Habari za airport na wageni wanaokuja tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari za airport na wageni wanaokuja tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JS, Aug 23, 2011.

 1. JS

  JS JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wadau niko hapa airport yetu tukufu JKNIA nauza sura kwa kwenda mbele nikisubiria wageni wangu kuwapokea. Uzuri niko huku ndani kabisa. Sasa hapa kwa bench nililokaa wamejaa watu kama 8 wahindi wametokea Bangladesh hawafahamu lugha yoyote kwa hiyo hata kujaza zile fomu za immigration na visa ni kazi kweli mpaka wanaomba msaada.

  Sasa nimewadodosa kidogo wanakuja kufanya kazi au kutembea au vipi.....wakanijibu jibu ambalo sielewi wakanionyesha barua kuwa kuna kampuni inaitwa maweni construction ltd au kitu kama hicho. Wanaombewa wapatiwe business visa na wanakuja kujenga cement plant. Na ni cheap labour maana wenyewe wachafu wachafu wananuka jasho basi tabu tupu. Na eti watakuwa nchini kwa miezi miwili.

  Sasa jamani kweli kweli yani hizi kampuni mpaka watu wanaingizwa kutoka huko asia kuja kujenga kwani sie hatuna wajenzi au cheap labour? Na immigration wanawapa visa. tuna vijana wangapi wanalalamika kila siku hakuna kazi kumbe kazi zipo ila wanapewa wageni? Na jinsi wanavyoonekana wakishavuka hilo geti hapo airport ndo basi tena hakuna cha kurudi kwako wala nini baada ya hiyo miezi miwili.

  inabidi immigration wawe serious kwa hili maana wanagawa visa tu kama maji. Wawafikirie wazawa wetu ambao nao wanahitaji hivyo vibarua. Bado niko hapa nacheki movements itakavyoendelea.
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Halafu sioni hata mmoja akilipia visa......hmmmm
   
Loading...