Habari Zenu Wana JF

Karibu Bi Chausiku, mimi kwa jina naitwa Nyani Ngabu, meya mstahiki wa mji huu wa Jamiiforums.com. Nakukaribisha kwa mikono yote miwili na jisikie uko nyumbani. Endapo ukiwa na swali au maswali usisite kuniuliza kwani mimi ni mwenyeji wa siku nyingi tu hapa. Nimeshapitia kila aina dhoruba, misukosuko na mikikimikiki ya kila aina na ninazijua njia za hapa kama ninavyokijua kiganja cha mkono wangu kwa hiyo naweza kukwambia kwa uhakika kabisa ni njia ipi yenye makorongo na ipi ilonyooka.

Karibu sana.
 
Aisee nimecheka mpaka wageni wangu wameshtuka wanataka kujua kulikoni? lol! Nyani! hahahahahahahahahahah
 
Karibu Bi Chausiku, mimi kwa jina naitwa Nyani Ngabu, meya mstahiki wa mji huu wa Jamiiforums.com. Nakukaribisha kwa mikono yote miwili na jisikie uko nyumbani. Endapo ukiwa na swali au maswali usisite kuniuliza kwani mimi ni mwenyeji wa siku nyingi tu hapa. Nimeshapitia kila aina dhoruba, misukosuko na mikikimikiki ya kila aina na ninazijua njia za hapa kama ninavyokijua kiganja cha mkono wangu kwa hiyo naweza kukwambia kwa uhakika kabisa ni njia ipi yenye makorongo na ipi ilonyooka.

Karibu sana.

ila wewe una vituko
karibi Bi Chausiku
 
karibu bi chau!!!!!!!!!!mimi jina lako ndio limenihamasisha kukuaribisha katika ulimwengu huu.
 
Karibu Bi. Chau... kuna sehemu ya Ibada huku mama, unakaribishwa kuungama dhambi zako...:amen:
 
Naamini umezipata kwa uzuri habari za JF kabla ya kujiunga. karibu uwe mshirika mkamilifu.
 
Tangu nikaribishwa mwaka jana nimeingia jukwaa hili haizidi mara 5. Una baraka kukaribishwa nami . Karibu kweli na ujisikie huru kunitafuta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom