Habari za Kusagana, Ngono, na Serikali ya CCM!

Fundi Mchundo, wa kwanza katika walio sawa.

Nakubaliana kabisa na hitimisho lako, lakini sio njia uliyotumia kufikia hitimisho hilo.

Nadhani ni kweli kwamba Mwana wa Adamu angeulizwa leo ni nini mawazo yake kuhusu usagaji na ushoga angesema sio makosa. Kama aliacha msingi mmoja tu wa imani aliyofundisha, "Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako," basi sidhani, sioni, unawezaje kumrudhu mwenzio kwa kuwa na urafiki wa kumsaga au kumjamia kishoga. Kama kuna madhara ya kibaolojia nitasahihiswa hapo.

Lakini sio kwa sababu eti wakati umebadilika basi na Mwana wa Adamu atabadilika. Baba yake aliahidi kwamba hatabadili misingi ya sheria zao, wala hatabadili ahadi kwamba hatabadilika, kwa maana akibadilika atakuwa amesogeza magoli pembeni, na mataifa yatasema amefanyika mwongo. Hatapatikana uongo kamwe.
Yakobo 1:17 Kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeuka-geuka.

Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana nyinyi hamkuangamizwa.

Zaburi 102:27 Lakini wewe U Yule yule, Na miaka yako haita koma.

Waraka Kwa Waebrania 6:17 - 18 Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana wairithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu.
 
Last edited:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom