Habari za vitisho kwa Madaktari ni za kutunga - Kibonde wa Clouds FM

Status
Not open for further replies.
Mi simlaumu sana Kibonde, i think he is making his life from the system ya sasa, no mater how smal it is. Clouds fm i hv hando n Anold. Hando with the orientation of the radio yet u can feel sences. Kayanda not details much bt u can get something also, he is always neutral. Kibonde, not detailed, skewed, dominant on things he doesnt kno.
Mzee wa porojo na misifa.
 
Katika kipindi chake cha jahazi leo jioni, Ephraim Kibonde amesema habari zinazoandikwa na magazeti ya kwamba kuna watu wamekwenda Afrika Kusini kwa lengo la kumdhuru Dk.Ulimboka na habari za vitisho wanavyopewa viongozi wa chama cha madaktari Tanzania (MAT) ni habari za kutungwa, na vyombo vya habari vinatakiwa kuthibitisha habari hizo kabla ya kuandika. mfano akasema habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 10 july 2012 ni habari ya kutungwa.
Naona huyu jamaa anazungumza upuuzi kama wa Stella Manyanya.

Huyu jamaa ukitaka kumjua kuwa ni mshika pembe msikilize kwenye mahojiano haya, yaani sura, mdomo na maneno havina ushirikiano, hasa kwenye swali la mgomo wa madaktari

 
Last edited by a moderator:
Kibonde ni mtumwa wa maGamba. Wamemtuliza kwenye pay role ya TBC na kipindi cha maisha ni nyumba. Hapo Clouds yupo Kama mamluki tu,Hilo watu wanalitambua. Kumshangaa huyu Kibonde ni sawa na kushangaa Mmamkonde akichonga kinyago.
 
Salaa wana JF.

Kwa masikitiko makubwa nimelazimika kuandika thread hii kuhusiana na tabia ambayo haiakisi weledi wa fani ya utangazaji inayooneshwa na mtangazaji wa clouds fm aitwaye Ephraim Kibonde. Huyu jamaa ktk kipindi cha jahazi ktk segment ya habari zilizojiri mjini ni mara nyingi saana huwa anaforce mitazamo yake ionekane ndio sahihi hata kama hana hoja za msingi.

Kwa mfano leo jioni ktk kipindi cha jahazi, jamaa ameponda sana taarifa zilizotolewa ktk magazeti kuwa viongozi wa CHADEMA wametishiwa kuuawa. Kwa maelezo yake ni kuwa hizi ni habari za uongo na anataka wasikilizaji wote waamini kuwa habari hizi ni za uongo. Akaendelea kueleza kuwa waandishi wa habari kabla ya kuchapisha habari kama hizi wanapaswa kupewa kwanza ushahidi. Je waandishi wa habari nao ni sehemu ya jeshi la polisi?

Maswali machache ambayo ningependa yeye binafsi ayajibu kama huwa anatembelea humu jamvini ni haya yafuatayo:
1. Unafahamu kuwa Dr. Harrison Mwakyembe aliwahi kutoa taarifa ktk vyombo vya habari na pia polisi kuwa kuna watu
wanasuka njama za kumuua? Wapuuzi kama wewe walipuuza na matokeo yake kila mtu anafahamu yaliyomkuta Dr.
Mwakyembe.
2. Unafahamu kuwa Amina Chifupa kabla ya kufariki aliwahi kuripoti kuwa anatumiwa sms za vitisho na watu ambao
walikuwa wanahofia kuwa angewataja kuwa wanajishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya? Wapuuzi kama
na wanafiki kama wewe walipuuza na matokeo yake kila mtu anafahamu kilichotokea.
3. Unafahamu yaliwahi kumkuta Imran Kombe? Naye pia alianza kwa kutumiwa ujumbe wa vitisho. Wanafiki, wapuuzi na
wazandiki kama wewe walikaa kimya lakini matokeo yake kila mtu anayakumbuka.
4. Unafahamu yaliyomkuta Horace Kolimba? Yaliyojiri si siri kwa umma wote wa watanzania.
5. Ufahamu matokeo ya vitisho alivyokuwa akitumiwa Said Kubenea wa mwanahalisi?

