Habibu Mchage na demokrasia ndani ya vyama vya siasa

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
HABIB MCHANGE AWALIZA WANACHADEMA MWANZA, WASHINIKIZA ASIONGEE UKWELI KUHUSU MGOGORO WA CHADEMA, HOJA ZAKE ZATEKA KONGAMANO.

Nilipata fursa ya kuhudhuria kongamano lililofanyika Mwanza hotel Jana. Nilishuhudia wanachama wa chadema M4C group Mwanza wakilizwa hadharani na mwanasiasa kijana Bw. Habibu mchange. Wanachama hao walilizwa na kupanikishwa na Bw. Mchange wakati wa kongamano lililokuwa likijadili mada isemayo (Kuelekea 2015, migogoro ndani ya vyama vya siasa je, inajenga democrasia?)

Katika mdahalo huo Bw. Habib mchange alikuwa mmoja wa watoa mada, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumuona mwanasiasa huyu aliyejitambulisha kama mjumbe wa taasisi ya Alliance for development organization (ADO) Mchange alitoa mada kuhusu Hali ya siasa nchini, tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Katika mada hiyo ambayo Bw. Mchange aliiwasilisha kwa umahiri mkubwa huku akitoa mifano hai ya migogoro mbalimbali ya kisiasa iliyowahi kutokea nchini, uwasilishaji wake ulivutia wanakongamano kumsikiliza kwa makini na kushangilia hoja alizokuwa akizijenga kwa utaalam wa hali ya juu, hoja zilizojaa mashiko,weledi na uhalisia.

VILIO NA JAZBA ZA WANACHADEMA M4C

Muda wote ambao Habib Mchange alikuwa akijenga hoja zake alikuwa akishangiliwa na umma wote wa wanakongamano kwani alikuwa akieleza mifano hai kutoka kwenye vyama vingine mbali ya chadema. Hali ilibadilika pale Bw. Mchange alipoanza kuzungumzia uhalisia wa chadema akifananisha na kutofautisha mifumo ya vyama viwili Chadema na CCM in institutional context, pia alifananisha migogoro mbalimbali iliyowahi kutokea katika vyama vingine vya siasa na ule wa chadema, hapa wanachadema wakaanza kuleta fujo kwa kubwabwaja bila utaratibu ukumbini wakitaka msemaji huyo asiendelee kusema walipoona anaendelea kusema wapo waliotoa machozi na kuondoka kwa hasira wakiongozwa na Katibu wa M4C kanda ya ziwa Bw. Humphrey Mhada ambaye aliondoka akiwa anafoka huku akitokwa povu na machozi hali iliyowalazimisha wanakongamano kumzomea.

Wengine waliokuwa wakifokafoka bila hoja ni pamoja na Andrew Kaniki na Meshack Micus Michael anayejiita afisa vijana kanda (cheo ambacho hakipo kikatiba, Meshack ni kijana wa Lema (Mhaya anayejiita mchaga kwasababu tu wachaga wameonesha kuwa na nguvu zaidi kwenye Chama chake) Pia kulikuwa na mama mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Lina mama huyu alikuwa kivutio kwenye kongamano kwani hoja za mchange zilimfanya mama huyu achanganyikiwe kabisa na kuvimba macho, akawa anaropoka hovyo akizunguka ukimbini mpaka sauti ilipomkatika lakini bado aliendelea kuongea kwa ishara alipoona hakuna anayemjali alijiondokea.

Mwenyekiti alilazimika kumkatisha Bw. Mchange kwa muda kutokana na vurugu iliyoanzishwa na wanaM4C waliojazwa upepo. Wanachadema hawakuwa tayari kusikia uhalisia ambao Mchange alikuwa akiueleza hasa kuhusu kiasi na matumizi ya ruzuku ya chadema, wakitoa hoja dhaifu kuwa mtoa mada huyo ametumwa. Cha ajabu wakati wa kuchangia mawazo hakuna mwana chadema aliyepinga hoja yoyote iliyotolewa na Bw. Habib zaidi ya kutumia hoja moja tu kuwa mgogoro wa chadema umesababishwa na ccm.

BAADHI YA HOJA ZA MCHANGE ZILIZOONEKANA KUWA MWIBA KWA CHADEMA

1. Mchange alisema migogoro ya vyama vya siasa mara zote imekuwa inatokana na maslahi binafsi ya viongozi wa chama hasa zinapokalibia chaguzi. Alionesha masikitiko yake kwa CDM kupoteza halmashauri kwa migogoro dhaifu isiyo na tija.

