Habari za Kusagana, Ngono, na Serikali ya CCM!

Hivi kwa nini sisi waafrika tunapenda sana theories za maadili wakati kiukweli hayo maadili hatuyajui na wala hatuna? Ukipita hutakosa kusikia "huo sio utamaduni wa mtanzania" au "huyo siyo mtanzania kwa sababu kafanya hivi au vile" Sasa unajiuliza utamaduni wa mwafrika au MTZ ni upi? kuiba? uzembe? upendo? .....wakati watu wanaiba ilhali mamilioni ya wenzao wanateketea kwa magonjwa na umasikini?.

Mfano mdogo: Neno ngono kuna watu mpaka leo wanapinga lisiongelewe hadharani..na hata ukienda kwenye luninga ukaliongelea..wanaharakati watakwambia unaharibu maadili ya watoto...harafu angalie maambukizo ya HIV kwetu sisi..especially vijana wa miaka 20-30... yako juu kuliko huko Ulaya na kwingineko ambako Ngono ni neno la kawaida..wenzetu ngono inaonyeshwa mpaka kwenye luninga.. watu wataangalia, watafanya watakalo....kwa assumptions zetu..hawa watu ingebidi wafe kwa UKIMWI zaidi kuliko sisi! Je kwa nini sisi ndo tunaathirika zaidi? does it mean sisi tunapenda ngono kuliko viumbe wowote duniani?

Maoni yangu: Transparency, transparency imetushinda. Hata kama ni ngono..waache watu waiongelee, waisome, waifanye..watajua madhara yake wenyewe. Kama ni mzazi kaa na mwanao..mpe elimu ya mahusiano kadri uwezavyo. Utakuwa umemsaidia zaidi ya ufikiriavyo. Tusitake kujifanya kwamba kuna mtu aliye superior mwenye moral standards ambazo wote inabidi tufuate. Nani huyo show me that person. Tuache kujificha kwenye vivuli vya maadili wakati tunateketea. Wasaganaji wapo wengi tuu. Unless niambiwe kwamba sisi huo usagaji ni tabia za wazungu..kwetu hakuna! Hivi tukiwakubali kama parti ya jamii..ilmradi wanafuata sheria za nchi..lipi tatizo? Tusitake kuchanganya IMANI zetu na MAISHA ya wengine. Tatizo hatutofautishi imani na sheria!

Mfano mimi kama Mkatoliki-mseminari, I can never allow a guy bishop or priest to administer a sermon to me. True, true, true. Lakini kama mtanzania na raia wa kawaida..sina shida na Pinda kuwa guy au yeyote yule..as long as anatekeleza wajibu wake kama sheria ya nchi inavyomtaka. I can not impose my moral values on others. Kitu ambacho ndo waafrika wengi tunapenda.

Hiyo picha sioni tatizo lake..infact mwanakijiji kama mwanao kauuliza..ingebidi ukae naye chini. Umpe darasa makini sana. Umpe madhara unayoyaona kama mzazi na kwa sababu ni mwanao..umwambie kipi anastahili kufanya. Lakini ukijificha chini ya kivuli cha maadili..atakuja kujifunza baadaye wewe haupo..na madhara yake unaweza usiyapende.

Kinachonisikitisha ni kwamba..waafrika bado tunaamini kwamba.."wakubwa" zetu ndo wa kutuonyesha njia..ndo wana moral standards ambazo tunastahili kufuata..lakini. surely, mtu kama Lowasa au Chenge..na madhambi yao yote..can I ever trust what they tell me, however genuine it might be?

Tujitahidi kuwa wawazi na yale tunayoyaogopa. Hata serikali inayoendeshwa kwa uwazi nadhani mtaona tofauti yake na ile serikali inayofanya kila kitu kwa usiri mkubwa kama za kwetu Africa.
 
maureen.jpg

Imetoka kwenye Gazeti la Ijumaa April 17-23, 2009.

