Habari ya magari 600 ya Dangote kuwasili mmezitoa wapi?

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
habari wadau!
hakuna mwaka ambao unaongoza kwa uzushi kwenye mitandao na vyombo vya habari kama huu mwaka wa 2016, baada ya dangote na Raisi Magufuli kukutana, Dangote alisema anampango wa kuleta magari 600 na mengine baadhi ya hayo yameshafika,aliongea kwa uwazi kabisa lakini ghafla kwenye mitando hasa humu jamii forum wakaja na thread eti magari 600 ya dangote yameshafika na mpaka wakaleta na picha za mameli na magari kuthibitisha kuwa magari mia sita yameshafika, inamaana wanajua zaidi kuliko mwenye nayo....na habari yenyewe imekuzwa utafikiri ni ukweli...wakati mwenyewe anasema first batch ndo imefika na baada ya Christmas magari yote yatakuwa yamewasili....sasa mtu ghafla eti magari mia sita ya dangote yawasili......jamani!!

hivi kwanini huu mwaka umekuwa wa kizushi hivi, si selikali si watu binafsi yaani ni uzushi uzushi tu, mwaka huu tumelishana matango pori kibao, ingekuwa uzushi ni sumu na ukikufikia na ukauamini unakufa wengi wangekufa.
 
Nadhani wewe huna uzoefu na mambo ya uandishi habari, hebu rudia kusikiliza alichosema Dangote
 
mtoa post ni huna akili we shida yako ipi hapo 600 au first batch??ilimradi magari yameshafika mengine yapo njiani haituhusu lakin taarifa tumeipokea kwa mikono miwili ujuo wa magari hayo.
 
Nadhani wewe huna uzoefu na mambo ya uandishi habari, hebu rudia kusikiliza alichosema Dangote
kaka rudia kasililize mwenyewe dangote anasema nini....ni kweli kasema analeta magari mia sita lakini kilicholipotiwa na wengi wanaseama kuwa yameshafika kitu ambacho si kweli
 
mtoa post ni huna akili we shida yako ipi hapo 600 au first batch??ilimradi magari yameshafika mengine yapo njiani haituhusu lakin taarifa tumeipokea kwa mikono miwili ujuo wa magari hayo.
ni kweli sina akili kama unavyosema, shida yangu ni upotohaji wa habari, kwanini wasilipoti ukweli kuwa sehemu ya magari mia sita yameanza kuwasili?
 
Nchi za wenzetu wenye kujua maana ya uwekezaji, Mkataba ungembana Dangote kuingiza magari yake, na hiyo kazi ya kusambaza cement wangepewa wazawa wenye magari yao ila hapa kwetu kampuni ina miliki vituo vya mafuta 120 nchi nzima na ina malori ya mafuta 500 hivi hawa wa hali za kawaida wanaolipa kodi zote wafanye kazi gani?
 
ni kweli sina akili kama unavyosema, shida yangu ni upotohaji wa habari, kwanini wasilipoti ukweli kuwa sehemu ya magari mia sita yameanza kuwasili?
inawezekana alioandika hiyo post kaandika tu alivyoona na si kufanya uchunguzi,pia kwa kuwa aliona maongezi ya dangote na rais yalikuwa hivyo ndo maana akaandika magari 600 pia magari mia sita sizan kama rais kupakiwa kwa meli moja.
 
hata maongezi ya dangote na rais yanaonyesha wazi kabisa kuwa ile ni first batch, dangote mwenyewe anasema kuwa ile ni first batch na nyingine itakamilika kabla ya krisimas, kwanini ilipotiwe kuwa tiyari magari 600 yameshawasili, kiuhalisia huu ni upotoshwaji....sina tatizo lolote na habari hiyo lengo langu ni kueleza ni namna gani mwaka hu tumekubwa na habari za kizushi kwa watu kudandia mambo bila kuyaelewa na kuyaleta hadharani kwa upotoshaji
 
Nchi za wenzetu wenye kujua maana ya uwekezaji, Mkataba ungembana Dangote kuingiza magari yake, na hiyo kazi ya kusambaza cement wangepewa wazawa wenye magari yao ila hapa kwetu kampuni ina miliki vituo vya mafuta 120 nchi nzima na ina malori ya mafuta 500 hivi hawa wa hali za kawaida wanaolipa kodi zote wafanye kazi gani?
Kwanza hawa ndio wanaohujumu usafiri wa reli, wacha wasome namba.

Halafu kwani kabla ya dangote walitegemea kuishije??? Waendelee na shughuli zao.huyu bwana kaja kutafuta hela, kaja kihela hela tu.
 
Back
Top Bottom