Habari za Kiintelijensia Kuhusiana na Gazeti ya Mwanahalisi

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Habari nilizozipata kupitia mtandao wa nchi kavu kuhusiana na Gazeti la Mwanahalisi ambalo huwa linatoka kila wiki siku ya jumatano ni kua wiki hii halijatoka huku mikoani hakuna hata matumaini ya kulipata wiki hii kama wanavyosema wauza magazeti.

Na habari nilizopata ni kua tokea mzee wa Monduli kuongea na wanahabari kua atafanya kitu mbaya kupitia kwa wanasheria wake kama magazeti kuandika habari za kumuhusu yeye binafsi, sasa umbea uliopo ni kua gazeti hili la Mwanahalisi lilikua limesheheni habari za kutikisa nchi kuhusina na bwana huyu.

Imebidi bwana Saidi Kubenea na jopo lake walifanyie Editing gazeti lao kuhusiana na habari zilizokua zinamuhusu mkulu huyu na ndio maana mpaka sasa haliko hewani.

Jamani naomba kuwakilisha na mtupe dondoo kama hili gazeti kuna mtu kalipata leo hii.
 
sasa mwanahalisi wasipoandika chochote kuhusu mzee wa monduli si watafilisika? Anyway personally nimechoka kusoma kuhusu lowassa kwenye mwanahalisi almost ktk lila toleo. Kuna mengi mapya yanatokea nchini mwetu and we shouldn't dwell every day talking about people.

Aaarrghh i'm thred wajameni
 
Kama ni kweli hayo ndiyo matokeo ya kuandika maisha ya watu binafsi. Kama gazeti lina data za kweli zenye maslahi kwa taifa hakuna sababu ya kufuta hizo data. Je lilikuwa na ajenda ya kumchafua tu mtu na sasa amesema sichafuliki, gazeti ndiyo linanywea ?? Ndicho mnataka tuamini ? Kubenea tupe ukweli wa mambo >
 
Kwahiyo tumaanishe kua hata tokea yule aliyekua mbunge wa Tabora baada ya kujivua magamba yote na kubakiza gamba moja la uanachama ndio kupelekea gazeti hili kukosa mvuto kwakua kila wiki halikua linakosa habari zake???
 
dah! Huyu jamaa muoga sana wa kupigwa madongo,anajiona yeye hakosei na kila anachokitaka yeye ndicho sahihi,je akiwa rais c ndo kutakuwa na gazeti la Uhuru tu? Nalog off
 
Jamanii hii taarifa nadhani ina mushkeli, gazeti nimenunua tangu asubuhi na habari kuu ni ya Kabila kuomba Msaada kwa JK, na mengine mmmmh, hio habario sio ya kweli kabisa ila wamemwandika Mzee Six
 
kuna uwezekano kweli hilo gazeti limekuwa edited manake tangu nianze kusoma mwana halisi kila week takribani miaka miwili sasa hivi sikumbuki siku ambayo gazeti hilo lilikosa picha au habari ya lowasa front page, lakini la week hii haliko na picha yake
 
mimi gazeti la mwanahalisi nmelinunua mapema sana.ni toleo Na.265
habari iliyolibeba ni;
kabila amuangukia rais kikwete na sitta kanyea kambi.mia
 
...yaelekea mwandishi wa Post hii anaota tu kuwa MwanaHALISI halipo mtaani. Mimi niko Dsm nimelipata,na nimempigia simu kakayangu aliyeko Tukuyu-Mbeya,naye anasema keshalipata asubuhiasubuhi. Huyu mtoa maada,anaongelea mkoa gani?
 
Back
Top Bottom