Habari za magazeti na Joe Kihampa TBC 1

vengu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
730
529
Joe kihampa ni mmoja wa watangazaji mahiri wa Jambo Tanzania TBC1 , tatizo alilonalo huyu bwana ni uoga wa kupitiliza wa kusoma vichwa vya habari katika magazeti ya kila siku, kuna baadhi ya magazeti amekuwa akiyaficha kwa makusudi kwa kisingizio kikubwa ni kubanwa na muda. USHAURI: Kama TBC 1 na huyo Joe kihampa wanaogopa kusoma baadhi ya magazeti kwa kisingizio cha muda ni bora waache kabisa biashara hiyo kuliko kutuboa wananchi...
 
Huenda amekusikia!

Kwa kukupa kionjo tu, Yule ni mwanaintelijensia, na yuko kikazi zaidi!
 
Nashukuru mwananchi mwenzangu km na wewe umeliona hili la huyu Joe Kihampa, anaboa aksoma magazet huyu!!! Km kuna habari inayohusu CCM ataisoma heading juu, atafunua uk.ilipo ataisoma yote, zngne anazpitsha juu juu, anakera huyu nkajua ni mimi peke yangu ndo ananikera, cjaelewa anaogpa nini wkt hata asiposoma magazeti 2takutana nayo tuu! Ana masifa sana huyu kaka.
Joe kihampa ni mmoja wa watangazaji mahiri wa Jambo Tanzania TBC1 , tatizo alilonalo huyu bwana ni uoga wa kupitiliza wa kusoma vichwa vya habari katika magazeti ya kila siku, kuna baadhi ya magazeti amekuwa akiyaficha kwa makusudi kwa kisingizio kikubwa ni kubanwa na muda. USHAURI: Kama TBC 1 na huyo Joe kihampa wanaogopa kusoma baadhi ya magazeti kwa kisingizio cha muda ni bora waache kabisa biashara hiyo kuliko kutuboa wananchi...
 
Ni kweli kabisa, wakati mwingine anadiriki hata kutunga baadhi ya maneno ili kupunguza ukali wa kile kilichoandikwa na gazeti.
Kwa kifupi sijapendezewa na uchambuzi wake wa sekunde 20 wa magazeti. Pia ni muoga sana wa kuyazungumzia magazeti ya Kiingereza, anapoteza muda mrefu kuzungumzia picha iliyoko front page..
 
Kweli wandugu, huyu jamaa ni muoga sana na huwa akiona kichwa cha habari kimekaa kiaina anasema maneno kichinichini: "imekaaje hii!"
 
Forgetting about intelligensia Joe ni moja ya watu waliolengwana ktk wimbo wa JD wa wanaume kama ............. Sorry ni vile nimeboreka naye mpaka.
 
Ni kweli kabisa, wakati mwingine anadiriki hata kutunga baadhi ya maneno ili kupunguza ukali wa kile kilichoandikwa na gazeti.
Kwa kifupi sijapendezewa na uchambuzi wake wa sekunde 20 wa magazeti. Pia ni muoga sana wa kuyazungumzia magazeti ya Kiingereza, anapoteza muda mrefu kuzungumzia picha iliyoko front page..

Hapo kwenye Red Mkuu nami nilitaka kuzungumzia hilo hilo!!! Mwisho nikawa nawaza labda kinamwona nini?! Yaani ataizungusha heading mpaka utachukia! Aaagh sijui kwa nini bwana kama huwezi lugha ya watu si uyaache hayo ya kimombo?

Lakini pamoja na roho yao mbaya magazeti tunakutana nayo mitaani, kwanza wanatupozea muda tu!!! Huyu dogo hebu ajirekebishe bwana!
 
ni kweli kabisa JOE KIHAMBA cjui; ana matatizo ktk kuendesha kipindi chake cha Jambo hasa sehemu ya kusoma magazeti. habari yoyote inayohusu serikali/ccm kama imevurunda na kuandikwa live utakuta anamung'unya maneno. kuna magazeti kama mwanahalisi, tanzania daima, raia mwema hata kama yamepelekwa mezani utakuta anayaruka,akiyasoma basi unamwona anacyochagua heading. kipindi kile kimepoteza maana kabisa. na ye mwenyewe mi namwona mjinga/mtumwa flani. ananiuuuzi sana jamaa yule hata kukutana nae sipendi
 
LABDA uelewa wake na taaluma yake kwani ni mwalimu na kasomea ka-diploma ka uandishi wa habari,nadhani bora arudi kule TBC FM alikokuwa mwanzo au akafundishe kwa waalimu wana hali ya woga na wanapenda kunyenyekea hata pale palipo na makosa.
 
Ni afadhali kuacha kuangalia hayo magazeti kuliko kumsikiliza Joe!!!!
 
Huyu anajipendekeza tu, kwani nini wanaposoma wengine na hasa somebody Mbapu husoma bila kuangalia kinamgusa nani. joe ni mwalimu wa ajabu na kinapofika kipindi cha magazeti huwa ninachukia kwanini yupo studio, sasa raha uwakute na Zacharia, wote wazee wa kujipendekeza:disapointed:
 
Ni mwalimu na Mzee wa Kanisa mtukuka, tofauti yake na na Elisha Elia ndiyo inayomfanya aendelee kubaki studio..kama news reporter na si mwandishi kivile kama Malin Hassan
 
Atambue kuwa TBC1 is just a stepping stone na ajue anaua ujuzi wake na kujifunga zaidi na TBC1 kana kwamba hatakwenda kufanya kazi sehemu nyingine. Kwa tathmini hii ya watanzamajia aelewe kwamba anapoteza umaarufu na kiwango chake kinashushwa kwa kasi ya ajabu kwani watazamaji ndo wanajua wanataka kuona nini na ndio wadau wakubwa wa habari. Kama nabisha basi fikiria watazamaji wakigoma kuangalia news au kususa kusoma magazeti nini kitatokea?
 
Huyu Joe mnataka asome kila kitu ili mzidi kupata habari za kutupaka magamba mapya. Mimi namfagilia sana kwa namna anavyofanya na watangazaji wengine igeni kama mnataka kutunza kazi zenu
 
Back
Top Bottom