Je, kuna vitu ambavyo magazeti hayawezi kuviandika bila kuwa graphic kama ilivyo kwenye makala hii?

Je, Serikali inatambua madhara ya habari kama hii kusomwa na mtoto mdogo wa shule ambaye anaweza kulipata gazeti hili mitaani?

Je, Wizara ya Habari na Utamaduni chini ya mtani wangu Mkuchika wanafanya nini kuzuia kile ambacho wagiriki wa kale walikiita corrupting the morals of the minors? na ambacho hata sisi tunacho kwenye sheria zetu?

Ni mpaka Waziri gani aandikwe kuwa anasagana ndipo watajua habari kama hizo ni detrimental to the welfare of our youth?

Kuna mtu anayejali? Wachungaji na Mashehe wako wapi kupinga uchafu huu au ndio wanasubiri hadi mwanasiasa awaalike?

Taasisi za haki za watoto ziko wapi au hadi waahidiwe fedha?

Mwanakijiji!

Mwanakijiji:

Maendeleo unayopigia kelele yanakuja na hayo mambo. Watu wanapoanza kuendelea, sex sio kitendo cha kuendeleza uzazi tena.

Huyo mlimbwende angekuwa angekuwa anaishi kijiji kwetu Bomba Mbili, ambapo angehitajika kutafuta kuni, kuchota maji, kulima na kuzeeka kabla ya kufikisha miaka 30, hayo yote yasingetokea.
 
Magazeti kama haya yangekuwa yanafungiliwa mbali yanatia kichefuchefu. Wao wakiguswa kwenye ishu zao haraka wanakimbilia kufungia magazeti, yale yanayoharibu maadili ya jamii kama haya wanayaachia, karibu Tanzania itakuwa na maduka ya vitu vya ngon "sex shops" aaagh
 
Je jamii ina haki ya kuwalinda watoto? au kwa vile mambo yanayozungumzwa ni starehe ya watu wazima basi jamii isijiwekee mipaka ya kulinda watoto wake? That is the bottom line. Mimi sizungumzii reaction ya watu wazima na madevu yao, kwa wale wanaojua I am also a good writer of erotic stories, so I know what I'm talking about..

Kwa vile ni mambo ambayo yapo, yameendelea kuwapo na si mageni ina maana watoto wadogo waachiliwe tu; inawezekana hapa ndio wapo wazazi ambao wanaangalia porno na watoto wao kwa kisingizio cha "siyo mambo mageni!"

What should be done then, we accepted globalisation, if not on news papers there big screens out there displaying the same. In this respect the kid has several ways to get these funny news and acts.
 
Swali langu hakuna mtu anayetaka kujibu; Je jamii inayo sababu ya kuwalinda watoto kutookana na exposure ambayo detrimental to the welfare? Ninaamini jukumu la malezi linabakia kimsingi la wazazi wenyewe; pamoja na hayo sitaki serikali au chombo cha habari kinilazimishe jinsi ya kumlea mtoto wangu.

Ndiyo maana hoja yangu haiko kwenye kilichoandikwa kwani I really don't care much about that.. hoja yangu iko kwenye access ya watoto to such materials. Mengine ambayo watu wanayasema siyajali sana kwani mtu mzima unawajibika kwa mambo yako mwenyewe.

Maana kama tunakubaliana kuwa jamii isiweke taratibu au kufuatilia taratibu ilizojiwekea juu ya malezi ya watoto n.k basi tuendelee kwa sababu we are the one paying for it.

Kama tunakubaliana pia kuwa mambo haya tayari yapo na yameendelea kuwapo na kwamba hatuwezi kuyabadilisha kwa sababu ndiyo reality (which is absurd argument) kwanini basi tusiamue kuyahalalisha tu? Kuna haja gani ya kuwa na sheria inayokataza sex with minors kama hao hao minors wanaangalia mambo yale yale ya watu wazima unfiltered?
 