Tatizo kubwa mimi ninaloliona kwa waandishi wa habari wa aina hii ni matarajio yao kuwa huenda wakapewa fadhila ya Ukuu wa wilaya kama ambavyo baadhi yao juzi juzi walivyolipwa fadhila. Kama wewe Kibonde ni mpuuzi usijaribu kuwafanya watu wengine kuwa ni wapuuzi wenzako. Kwa hasira nilizonazo tu ni kwamba ninaisuburi kamati ya kuratibu maoni juu ya katiba mpya na hoja yangu ya kwanza ni kufutwa kwa vyeo vya mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa kwani naona ndio chanzo cha baadhi ya watangazaji kupotosha ukweli wa habari wanazozitoa. Ninawaomba sana radhi kwa kutoiweka ktk mtiririko mzuri thread hii kwani nilikuwa na hasira zisizo kifani.
 
Clouds wana page yao Facebook, Kibonde hana hadhi ya kujadiliwa hapa JF. Peleka huu ushuzi wako Facebook, hujalazimishwa kusikiliza clouds, kuna station kibao za redio za kusikiliza. tusichoshane hapa tuna mambo mengi ya msingi kujadili na siyo Kibonde ambaye jina lake linajieleza.
 
Achana nae anatema uozo bila kujijua bora angeungana na lile kundi la kitu tigo awe ananengua angeeleweka kuliko majungu anayoyapikb
 
Sii mmeshatuambia huyu jamaa ni mgonjwa? sasa kwa nini mnatusumbua na thread za kauli zake? Au huwa ana ID tofauti na anazianzisha mwenyewe?
Mkumbusheni akanywe dawa zake aongeze maisha,asitumie airtime kupotosha wale wenye uelewa mdogo kuhusu sakata hili la madaktari.
Madaktari wanataka vifaa na madawa yawepo hospitali ili wafanye kazi zao kwa uhakika (wao Clouds) wanapotosha kwanba madai ya madaktari ni posho. PUMBAVU ZAO.
Hivi Daktari hata akimuona mgonjwa na hakuna dawa wala X ray au T scan au Utra sound haifanyi kazi ataokoa maisha ya mgonjwa? Sasa wao wanasema wanahitaji serikali iboreshe hayo halafu WAPUMBAVU WACHACHE bado wao wameelekeza akili zao kuwa wao msingi mkubwa wa madai yao ni maslahi.
Tuache ujinga Watanzania kukubali kupotoswa na watu waliochoka kiakili,
BINAFSI NAWASHAURI MADAKTARI RUDINI KAZINI HIVYO HIVYO BILA DAWA WALA VIFAA HALAFU TUONE KAMA KWA KUANDIKA DAWA BILA DAWA NDIO VIFO VITAONDOKA. Wapo watanzania wameaminishwa kuwa nyie kuwepo tuu kazini ni Tiba kwao na wamekubali,ila watajua watu wanapigania nini kwa manufaa yao
 
Clouds wana page yao Facebook, Kibonde hana hadhi ya kujadiliwa hapa JF. Peleka huu ushuzi wako Facebook, hujalazimishwa kusikiliza clouds, kuna station kibao za redio za kusikiliza. tusichoshane hapa tuna mambo mengi ya msingi kujadili na siyo Kibonde ambaye jina lake linajieleza.

Sio kila mtu ana facebook account, na wewe hujalazimishwa kuchangia hii thread ungejipitia kimyakimya. Jf wengine ndo tunapata kila kitu so usitusemee na sisi. Nenda wewe kwenye wambea wenzio wa Facebook
 
Hiyo ni strategy ya kupata fadhila kwa watu wasio na uwezo...kumbuka dhaifu akishafanyiwa kazi zake kwa njia hiyo huteua watu hao dhaifu kuwa wakuu wa mikoa, wabunge na wakuu wa wilaya na ndiyo maana tuna serikali dhaifu! simple equation!
 
msihangaike na mpumbavu kibonde ashajifia huyo.ye anataka kila kitu atoe yeye majibu
 
SHAURI YAO wapnzani wakishindwa clous fm itakoma.

huyu anatafuta cheo toka ccm. hakuna lolote ni big deperado
 
Kibonde najaribu kujua anafanana nani sipati jibu yote nimemwachia mungu lamsingi nimefanya kama chombo chakunitoa stress basi lakini hana chakuonge ukakaa na kumsikiliza!!Kwakuwa na Media aliyopo ni kwamba haizingatii maadili ya utangazaji....wanachozingatia ni kama unajua kubwabwaja basi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom