Habari za magazeti na Joe Kihampa TBC 1

I thought I was the only one.....Kwa wale wanaoangalia Local TV kwa kupitia Dstv ndiyo mbaya zaidi kwani,TBC1 ndiyo pekee inayorusha matangazo ndani ya dstv.Mwenyewe nimeshuhudia mara kadhaa mtajwa akipotezea baadhi ya vichwa vya habari,hata hivyo mara nyingi kamera inamuumbua kwani headings zinakuwa zimeshanaswa na kamera!!.
 
Daaah nilijua mim tu naboreka kumbe tko wengi sana. Pale akae R. Mhando tu at least anajitahidi.
 
Hivi wanapewa maelekezo namna ya kusoma hayo magazeti? Wengi wanasoma vibaya lakini huyu jamaa kazidi...
 
kihampa badilika, kama huwezi kazi ya utangazaji rudi class kafundishe!!!
 
kihampa badilika, kama huwezi kazi ya utangazaji rudi class kafundishe!!!

Tupeni CV yake haka kabwana kwani inawezekana kameingia pale TBC1 kwa undugunization. Sioni kwa nini kama mtangazaji anajua Job Description yake kuwa nikusoma magazeti asubuhi, naye anaonekana hasomi na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake! Inawezekana kuna mtu anamlinda pale
 
State run press

What do you expect

If they own the information

They can bend it all they want
 
Chunguza taarifa za habari zote za tbc. Kwenye uchanganyaji picha siku zote lazima wakosee. Ujio wa picha ya tukio huwa unachelewa sana. Wakiona wamechemka huwa wanamrudisha sura ya mtangazaji ambae nae huwa hajui aendelee kusema nini mwisho hukaa kwenye screen kama kinyago. Kwa kuwa TBC1 huwa inaonekana dstv pia kwa kweli tunatia aibu kwa nchi za wenzetu ambao wao wako makini sana hasa kwenye habari.
 
joe tunajua upo humu humu, tatizo hatujui unatumia jina gani, ila masage sent!!!
 
Huenda amekusikia!

Kwa kukupa kionjo tu, Yule ni mwanaintelijensia, na yuko kikazi zaidi!
Huu utelijensia umeanza baada ya kumuondoa Mhando!maana siku hizi wnapoteza mvuto!kila kukicha habari za Magamba wapo huku kesho watakuwa kule kama bendi ya muziki wa dansi!pheew!
 
Kwa kweli muda wa sekunde kadhaa wanazotumia kusoma magazeti ni kidogo mno, kuna mwanamama kama sikosei anaitwa Rahel analazimisha kuhoji watu na huku anakenua meno tu, kwa kweli Marine Hasan ndio hodari na pia anawapa kila watu haki zao, Kwani Marine kamwagwa? mbona haonekani?
 
Mojawapo ya vitu ninavyofuatilia kila asubuhi ni muhitasari wa Magazeti ya siku husika. Kwa bahati mbaya TBC1 wanatusomea Magazeti yenye affliation na Chama Twawala (sio tawala). Kila uchao wanaanza na Uhuru, Jambo Leo, Zanzibar Leo na mara chache Mtanzania na Majira. Kwa nini hamfanyi mapitio ya Magazeti yenye kukosoa Serikali mfano; Tanzania Daima, MwanaHalisi, Raia Mwema??? Hata iweje hatudanganyiki, mnajisumbua bure kufanya upendeleo wa wazi! Hicho ni chombo cha Taifa kwa hiyo tangazeni habari zenye mizania. Mnatukera sana wananchi.
 
ulishawahi kumkosoa bosi wako ukaona matokeo yake? Siku tbc ikifanya ikisoma magazeti ya mwanahalisi na tanzania daima huyo atake yasoma siku hiyo ajue kibarua hana tena hiyo ndo bye bye
 
Back
Top Bottom