Mkuu, mbona unakuwa disingenuous. Ni kitu gani katika taarifa ile ambacho unaona mtoto hastahili kujua? Kwamba Tanzania kuna lesbians na gays? Naona tatizo lako ni neno kusagana. Sasa kwa vile mwandishi alikuwa anazungumzia lesbians, ulitaka atumie neno gani ambalo halitamdhuru mwanao? Kama nilivyosema awali, neno lesbian ( msagaji ) si tusi. Ni mtu mwanamke ambae anavutiwa na wanawake wenziwe. Kwa kutaka kulifanya kuwa tusi ndiyo unaingia katika kundi la homo phoebes waliojaa nchini kwetu. Unataka kudekeza hypocrisy ambayo inatufanya tuone kuwa kujadili matumizi ya kondomu kuwa kosa, heri wanetu waendelee kuambukizana haya magonjwa ya siku hizi. Draconian laws tulizo nazo kuhusu homosexuality hazina nafasi katika jamii yeyote inayoheshimu haki ya wananchi wake. Wanachofanya watu wazima kwa matakwa yao bila kudhuru wengine serikali haitakiwi kuingilia. Ni muhimu tuanze kuheshimu uhuru wa raia mtu mzima kuchagua nani anaetaka kuwa na uhusiano nae. Hata kama ni wa jinsia yake. Ili mradi huyo mwenzie nae ni mtu mzima na amefanya hivyo kwa ridhaa yake.

Argument yako tena kuhusu kuhalalisha paedophilia ati kwa sababu watoto hao hao wanaona vitendo hivyo vile vile haina mantik. Nchini mwetu hamna gazeti linaloonyesha pornography hata of the soft type! Au unataka kutueleza kuwa hizo picha za watu wakipigana busu kwa mtazamo wako ni porn? Haya magezeti ni ya udaku, yakitumia lugha ambayo ni titillating lakini si obscene. Ukitaka obscenity nenda kwenye ngoma za mchiriku,mdundiko n.k. Nenda kwenye klabu za pombeuone paedophiles wanavyotesa wazi wazi.
Au hayo hayakutatizi kwa sababu yamefunikwa na kitambaa cha utamaduni wetu?

Si kila kitu kila kinachofanyika katika jumuia lazima kihalalishwe. Hakuna jamii isiyotumia madawa ya kulevya lakini hii haimaanishi kuwa yahalalishwe? Hivi unaamini kuwa wote wanaobaka watoto wanafanya hivyo kutokana na haya magazeti? Au watoto wanajiingiza kwenye vitendo hivyo kutokana na sinema za wazungu na magazeti hayo? Mbona wakati wetu vyote hivyo havikuweko na vijana nahata baadhi ya watoto walijiingiza kwenye vitendo hivyo!

Tusipende majibu mepesi kwa matatizo yetu ya msingi.

Amandla..............
 
Ni kweli kuna umuhimu wa serikali kufanya kitu flani kuhusu hili.Lakini tatizo zaidi haliko kwenye uzembe huo wa serikali bali JAMII.Hivi hizo graphics za Global si nafuu ukilinganisha na uchafu unaoongezeka kila kukicha huko mitaani!?Hiyo kwenda na wakati sasa imegeuka kama kuruhusu baadhi ya akinadada kutembea nusu uchi.Hiyo mipasuo imegeuka mipasuko.Na hao akina Maimartha wanaouza kemikali za kukuza makalio imekuwa balaa juu ya balaa.

Of course,serikali inatakiwa kufanya kitu flani lakini pasipo JAMII yenyewe kutambua kuwa mwelekeo huu haufai itakuwa ni zaidi ya kazi pevu.Na ni kweli kwamba kuzoeleka kwa jambo chafu sio excuse ya kuliacha liendelee lakini kuitegemea serikali hii inayoshindwa kudhibiti fedha zake huko BoT imudu ulinzi wa maadili yetu...TUTAUMIA.
 
