Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu,

Huenda Kabendera akawa huru leo baada ya Hati ya Mashtaka kufanyiwa marekebisho.

Baada ya Erick Kabendera kukubali makosa, Upande wa Serikali wamemsomea Mashtaka Rasmi.

Mashtaka hayo ni pamoja na Uhujumu Uchumi pamoja na Kukwepa Kodi baada ya kosa la kuongoza Genge la Uhalifu kuondolewa Rasmi na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

UPDATE:

Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) ameridhia maombi ya mwandishi wa habari, Erick Kabendera kukiri mashtaka yake na kuomba msamaha. Alikuwa anakabiliwa na mashtaka 3 likiwemo la kutakatisha fedha, TSh. Milioni 173.

Aidha, DPP amewasilisha hati ya kuiruhusu Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi huyo.

=====
FINAL UPDATE:

Kabendera aachiwa huru
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemuachia huru mwandishi wa Habari za Uchunguzi Erick Kabendera.

Katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Janeth Mtega imemtaka mtuhumiwa Erick Kabendera kulipa kiasi cha pesa za kitanzania shilingi laki mbili na elfu 50 (250000) au kutumikia kifungo cha Miezi mitatu jela. Adhabu hiyo inaambatanana fidia ya Shilingi za kitanzania Milioni 172, hii ni kwa kosa la kushindwa kulipa kodi.

Kosa la pili limemtaka Erick Kabendera kulipa faini ya shilingi za kitanzania Milioni mia Moja (Mil 100) hii ikiwa ni adhabu kwa kosa la Utakatishaji fedha katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili.

16A6D596-3DAE-4074-8DFC-8168F3154163.jpeg

5493AD2E-1A05-4936-B298-FA7A1D0C15CB.jpeg

22C547CD-3507-41D1-A189-FD5B497C713B.jpeg

B1D5DA7E-A81D-44BD-87BA-55E7D2C0537B.jpeg

EBB685A3-0D8D-4EF7-909C-715656EC8B9A.jpeg


======
Agreeement

B8201E7E-F5F3-43E1-AF42-18F63E1A1BCF.jpeg

4D611283-F76B-47C5-87FF-42E5CDEF05A0.jpeg

E6F1C9C5-494B-4ACB-84B6-3285059140FF.jpeg

219974BA-B848-427C-99B7-1641DF321B41.jpeg

96EA6B68-C1E0-484B-81B8-536B4D743C24.jpeg

6974E89C-FCDB-40A3-BC20-8AC184FAB530.jpeg



=====

Pia, soma:
1). Kisutu: Erick Kabendera afikishwa mahakamani, upelelezi dhidi yake haujakamilika

2). Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

3). Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera aomba msamaha kwa Rais Magufuli
4). Rais Magufuli: Waliopo mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi, kama wapo tayari kuomba msamaha na kurejesha pesa, kama Sheria inaruhusu nashauri waachiwe
1582539179988.png
 
Kuvujisha siri za serikali yoyote duniani ni sawa na kuisaliti nchi husika.
Afanyae mchezo huo adhabu yake ndogo kabisa ni kukaa jela maisha yake yote,mara nyingi hua ni death sentence tu.

Naiomba serikali isifanye ajizi kwa yoyote yule atakaebanika kuhujumu serikali kwani atakua kahujumu nchi kwa ujumla.

Serikali hupatikana kwa njia ya uchaguzi hivyo afanyae hujuma huathiri ufanisi kwa wananchi walioiweka serikali hiyo na nchi kwa ujumla
 
Sasa kwa nini wameondoa baadhi ya mashitaka kama kutakatisha fedha na kuongoza genge la kihalifu? Huku si ndio tunasema kubambikiwa kesi?

Haraka za kumbandikia makosa ya urakatishaji fedha na kuongoza genge la uhalifu zilikuwa za nini? Ni afadhali wangeanza na makosa madogo na kisha kurekebisha na kumwekea hayo makosa yasidhaminika.

DPP na polisi wanaichafua serikali. Wasiwasi wa wananchi, wanarakati, watetezi wa haki za binadamu na mabalozi waliopo nchini walikuwa na mashaka na hii kesi kuanzia namna polisi walivyomkamata kama 'watu wasiojulikana' , haya mabadiliko ya mashitaka yanadhihirisha huo 'ubambikizwaji' wa kesi dhidi ya Kabendera.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakatanta,
Hivi mtu kama Kipilimba, Rajabu Luhavi na wengineo walioshika sensitive post za kuwa kwenye inner circle ya Raisi kuna kipi wasichokijua kuhusu Tanzania.

Halafu watu kama hao ukawape nafasi za ubalozi nje ya nchi bila kujua huko watakutana na nani tena kirahisi tu with official meetings after all they are humans na hizo ndio asset watu wanazozitaka.

Hao watu usione shida kukaa nje ya nchi maandishi ya Kabendera ndio uone risk to National security.

Hakuna mtu mwenye shida ya kuhujumu nchi ambayo ni heavily dependent on aid; wakifuta misaada tu ni sanction tosha.
 
Back
Top Bottom