upelelezi haujakamilika! Hii ni "saikolojikol tocha" na makusudi na kuwaumiza binadamu wenzako.
Hili shtaka la ML ukilitazama limekaa kimkakati sana. Makosa mengine yamewekewa ukomo wa investigation na kuna kipengele kinaipa mahakama mamlaka ya kufuta kesi kama upelelezi haujakamilika ndani ya muda huo. Kuonesha huruma ya dhati, badala ya kusubiri miaka 3 au zaidi watu wakisota ndani ndio wasamehewe, ni vema hili kosa nalo liwekewe ukomo wa muda wa uchunguzi/upelelezi kama mengine na lidhaminike. Wema tunaouona ukigeuzwa kua sheria utaleta mantiki zaidi badala ya kua hisani
 
Mitambo yake ya kufua umeme bado inatumiwa na TANESCO akitoka jela anaanza kuingiza pesa kama kawaida.

Waliokuwa wanazila pesa zake alipokuwa jela wanajiharia saa hizi.
 
Katubu!! Kweli hakuna jiwe litalosalia juu ya jiwe labda yule mmakonde ambae anasema hawezi kuchenji buku kwaajili ya njaa ya mtoto
Wanawezaje kumtumia wakati maagizo yanaweka wazi kuwa baada ya kutubu dhambi zake zinakua nyeupe kama theluji😊😊😊
 
Hata yeye katiba inasema kwa makosa aliyofanya kabla ya kuwa Rais anastahili kushtakiwa nayo.
Akitoka madarakani wanaye!View attachment 1228328
Huwezi kumchafua Rais Magufuli kwa issue hiyo. Kwanza ni aibu kusema kati ya nyumba zooooooooote alizouza eti ka apartment ka vyumba viwili na sebule ndio ufisadi. Mngeliweka majumba ya Masaki, Msasani, Uzunguni Bukoba Mjini au Isamilo, Capri Point Mwanza kuwa ndio kayafisidi kuwa yake au ndugu zake ningeelewa. Lakini mnatuletea ka apartment ka Ubungo? Eti ufisad?
 
Back
Top Bottom