Wacha mi niende Iran nikajifunze Sharia. Nikirudi naenda gombea ubunge kwetu. Wakinipa ubunge mie tayari waziri wa habari au wa Sheria. Dawa ya waandishi wanaoharibu jamii kwa kutumia mikono yao ni kukamata mkono wake anaoandikia na kuweka chini ya katapila usagwe na tairi

Kuandika au kuto andika hakuwezi kuzuia usagaji na uchoko.
Umefika wakati wa kuweka mipaka ya uandishi na pengine kuwa na maduka au sehemu ziuzazo magazeti yenye habari za Wahanga.
Usagaji na Ubasha ni tatizo la dunia nzima, sioni ni vipi sisi watanzania au nchi fulani zenye misimamo mikali zikijifanya kutaka kujitenga na dunia.
Ukiacha mafisadi watanzania si Wazebaki ni Wadunia, yaliyomo duniani yatawaathiri tu.

Huko Iran kuna wasagaji kibao, kisichokuwepo Iran ni magazeti yenye habari za usagaji.
Hulko Iran kuna machoko kibao ksicho kuwepo ni magazeti yenye habari za machoko

Nchi zote za kiarabu zimeoza kwa vitendo vya kusagana na kujamiiana kinyume cha maumbile. Kwa sababu ya sheria za kikatili wengi hufanya mambo haya na ndugu wa karibu.

Nchi za Ulaya na Marekani mambo hayo yanafanywa mchana kweupe tena kwa Leseni za serikali. N irahisi sana kudhani Usagaji na usenge upo Ulaya na Marekani zaidi kuliko nchi nyingine.
Avumae Baharini ni Papa lakini usisahau Nyangumi, taa na pweza nao wamo.

Nenda Zanzibar Mombasa Lamu na hata mitaa fulani hapo Dar, huhitaji kuchunga mkeo asiopolewe na njemba kwa vile njemba nyingi hazina mpango. Lakini ni vigumu sana kuzuia mkeo asitongozwe au kuishia kubarazwa na mijimama misagaji inayokuja kwa gia ya "shoga unasuka vizuri kweli" huku nia yao ikiwa ni kumasa mkeo kwa kila hila.

Ni vema tutambue kwamba kukaa kimya hakuta maliza au hakutatoa elimu ya kupambana na masula haya yenye kubeba aibu na kutatanisha katika jamii.
 
Kuandika au kuto andika hakuwezi kuzuia usagaji na uchoko.

Huko Iran kuna wasagaji kibao, kisichokuwepo Iran ni magazeti yenye habari za usagaji.
Hulko Iran kuna machoko kibao ksicho kuwepo ni magazeti yenye habari za machoko

Ni vema tutambue kwamba kukaa kimya hakuta maliza au hakutatoa elimu ya kupambana na masula haya yenye kubeba aibu na kutatanisha katika jamii.

Mkuu nashukuru kwa kunielewa maana umerudia nilichoandika mimi kwa kutumia maneno tofauti. Kila mtu 'MZIMA' ana uhuru wa kuamua kufanya atakalo, cha msingi asivunje sheria za nchi au kanunu za maisha za mahali husika. Kama mtu anafanya uchoko huko chumbani kwake bila kumkwaza mtu mwingine mtaani huo ni utashi wake na aendelee. Hata akifanya kutwa mara tatu, ni starehe yake.

Nisichotaka mimi (pengine ndicho anachozungumzia MMK) ni kutumia wino wako au TV yako kumshawishi mtu mwingine (hasa mtoto ambaye anapaswa kuelekezwa) ajifunze kufanya kitu ambacho kwa macho ya wengi ni upotofu. Maana yangu ni kuwa kama isingekuwa huyo mwandishi ku 'expose' huo utumbo, basi huyo mtoto wangu ambaye nilimfundisha kuwa "hiki kitu ni kibaya usithubutu kufanya", asingetamani kujaribu kufanya huo utumbo .Lakini kitendo cha kuanika huo utumbo hadharani mtoto anazoea na matokeo yake anaona ni kitu cha kawaida na siku moja na yeye anatafuta jiti au chochote anachoona kinafanana (pengine na mdogo wake) wanajifungia chumbani wana test alichokisoma au kukiona.

