Habari ya uchaguzi mdogo wa madiwani imeishia wapi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Nakumbuka siku chache zilizopita gazeti la Mwananchi liliandika habari kuhusu kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 21 nchi nzima kujaza nafasi za madiwani 22 pamoja na uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Dimani kwa upande wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mwananchi,kampeni hizo zilikuwa zimepangwa kuanza tarehe 22 mwezi huu mpaka tarehe 21 mwezi January mwakani.

Swali langu ni je,uchaguzi huu mdogo umeahirishwa au ni ratiba imebadilika?

Waandishi tusaidieni kupata majibu.

Habari husika isome kupitia link ifuatayo:

Kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kuanza December 22
 
Mkuu unawauliza chadema au tume?
Wakati chadema wapo bize kufanyanyiana figisu na kuweka wagombea pekee,ccm wameshamaliza kazi.Kwa udiwani kampeni zinafanyika ndani ya kata tu pengine ndio maana huyaoni mafuriko na wapiga deki lakini uchaguzi upo pale pale
 
Wakishiriki uchaguzi wakati tayari mgombea Mmoja wa 2020 ameishajiwekea refa wake nitajua Mbowe ni janga la kidunia. Pia ataumiza wagombea ubunge ambao wataibiwa na kura na wanasisiem wakurugenzi wa Halmashauri
 
Njaa mbaya sana,wasuse wakose ruzuku?
 
Uchaguzi upo huku kwetu Chadema wanapiga kampeni za udiwani na magari yanapiga nyimbo za kumsifia Lowasa utafikiri siyo wao waliokuwa wanasema Lowasa ni fisadi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom