Habari za kutisha gazeti la mtanzania kuhusu chadema

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wadau nimekufa ganzi asubuhi hii baada ya kuona gazeti la mtanzania la leo,limeandika habari za matusi makubwa dhidi ya Chadema.Limeandika kwamba Chadema wamevurugana kwa sababu ya udini waliouanzisha,pili wamesema vurugu za Arusha wamewahadaa wananchi kwa sababu ya udini wao na tatu wanasema mauaji ya Arusha yamesababishwa na Chadema.Ni habari mbaya kwa mtu yeyote akisoma.Habari hii kwa jinsi ilivyoandikwa nikihusisha na kipindi maalum kilichorushwa na ITV juzi inaonekana kuna mkakati maalum umesukwa wa kuichafua na kuiangamiza Chadema.Yeyote anayeweza kulipata hilo gazeti alisome aone hayo matusi.....kwa uandishi huu sijui kama tutafika.
 
Kuwa mvumilivu, ndio siasa. unataka kila mtu afikiri sawa na wewe?
hata mimi nadhani kuna ukweli kiasi ktk hayo, chadema wasingelazimisha kuandamana kungetokea mauaji?
 
Wengine hatuna "access" na hilo gazeti - had it been better ungetoa "summary" ya nini kilichochapishwa kabla ya jazba?
 
Ni habari mbaya kwa sababu zinaitaja Chadema au ni mbaya kwa sababu hazina ukweli? Ulichoonyesha hapa ni woga na masononeko yako bila kupiga analysis juu ya kwa nini unadhani habari hiyo ni mbaya. Ninaanza kushuku uwezo wako wa kupigana!
 
Kuwa mvumilivu, ndio siasa. unataka kila mtu afikiri sawa na wewe?
hata mimi nadhani kuna ukweli kiasi ktk hayo, chadema wasingelazimisha kuandamana kungetokea mauaji?

Walipoandamana katika mazishi ya wale marehemu kulitokea mauaji?????????!!!!!!!!
 
Kipindi nilikiona kilitayarishwa na Idara ya Habari Maelezo. Mimi ndiyo mara yangu ya kwanza kuona Maelezo wameandaa kipindi wakati never on earth wamewahi kudeploy camera zaidi ya still!.

hivyo sishangazwi na hoyo habari ya Mtanzania pale newsroom yao wanavichwa moto chini ambao kwenye tasnia ya habari niwapiganaji wenye vyeo vya makamanda, kama makamanda wamtumikia fisadi mkuu unategemea nini?!.

Viongozi wa Chadema kama wana akili ya ukweli, wasireact wala wasijibishane kabisa na Mtanzania. Wao waendelee na agenda zao wanaowaelewa. wanawaelewa?
 
Mbona hamna hoja mpya hapo? ni marudio tu kwa kuwahoja zote 3 zilishatolewa na kujadiliwa sana hapa JF. Labda kama kuna ambayo umesahau kuiweka
 
Ni gazeti la Mtanzania. Taratibu limegeuka gazeti la udaku. Walioshiriki maandamano ya Arusha wanaujua ukweli hawahitaji kuonyeshwa picha. Walio na uelewa na ambao hawakushiriki wanaujua ukweli hawatabadilishwa kwa propaganda! Suala la Arusha kwa CDM ni msiba na hakuna haja ya kulumbana na magazeti. La msingi ni kuendelea kuwatetea watanzania! CCM wanajizika wenyewe!
 
Habari gani ya kutisha hapo mbona ni mambo ya kawaida tumewazoea ulitarajia nini zaidi, kwangu mimi wewe ndiyo unanitisha kutokuwa na ufahamu huo hadi leo.
 
Kuwa mvumilivu, ndio siasa. unataka kila mtu afikiri sawa na wewe?
hata mimi nadhani kuna ukweli kiasi ktk hayo, chadema wasingelazimisha kuandamana kungetokea mauaji?

Swali la kujiuliza wale walio uwawa waliuwawa kwenye maandamano au baada ya mkutano pale viwanja vya NMC? ikiwa waliuwawa baada ya mkutano then Chadema hawana pa kujitoa ila tuwaulize wamesababisha vifo kwa faida ya nani? ikiwa waliuwawa wakati wa maandamano the Polisi na serikali ndio wa kulaumiwa na wanashatahili kutueleza zaidi amri ya kuua ilitoka kwa nani?
 
Kuwa mvumilivu, ndio siasa. unataka kila mtu afikiri sawa na wewe?
hata mimi nadhani kuna ukweli kiasi ktk hayo, chadema wasingelazimisha kuandamana kungetokea mauaji?
Yangetokea tu unadhani hatujui kuwa nyinyi ndo MAJAMBAZI!
 
Kwa kweli sio siri nilipaki gari pembeni kusikiliza vizuri na nilitoka pale na hasira kubwa sana. Yaani kama ningemjua mwandishi aisee tungefikishana mbali. Hawa ni waandishi ambao wanapotosha ukweli katika jamii nawaombeni jina la mwandishi wa habari hizi wana forum kweli i am serious
 
Wakuu nawaombeni jina la mwandishi wa Mtanzania aliyeandika habari kuwa Chadema udini or something mauaji ya Arusha na picha yake tafadhari nataka kumjua tu.

nawakilisha
 
Wadau nimekufa ganzi asubuhi hii baada ya kuona gazeti la mtanzania la leo,limeandika habari za matusi makubwa dhidi ya Chadema.Limeandika kwamba Chadema wamevurugana kwa sababu ya udini waliouanzisha,pili wamesema vurugu za Arusha wamewahadaa wananchi kwa sababu ya udini wao na tatu wanasema mauaji ya Arusha yamesababishwa na Chadema.Ni habari mbaya kwa mtu yeyote akisoma.Habari hii kwa jinsi ilivyoandikwa nikihusisha na kipindi maalum kilichorushwa na ITV juzi inaonekana kuna mkakati maalum umesukwa wa kuichafua na kuiangamiza Chadema.Yeyote anayeweza kulipata hilo gazeti alisome aone hayo matusi.....kwa uandishi huu sijui kama tutafika.

Hakuna "Fake Report" au Utumiaji wa Vyombo vya Habari Hasa Mengi Production Kutawadanganya Wananchi Tanzania. Poleni CCM...Kama Amani Inachafuliwa kwa Hii Njia "Tutaona Nani Atashinda" Wananchi au Mafisadi. Mengi Sio Fisadi? Chadema Wakiingia Madarakani, Mengi Atakwenda Jela Nae...Hizi Resources Zote za Mengi Amepata Wapi Huu Utajiri? Wananchi Tangu Siku Nyingi Tunajua There is No Way Mengi is That Honest...
 
wametumwa na hawataweza kutimiza malengo waliyotumwa kutimiza kwani ni makubwa na wameshachelewa sana
 
Back
Top Bottom