Kuna haja ya waandishi wa habari na vyombo vyao kutuachia wenyewe tuwafundishe watoto wetu tutakavyo na si watakavyo wao. Bila kuwa na sheria kali zenye kudhibiti, haya mambo yataendelea kila kukicha. Si lazima iwe sheria ya kuponda mkono kama nilivyosema, cha msingi iwe shiria ambayo mkosaji atajutia kosa lake mara itakapomkumba.
 
Last edited:
Naona tatizo lako ni neno kusagana. Sasa kwa vile mwandishi alikuwa anazungumzia lesbians, ulitaka atumie neno gani ambalo halitamdhuru mwanao? Kama nilivyosema awali, neno lesbian ( msagaji ) si tusi. Ni mtu mwanamke ambae anavutiwa na wanawake wenziwe. Kwa kutaka kulifanya kuwa tusi ndiyo unaingia katika kundi la homo phoebes waliojaa nchini kwetu.

Wrong on the first count, na kuwa homophobe ni label tu unayojaribu kunipachika. Ni sawa na mtu kusema wewe ni homophile!

Unataka kudekeza hypocrisy ambayo inatufanya tuone kuwa kujadili matumizi ya kondomu kuwa kosa, heri wanetu waendelee kuambukizana haya magonjwa ya siku hizi. Draconian laws tulizo nazo kuhusu homosexuality hazina nafasi katika jamii yeyote inayoheshimu haki ya wananchi wake. Wanachofanya watu wazima kwa matakwa yao bila kudhuru wengine serikali haitakiwi kuingilia. Ni muhimu tuanze kuheshimu uhuru wa raia mtu mzima kuchagua nani anaetaka kuwa na uhusiano nae. Hata kama ni wa jinsia yake. Ili mradi huyo mwenzie nae ni mtu mzima na amefanya hivyo kwa ridhaa yake.

wrong on the second count; nimeshasema sina tatizo la watu wazima wanafanya nini chumbani kwao! Inaonekana unataka kutetea kitendo cha usagaji au homosexuality kitu ambacho hakiko kwenye hoja zangu. Tetea tu unavyoweza, to me hoja yangu iko kwa watoto. Once you get over your defence of homosexuality (kitu ambacho ukiniuliza mimi I can give a very strong defence ya haki za mashoga!).

Argument yako tena kuhusu kuhalalisha paedophilia ati kwa sababu watoto hao hao wanaona vitendo hivyo vile vile haina mantik.

Once again.. it seems you don't know what paedophilia is all about. So wrong on the third account. Angalia maana ya paedophilia utaona it is not the subject ya hoja yangu.

Si kila kitu kila kinachofanyika katika jumuia lazima kihalalishwe. Hakuna jamii isiyotumia madawa ya kulevya lakini hii haimaanishi kuwa yahalalishwe? Hivi unaamini kuwa wote wanaobaka watoto wanafanya hivyo kutokana na haya magazeti? Au watoto wanajiingiza kwenye vitendo hivyo kutokana na sinema za wazungu na magazeti hayo? Mbona wakati wetu vyote hivyo havikuweko na vijana nahata baadhi ya watoto walijiingiza kwenye vitendo hivyo!

Tusipende majibu mepesi kwa matatizo yetu ya msingi.

Amandla..............

Inaonekana wewe hutaki hata watu waulize maswali ya msingi kwa sababu inaonekana kuyauliza tunaonesha homophobia! Once you get over the question of sexuality utaona kuwa hoja yangu is beyond mere people's orientations.
 
maureen.jpg

Imetoka kwenye Gazeti la Ijumaa April 17-23, 2009.