2. Mchange alionesha kukerwa na vyama vya upinzani kujiendesha kama kampuni binafsi kwa kuwabandika lebo ya usaliti vijana wote wanaoonekana kuwa na fikra mpya ndani ya vyama hivyo badala ya kujiendesha kama taasisi.

3. Mchange alisema watu wasitafute mchawi kutoka CCM kwani mgogoro wa chadema umesababishwa na wanachadema wenyewe kutokana na vita ya madaraka. Alisema jina msaliti litamkuta mwanachadema yeyote Yule atakayekuwa na fikra chanya zinazokinzana na viongozi wa juu wa CDM.

4. Mchange alihoji uhalali wa viongozi wa chedema kukataa matamko na misimamo inayotolewa na wanachama wao kwa kigezo kuwa vyeo vyao havipo kwenye katiba ihali wao wanajiita viongozi wa M4C kitu ambacho hakipo kikatiba. Baada ya kulisema hili kuna wanakongamano walioibua hoja kuwa M4C iliundwa kutafuta chakula cha Lema akiwa nje ya Bunge ndio maana mahesabu yake hayajawahi kuwekwa wazi na uchangishaji wa pesa umesitishwa baada ya Lema kurudi bungeni.

5. Mchange alimaliza kwa kusema kuwa "Kama chadema kimeshindwa kuwatendea haki wanachama wake, kamwe hakiwezi kuwatendea haki wananchi"

MCHANGE ALIVYOSHAMBULIWA KAMA MPIRA WA KONA BAADA YA KUMALIZA KUONGEA

Mara baada ya kumaliza kuongea kwa mara ya pili akiwa anahitimisha, Bw. Mchange alizongwa na zaidi ya robo tatu ya wanakongamano hali iliyoleta tafrani katika ukumbi wa kongamano. Wanakongamano hao walikuwa wakimzonga mchange wakitaka awapatie mawasiliano yake ya simu, hii ni kutokana na umahiri, ujasiri na msimamo aliouonesha Mchange kwa wanamwanza toka mwanzo mpaka mwisho wa kongamano kwani aliposimama kuongea kwa mara ya pili mchange aliongea kwa zaidi ya nusu saa kutokana na wananchi kumshinikiza mwenyekiti kutomnyang'anya kipaza sauti mwanasiasa huyo.

Katika maisha ya binadamu Mwenyezi Mungu hutoa watu,wachache sana,wanaojitoa mhanga na kubadili historia na maisha ya wengine.Kwa sasa Mchange amekuwa gumzo hapa Mwanza kutokana na uwezo wake na elimu aliyoitoa kwa watu jana. Wanachadema M4C wanahaha kumchafua kwa hoja dhaifu lakini umma uliosikiliza hoja zake umepata elimu ya kutosha kuliko siasa nyepesi za wanachadema wa M4C.

NI KWELI ZITTO AMEWAPONZA VIJANA WENGI NDANI YA CHADEMA, WENGE WAMEPOTEZA NDOTO ZAO, LAKINI NI WAJIBU WA UONGOZI WA CHADEMA KUTAFUTA AU KUUNDA BARAZA LA WAZEE LA USULUHISHI ILI KUWASAIDIA VIJANA AMBAO NI NGUVUKAZI YA CHAMA CHETU, NI WAJIBU WA KILA MWANACHADEMA KUPIGANIA HILI.
 
Huyu Habib Mchange anafanya shughuri gani kujipatia riziki yake?

Maana hizi nguvukazi sasa zijielekeze kwenye uzalishaji mali.
 
1-+Nape.png


Siasa za maigizo...
 
Jifunze basi hata kuandika makala, huyo Mchange wako umemuandika zaidi ya mara mia, JF tunamjua kama ni salia, lilifukuzwa CHADEMA.

Unatuletea uzi mrefu kwa kurudia rudia jina la salia gamba ili iweje?
 
pengine alikuwa na hoja zenye nzito na zenye mashko ila uwasilishaji hapa kama ilivyo kwenye andko lako umekaa "KISHABIKI" zaidi.
 
maandiko yanasema hakuna aliyekuwa muimbisha sifa mbinguni kama lusifa alipolewa sifa akataka kumpindua mungu leo ni makarine toka atupwe dunian ,ata uwe mzuri vipi kama wewe umejaa tamaa ufai
 
Hivi ni huyu Mchange aliye-disco chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)?
 
Huyu Habib Mchange anafanya shughuri gani kujipatia riziki yake?

