Zanaco
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 1,621
- 1,581
KumbeKwanza tuwapongeze Gazeti la Jamhuri kwa kuibua hii kitu. Combination ya Balile na Manyerere sio mchezo. Namfahamu jamaa mmoja aliombwa matangazo ya serikali, nadhani aligoma, sasa atajuta!.
Pamoja na hoja hizi za ufisadi kuwa kweli, pia kuna uwezekano waandishi wa uchunguzi wa gazeti la Jamuhuri kutumiwa kwenye smear campaign ya vita vya kibiashara.
Jamuhuri nitawaona ni watu wa maana sana kama watatufanyia value for money audit kuwa tulichonunua ni inferior quality huku tumelipa pesa nyingi!. Sometimes cheap is expensive!.
Nakumbuka issue ya gharama iliibuka BOT kuhusu uchapishaji wa noti zetu kuwa zinachapwa ghali na Gavana Balali aliridhia. Prof. Ndulu akaamua kubana matumizi kwa cheap printing, kilichotokea ni inferior products!.
Watanzania wengi, kutokana na levels za umasikini wetu, affordability yetu kununua magari ni Japanese kwa sababu ni cheap na sio durable!.
American, UK, Germany cars are expensive but more durable. Tungefanya research ya vifo vinavyotokana na hizi cheap Japanese cars kutokana na durability, tungeshangaa!. Ndio maana mpaka leo mpaka kesho, viongozi wetu wakuu hawatumii Japanese saloon cars!.
Sasa akiibuka mtu kufichua bei za magari ya viongozi kutoka DT Dobbie ukilinganisha ya Japan toka KJ Motors, utaitwa ni ufisadi wa kutisha!, kumbe ni vitu viwili tofauti in terms of quality, security, performance and durability!.
Tusihamanike sana na huu ufisadi, usikute kumbe tumeuziwa kitu bora kwa bei sahihi!.
P