Je, kuna vitu ambavyo magazeti hayawezi kuviandika bila kuwa graphic kama ilivyo kwenye makala hii?

Je, Serikali inatambua madhara ya habari kama hii kusomwa na mtoto mdogo wa shule ambaye anaweza kulipata gazeti hili mitaani?

Je, Wizara ya Habari na Utamaduni chini ya mtani wangu Mkuchika wanafanya nini kuzuia kile ambacho wagiriki wa kale walikiita corrupting the morals of the minors? na ambacho hata sisi tunacho kwenye sheria zetu?

Ni mpaka Waziri gani aandikwe kuwa anasagana ndipo watajua habari kama hizo ni detrimental to the welfare of our youth?

Kuna mtu anayejali? Wachungaji na Mashehe wako wapi kupinga uchafu huu au ndio wanasubiri hadi mwanasiasa awaalike?

Taasisi za haki za watoto ziko wapi au hadi waahidiwe fedha?

Mwanakijiji!

Mkuchika yeye anaona makala zinazo isema CCM tu lakini mengine huwa haoni ni upumbavu wa viongozi wa CCM ambao wao wanaona siasa tu na si vingine
 
Tanzania imekamatwa katikati...huku wananchiw ake wanataka kuiga uzungu, lakini hakuna sera zilizo tayari kwa ajili ya kuhakikisha kuwa maigizo hayo hayatakiuka maadili (hata maadili ya uzungu wenyewe). Unachopuliza Mwanakijiji, nadhani kinakwenda mbele ya hapo au ni matokeo ya hizo sera kama zingekuwepo. Naamini kuwa ni kupitia katika sera za aina hiyo ndipo tunapoweza kuweka huo ulinzi juu ya watoto na taarifa kama hizo.
 
Hii ni kutoa kwa uhakika kuwa mfumo mzima umeoza.
Nchi inaongozwa na chama kilichooza c henye maadili yaliyooza basi na watoto wake wanapewa malezi yaliyooza.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Mkjj naona unaumiza kichwa bure.
Kila kizuri cha jiuza kwa uzuri wake.
Watu wakijua kwamba gazeti ulilolitoa linaandika mambo mabaya kwa watoto basi watachukua tahadhari kwamba endapo wakilinunua watakua makini kwa watoto wao wasilikaribie. Au pengine ndio litakosa umaarufu kwani linazungumzia mambo ambayo sio mazuri kwa watoto kwahio wateja wataacha kununua.

Naniachoona hapa kama mkuu mwingine aliyepost nikuhusu huyo mwanao kuuliza baba nini maana ya USAGAJI
Yuko mwengine alisema wako watoto wengine watauliza baba watoto wanatoka wapi.

Unaongelea usagaji mbona kuna mambo mengine mengi tu ambayo watoto hawatakiwi kuyaona lakini wanaona kwenye national Television zetu.
Kibaka akipigwa live tena waandishi kama nyie ndio mnaonyesha kwenye tv mtu akibundwa mpaka kukaribia kufa.
Na hapo je utazima TV yako?
Watuhumiwa Tz hawatajwi kwa majina mkato bali mpaka ukoo.
Ulaya mtu akiwa mtuhumiwa anatajwa jina lake lakwanza tu mpaka ajulikane ana hatia nakufungwa ndio penginepo litajwe.

Kama sio hilo neno la USAGAJI tu mwanao atakuja kukuuliza baba nini maana yakufumaniwa ugoni.
 
