Tetesi: Habari ya kuanzishwa Tanzania Commercial Bank ina ukweli? Na iwapo ni ya kweli, nini zitakuwa faida na hasara zake kwa benki za biashara nchini?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,258
2,000
Katika pita pita yangu mitandaoni muda mfupi uliopita, nimekutana na hii habari isiyo rasmi kutoka kwa mtumiaji mmoja wa mtandao wa twitter kuwa kuna mpango wa kuanzisha Bank ya aina hiyo hapa nchini.

Swali: Iwapo habari hii ni ya kweli, nini zitakuwa faida na hasara zake kwa sekta ya mabenki hapa nchini iwapo benki hii kweli itaanzishwa na kuwa ni benki ya serikal?

Je, wananchi watafaidika kupitia benki hii huku mabenki binafsi yakiathirika?

Au mabenki binafsi yatajiongeza kiushandani na hivyo kumfanya mwananchi ndio afaidike?

Au benki binafsi zitayumba na kuondoa ushindani hivyo kutotoa nafuu yoyote kwa mwananchi?

Na kama ni kweli benkii hiii itaanzishwa,serikali itamudu kuiendesha kwa faida?

Kama kweli mpango huu upo,je unapendekeza benki iendeshwe vipi?

Benki hii iendeshwe na kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 au iendeshwe kwa ubia na mabenki binafsi?

Tutoe maoni yetu yanayoweza kusaidia namna bora ya uanzishwaji wa benki hiyo kama kweli mpango huo upo,

Vile vile kama yupo anaeweza kututhibitisha habari hii, basi afanye hivyo.
 

EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
737
1,000
Unaposema "kuanzishwa kwa benki ya aina hiyo" unamaanisha nini. Tanzania tayari kuna commercial banks nyingi tu. Zisizo commercial banks ni chache sana. Hilo Tanzania Commercial Bank ndilo jina la hiyo benki au ni aina ya hiyo benki mpya? Nafikiri utafute taarifa zaidi uwe "more informed" juu ya hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
10,217
2,000
Ana maana bank yenye jina la Tanzania Commercial Bank TCB ambaye inasemekana ita replace TPB na TIB.
Unaposema "kuanzishwa kwa benki ya aina hiyo" unamaanisha nini. Tanzania tayari kuna commercial banks nyingi tu. Zisizo commercial banks ni chache sana. Hilo Tanzania Commercial Bank ndilo jina la hiyo benki au ni aina ya hiyo benki mpya? Nafikiri utafute taarifa zaidi uwe "more informed" juu ya hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
14,621
2,000
Nnachofaham, NMB, NBC, CRDB, TPB, TIB zina chembe chembe za userikali. Tujiulize kuna unafuu wowote huko kwa watumiaji?

Endapo itaanzishwa wajipange kuwa na huduma bora wakitumia zaidi teknolojia, hakuna haja ya kuwa na matawi mengi, mambo yote mtandaoni na kiganjani kwa simu. Riba rafiki kwenye mikopo na vigezo vinavyoendana na mazingira yetu wananchi tulio wengi.

Ni hayo tu kwa sasa.
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,354
2,000
Unaposema "kuanzishwa kwa benki ya aina hiyo" unamaanisha nini. Tanzania tayari kuna commercial banks nyingi tu. Zisizo commercial banks ni chache sana. Hilo Tanzania Commercial Bank ndilo jina la hiyo benki au ni aina ya hiyo benki mpya? Nafikiri utafute taarifa zaidi uwe "more informed" juu ya hili.
hapo unataka utafutiwe nini tena wakati mambo yote yapo wazi, kila kona habari hizo zipo
na wote ni malalamiko zile Benki TPB (Twiga &Postal) sasa kuunganisha na TIB ambayo ndio imevurugwa na kufilisika kutokana na kiuongozi

sasa watapewa majukumu yote ya Serikali km ilivyo NMB na CRDB malipo, mishahara nk
ingia ndani ukajipatie yaliyomo kuliko kumtuma mwenzio kwenye moto akutolee kiazi ule
 

bg2017

Member
Jul 31, 2017
79
150
Hizi taarifa za muda labda mchakato ndio umekamilika sasa, sana nina imani wao walisha jiridhisha kua kuna manufaa kiuchumi ni suala endelevu bank nyingi tu wataziunganisha. Mwanzoni wakati magua anaingia ndio ilikua moja ya agenda zake, nchi hiwe na bank chache zenye nguvu kuliko kuwa na msululu wa mabank kibao amabyo hayana tija, na sio jambo la ajabu kuna nchi kibao zina benki chache imara, cha msingi ni kuongeza wateja kwa kuwafikia wananchi wengi zaidi na huduma bora
Screenshot_20200522-134853_Samsung%20Internet.jpg
Screenshot_20200522-134831_Samsung%20Internet.jpg
Screenshot_20200522-134033_Samsung%20Internet.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom