Habari ya Zamani lakini imenivutia kiukweli hebu na nyinyi muione jamani.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
RAIS KIKWETE ANAFANYA VIZURI ANAPOFANYA HIVI




  • Picha hizi za Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete zinahuzunisha, zinafariji na pia zinatia matumaini. Zinahuzunisha kwa sababu zilipigwa wakati Rais alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Evaristi Semeni - mtoto mwenye umri wa miaka kumi na moja aliyefariki katika ajali ya kugongwa na gari tarehe 26/4/2010 jioni katika kijiji cha Msoga ambapo yeye pamoja na watoto wengine wawili walifariki dunia.

KIKWETE4.jpg

  • Unaweza kuiona huzuni katika uso wa raisi pamoja na baba mzazi wa Marehemu Evaristi Semeni. Tulikuwa tumezoea kuwaona viongozi wa ngazi za juu wakihudhuria mazishi ya familia zenye majina. Picha hii inagusa hisia sana na inamwonyesha raisi katika ubidanamu na utu wake kabisa. Naamini kwamba mzazi huyu, pamoja na huzuni yake yote ya kuondokewa na mtoto wake, alifarijika kwa pole na faraja iliyoletwa na ujio wa kiongozi mkuu wa nchi.


  • Hapa Rais yupo na waombolezaji ndani ya nyumba. Na ukitazama vizuri utaona. Haya ndiyo maisha halisi ya Watanzania wa vijijini ambao kwa bahati mbaya ndiyo wengi. Sijui Rais anawaza nini...




  • Hapa Rais anatoka nje kwenda kuungana na waombolezaji wengine. Nimefikiri mambo mengi sana baada ya kuzitazama picha hizi. Pengine safari kama hizi za viongozi wa kitaifa kwenda kuyaona maisha halisi ya Mtanzania wa kawaida kule kijijini zinaweza kuwa kichocheo kinachoweza kuiamsha upya ari mpya na kuhakikisha kwamba kweli maisha bora kwa kila Mtanzania yanapatikana tena kwa kasi mpya na nguvu mpya!


  • Mungu Awalaze marehemu mahali pema peponi; na tunamuunga mkono rais kwa kwenda kuungana na wananchi hawa wa kijijini katika huzuni yao; na kama alivyosemaMjengwa, kuwapelekea mwanga katika giza lao na matumaini katika hali yao ya kukata tamaa.

 
Ndo maana tunataka mtu ambaye kwa kugundua ufukara uliopo miongoni mwetu hasa vijijini,ataweza kupigania kuongoza nchi kuondokana na balaa hilo.
 
Hvi anajickiaje kuwaona watanzania wenzake anaowaongoza wanaishi kwnye nyumb kama hyo?inackitisha na bdo ajifunzi k2 hapo?
 
Huyu tuna hasara naye sana!

Na cjui kaja kubadilikia wapi kwn alianza kwa maneno mazuri lakini nimeshindwaga kuElewa alitelezea wapi!

Tuna pigo naye kubwa Kitaifa sana!
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
Jamaa kabla ya kuwa waziri na hata rais kwa wanaomjua nasema tena kwa wanaomjua Jakaya ana moyo wa kibinadamu moyo wa kiutu...Ila ndio kila binadamu ana mapungufu yake yepi mimi siyajui
wasalaam
 
Back
Top Bottom