Uzuri mmoja wa hili jukwaa letu ni kuwa ukiteleza, unaelimishwa. Ndiyo maana namshukuru Mzee Mwanakijiji kwa kunisahihisha spelling ya neno Homophobe na kunifundisha neno jipya kwangu Homophile. Shukrani sana. Ila kwa bahati mbaya, pamoja na msaada huo bado arguments zako kwangu hazi-hold water. Zifuatazo ni sababu zangu.

a) Mimi nimesema kuwa inaelekea kwako wewe tatizo ni matumizi ya neno kusagana. Neno hili (kwa jinsi ulivyoandika) limeifanya habari hii kuwa haifai kuweko kwenye family paper. Wewe ( kama nimekuelewa vizuri) umekana hii tafsiri yangu. Lakini ni wewe mwenyewe ambae katika posting zako ndiye uliyesema kuwa kutokana na neno hili kutajwa, mtoto wako amekuulizia maana yake! Maana nyingine ni kuwa lisingetumika neno hili, mtoto wako asingekuuliza swali kuhusu kitu ambacho unadhani si wakati wake kujua! Swali langu linabaki pale pale na ni " kwa vile mwandishi alitaka kututaarifu kuhusu binti anayejihusisha na vitendo vya lesbians ulitaka atumie neno gani ambalo lisingekukwaza lakini lingeleta ujumbe?" Je mwandishi angesema moja kwa moja kuwa Maureen ni msagaji ndiyo ingekubalika zaidi? Lakini mtoto mdadisi si angeweza kuuliza "msagaji anafanya nini?". kama vile swali kama hilo linavyoweza kuja kuhusu " kunyimwa unyumba, ubakaji, au kama alivyouliza Darwin, kufumaniwa ugoni!" Yote haya si kuhusu ngono? Au unataka kutuambia kuwa kutumika kwa maneno haya na kwenyewe kumechangia kuporomoka moral values za watoto wetu? Kama kweli hoja yako ni beyond sexual orientation kama unavyodai basi ungelalamikia na magazeti yote yanayoandika habari hizi!

mtoto wangu wa kike baada ya kusoma gazeti hili ambapo kichwa hicho cha habari kipo ukurasa wa mbele kauliza "Baba kusagana ndiyo nini"?..

Unanishutumu kuwa hoja yangu ya msingi ni kutetea kitendo cha usagaji au homosexuality halafu unatamba kuwa ukiulizwa unaweza kutoa utetezi mzuri kuhusu haki ya mashoga. Utetezi gani huo wakati umeshawasema kuwa hawa wanashiriki katika kitendo ambacho hata wagiriki wa kale walikikemea na kukiona corruptive? Si hilo tu, unaendelea kusisitiza kuwa kitendo hiki ni criminal act kwenye sheria zetu! Sasa utawateteaje watu ambao unaona wanaweza kucorrupt watoto wako na vile vile ni criminals ( inaelekea unakubaliana na hiyo sheria)? Ninavyoelewa mimi mtu mwenye mawazo kama haya ndiye anayeitwa homophobe. Au ndiyo case ya kutaka kuwa na keki na kuila pia?

Je, Wizara ya Habari na Utamaduni chini ya mtani wangu Mkuchika wanafanya nini kuzuia kile ambacho wagiriki wa kale walikiita corrupting the morals of the minors? na ambacho hata sisi tunacho kwenye sheria zetu?

wrong on the second count; nimeshasema sina tatizo la watu wazima wanafanya nini chumbani kwao! Inaonekana unataka kutetea kitendo cha usagaji au homosexuality kitu ambacho hakiko kwenye hoja zangu. Tetea tu unavyoweza, to me hoja yangu iko kwa watoto. Once you get over your defence of homosexuality (kitu ambacho ukiniuliza mimi I can give a very strong defence ya haki za mashoga!).

c) Unasema kwa vile tunasema kuwa kitendo hiki ni sehemu ya jamii yetu basi kwa nini tusihalalishe? Argument ambayo ingawa nakubaliana nayo lakini sioni kuwa ni ya msingi kwa vile naona unai-base on the shallow grounds kuwa chochote kinachoandikwa ni halali. Which is absurd! Kwa msingi huo basi mtu anaweza ku-argue kuwa tusiandike kuhusu uvutaji bangi ( ambao ni sehemu ya jamii yetu na ni criminal act). Kitu ambacho tusingependa watoto wetu wajifunze.