Maana hizi nguvukazi sasa zijielekeze kwenye uzalishaji mali.
Ni mfuasi mtiifu wa MNAFIKI MKUU (MM).
Ni mojawapo ya vile vi-M vidogo vidogo vya chini vilivyotajwa kwenye ule waraka uliokamatwa!!
 
Mchange Ni sawa NA debe tupu hanitishi hana sumu. Nakuonea huruma ulotumia muda wako kuandia uzandiki kumsifu Mchaga naamini unaitumikia ajira yako vyema buku saba chap unapata mlo WA siku
 
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo
 
ukiona watu hawachangii tambua unachokiuza hakiuziki

Kinachouzika kwa sasa hivi ni hiki hapa;

QUOTE=pcm;8030034]NINAVYOMFAHAMU ZITTO ZUBER KABWE
-KILIO CHA USALITI (Sehemu ya Jina Langu ni MTELA ALLAM MWAMPAMBA mwanachama mchanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),

Nikiwa ni Mwanachama wa CCM, nimeapa kwa Imani ya Chama Changu kuwa NITASEMA KWELI DAIMA NA FITINA KWANGU MWIKO. Kiapo hiki ni ndani ya Chama Changu, Serikali yangu na mbele ya Jamii yangu.

Kwa kuwa LENGO langu si KUFITINISHA wala KUJIHUSISHA NA CHAMA CHAKE, Nitabainisha (kwa Ufupi) namna ninavyomfahamu ZITTO ZUBER KABWE, tena ikibidi nitabainisha kinagaubaga na wazi wazi (kama italazimu kufanya Hivyo) kiasi Umma ubaini ni nani ZITTO ZUBER KABWE ndani ya Chama mjenzi, nguzo, mhimili ama mhujumu chama. Nafanya hivyo kwa lengo la kutetea maslahi ya Kitaifa, maana watu hawa wanabeba nembo na sura ya Utaifa, na ni ubaya ulioje watu wasio na DHATI ya kiutawala kuaminiwa katika Utawala. Na kwa bahati mbaya katika taarifa hiyo nimetajwa tena kwa jina langu kamili, hivyo jukumu la kunyoosha maelezo ya ZITTO ni la msingi na lenye msukumo Binafsi (Si chama Changu kwa namna yeyote) Ni kwa

SEHEMU HII YA KWANZA: Nakubaliana kabisa na Zitto kuwa hakukuwa na kikao ambacho kilitukutanisha Sisi Wanne pamoja, pale LUNCH TIME,hayo ni ya mwandishi mwenyewe, maana Mimi si chanzo chake. Lakini hiyo hainamaanishi kwamba sisi hatukuwa tukikutana.

Kama pamoja na yote ambayo yaliyopita na yanayoendelea CHADEMA hadi hivi sasa bado yupo anayeamini maneno ya ZITTO kuwa hamfahamu BEN SAANANE na kuwa anaweza kupishana nae njiani bila kumtambua na aendelee kuamini hivyo lakini nasema hiyo ni too much of exaggeration on his expressions.

kuondoka kwangu na wengine ni kafara ya jambo hilo. Kuna mambo si sahihi kuyaeleza kiundani na hadharani kwasababu tuliambizana na kupanga kwa Usiri na Kuaminiana, hatujafikia hatua hiyo ya kuuvunja hata Uamini tuliopeana kwa Viapo ila kama tutaendelea na maneno ya namna hii na UZANDIKI,

Karata yako ya mwisho inayo-determine maisha yako kama mwanachadema iko mikononi mwetu, Please brother, Don’t mess with your last poker chip, will lose the game. Kauli yangu Moja ya Ushuhuda inamaliza Uhai wako ndani ya Chadema.,

Mwisho kabisa katika signature yako ya JF umetumia nukuu ya Mwalimu Nyerere kwenye kitabu chake cha TUJISAHIHISHE cha mwaka 1962 mwaka mmoja baada ya Uhuru, kuwa UKWELI haupendi kupuuzwa puuzwa, soma tena kitabu hicho upate hazina ya mawazo ya kiutawala na uondokane na UNAFSI kwa tafsir ya Mwalimu Nyerere ya neno hilo katika kitabu hicho.[/QUOTE]

HAPO MTU UTAONGEZA NINI ZAIDI!?
 
mchange ndio mdudu gani?au ndio kale ka-houseboy ka briefcase nyekundu?kibaha wanasubiri siku kakanyage wakachanechane na viwembe
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom