Habinder Sethi aomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabiri ya Uhujumu Uchumi

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
664
1,272
Habinder Seth, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha, wakili wake Michael Ngalo ameieleza Mahakama ya Kisutu leo.

---
Harbinder Sethi anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ameandikia barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukiri makosa yake na kuomba msamaha

Wakili wake, Michael Ngalo amesema hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipotajwa

Sethi, Mwenyekiti Mtendaji wa PAP pamoja na James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa VIP wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar, Afrika Kusini, Kenya na India

Wakili wa Jamhuri, Wankyo Simon ameeleza kuwa wamepokea barua ya Seth wanaifanyia kazi na majibu yatatolewa ila kuhusu upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika

Miongoni mwa mashtaka yao ni kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Tsh. Bilioni 309.

IPTL+PIC.gif
 
Habinder Seth, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha, wakili wake Michael Ngalo ameieleza mahakama ya Kisutu leo
Kafanya la maana Sana akitutajia aliowagawia rushwa na kutupatia vielelezo wamwachie maramoja, tkkr mtumieni huyu Kama shahidi namba moja.
 
Back
Top Bottom