Habari za vijana kujiajiri ni maneno matupu, vijana, Serikali na sekta binafsi tafuteni muarobaini wa ukosefu wa ajira

Landson Tz

JF-Expert Member
May 8, 2011
295
221
Duniani kote tatizo la ajira kwa vijana halijawahi kutatuliwa na vijana kujiajiri maana kujiajiri ni issue ngumu. Ukiangalia tatizo la ajira linahusisha makundi makuu mawili:

1. Waajiri (Serikali na sekta binafsi)
2. Waajiriwa (Vijana na makundi mengine)

Tuache kuchanganyana kila kundi lifanye kazi yake.

Serikali ikae pamoja na sekta binafsi wapange namna ya kutengeneza nafasi za ajira. Vilevile waajiriwa wajiandae kuajiriwa ikiwa ni pamoja na kujijengea uwezo wa kufanya kazi (elimu na ujuzi) na kuwa waaminifu maana nasikia uaminifu kwa vijana wetu ni kiwango cha chini sana.

Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka, tusikubali kuharibu nchi yetu kwa kuwaacha vijana bila kazi, bila kipato.

Nawaka wana wa jamii forum kutoa maoni na ushauri utaweza kusaidia kutatua tatizo la ajira nchini.

NB: Kujiajiri ni jambo jema ila lisitumike kutufanya tubweteke kutengeneza ajira maana haliwezi kutatua tatizo la ajira.

Naomba niwakumbushe watanzania, vijana ni nguvu kazi ya kujenga taifa la leo na kesho. Kuacha vijana wenye nia, uwezo na nguvu za kufanya kazi kulandalanda bila kazi ni ufisadi mwingine wa muda. Kama usemi usemao "time is money" tukishesabu masaa yanayopotea bila kuyatumia na thamani (Tshs) tutagundua kwa huu ni ufisadi namba moja kuliko ufisadi wowote ulio wahi kushuhudiwa nchi hii.

Landson Tz
 
Wajibu wa serekali sio kukusanya kodi peke yake serekali inapokwepa majukumu yake ndio kama hivyo njia pekee ni kuiondoa kwangu ya umma
 
Back
Top Bottom