d) Unazungumzia kuhusu sex with minors halafu unaniambia sijui maana ya neno paedophilia? Nimekuwekea chini tafsiri niliyoitafuta kutokana na ushauri wako na yenyewe inazungumzia criminal activity involving sexual offences against children by adults. Au children sio minors? Uliyeleta suala la paedophilia ni wewe, Mkuu na si mimi. Kwa kufanya hivyo umeifanya kuwa sehemu ya hoja yako.

Kama tunakubaliana pia kuwa mambo haya tayari yapo na yameendelea kuwapo na kwamba hatuwezi kuyabadilisha kwa sababu ndiyo reality (which is absurd argument) kwanini basi tusiamue kuyahalalisha tu? Kuna haja gani ya kuwa na sheria inayokataza sex with minors kama hao hao minors wanaangalia mambo yale yale ya watu wazima unfiltered?

Once again.. it seems you don't know what paedophilia is all about. So wrong on the third account. Angalia maana ya paedophilia utaona it is not the subject ya hoja yangu.

Maana ya paedophilia ni hii hapa. Asante kwa ushauri wako.

Paedophilia is criminal activity involving sexual offences against children by adults, including the production and distribution of child pornography. It is also known as criminal paedophilia

Mimi sikatai kuwa kuna vitu ambavyo watoto hawastahili kuangalia. Tatizo langu ni kuwa umebebea bango habari ambayo ingawa ni ya kipuuzi na infatile lakini ni long stretch kudai kuwa ni porn. Umeshindwa kuweka bayana hiyo graphic language iko wapi kwenye hiyo taarifa. Au ni hapo anapozungumzia kifaa kinachofana........miguno ya mahaba? Unfortunate choice of words lakini sio graphic!

Hypocritical morals kama hizo ndizo zinazotufanya tuone kuangalia mtu anambusu mpenzi wake, mtoto wake, mke wake n.k. kwenye luninga au gazeti kuwa ni porn lakini hatuoni tatizo kuangalia maonyesho ya ngoma zetu ambako watu wanaigiza vitendo hivyo wazi wazi!

Kudai kuwa magazeti ya Shingongo ndiyo yalio at the forefront wa kuanguka maadili yetu ni kumpa sifa asiyostahili. Ni sisi, wewe na mimi, ndiyo tunaotakiwa kuwafundisha watoto wetu athari ya kufanya vitendo hivi kabla ya kupevuka. Kuyalaumu magazeti kwa ku-introduce masuala ya ngono kwa minors wakati huo huo tunaruhusu watoto wa miaka 12 kuolewa ni kuwa disingenuous! Hakuna gazeti lililosajiliwa bongo linalo-peddle porn, hata ile inayoitwa soft ambayo iko kila mahali kwa wenzetu.

Kwa vile ni mambo ambayo yapo, yameendelea kuwapo na si mageni ina maana watoto wadogo waachiliwe tu; inawezekana hapa ndio wapo wazazi ambao wanaangalia porno na watoto wao kwa kisingizio cha "siyo mambo mageni!
"

Mwisho ni kuwa kisingizio kuwa hatujakuelewa kinaanza ku-wear thin. Si lazima kila wakati uwe sahihi. Kwenye hili, Mkuu, ( kwa mtazamo wangu) umechagua the wrong case. Unageuza kichuguu kuwa mlima bila sababu yeyote.

Amandla...........
 
Last edited:
FM: NI katika mazingira gani jamii (serikali ikiwemo) inapaswa kuweza mipaka na kuregulate habari za kingono zinazoweza kufikiwa kwa urahisi na watoto?
 
Back
Top Bottom