Nimeingia Dodoma; mtaji wa milioni nne naweza kufanya biashara gani?

mtemi tagallah

Senior Member
Apr 4, 2015
101
57
Nimekuja kuomba ushauri kwenu nina mtaji wa milioni nne naweza kufanya biashara gani Dodoma.

Nina ujuzi wa computer na uzoefu katika kutengeneza computer hadi chip level, kutengeneza simu sinauzoefu ila nimeshapata mafunzo kidogo.

Kichwani kwangu nina mawazo matatu moja kufungua mgahawa, mbili kufungua biashara ya kuuza mafuta ya kujipaka yaani losheni n.k, tatu kufungua ofisi ya ufundi computer. Naomba ushauri wenu wakuu.
 
Fanya utafiti wa eneo na uhitaji wa huduma wa hiyo namba 3 ambayo unauzoefu nayo.
 
Back
Top Bottom