Habari ya ITV iliyowang'oa DED na DC Mvomero: Vyombo vya habari kutakiwa kuomba ruhusa kabla ya kurekodi na kutangaza habari

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Mvomero Morogoro: Wanafunzi wapatao 733 Wanakalia Viroba juani kutokan ana madarasa kuchakaa
IMG_20200706_074903.jpg
 
Nilijua tu hii habari haiwezi kuwaacha salama ITV na huu ndio ujinga unaoendelea awamu hiii.

Mimi ndio maana siku hizi sina muda wa kufuatilia media za hapa nyumbani kwani ni wazi zinadhibitiwa na haziko huru.Wanachotakiwa ni kutangaza habari za kufuruhisha tu watu/mtu fulani!!

Mambo ya hovyo sana haya!!
 
Dah!..hao wananchi wa huko wahamasishwe kujenga vyumba vya madarasa hata kama elimu ni bure lakini huu ni uzembe.
 
Eti uchumi wa kati, tushaonekana mataahira watz. Mungu atuponye akili zifunguke tujue kuhoji sio kila kitu wasemacho ni ndioooo....!
 
Nilijua tu hii habari haiwezi kuwaacha salama ITV na huu ndio ujinga unaoendelea awamu hiii.

Mimi ndio maana siku hizi sina muda wa kufuatilia media za hapa nyumbani kwani ni wazi zinadhibitiwa na haziko huru.Wanachotakiwa ni kutangaza habari za kufuruhisha tu watu/mtu fulani!!

Mambo ya hovyo sana haya!!
Mie nilihamia Aljazeera kitaaaaambo media za tz tupa kuleeeeee
 
Sasa wazee wa uchumi wa kati mbona mambo yanakataana? Au ndio ya wahabeshi wa Ethiopia na matreni ya angani huku wananchi wakitoroka kwa kubebwa ndani ya containers za mizigo!
 
DED na DC wameng'olewa sababu habari imerushwa hewani (wamezembea hadi ITV wakarusha hii habari) au wametenguliwa kwa sababu ya uzembe na wanafunzi wanakaa chini katika wilaya yao?
 
ITV wametimiza wajibu wao,wao kama chombo cha habari.Haikuhitaji kuomba ruhusa,aliyekosea awajibishwe,tatizo litatuliwe.Mficha uchafu maradhi humuumbua,hizo ndo habari za kuisaidia jamii.Nawapongeza Itv/Radio one kwa hilo.
Kweli hao watakao support huu uzi kuwa vyombo viwe vinaomba ruhusa kwanza ndio wanaotaka kuminya uhuru wa vyombo vya habari
 
Nilijua tu hii habari haiwezi kuwaacha salama ITV na huu ndio ujinga unaoendelea awamu hiii.

Mimi ndio maana siku hizi sina muda wa kufuatilia media za hapa nyumbani kwani ni wazi zinadhibitiwa na haziko huru.Wanachotakiwa ni kutangaza habari za kufuruhisha tu watu/mtu fulani!!

Mambo ya hovyo sana haya!!

Kama sheria hairhusu kutoa habari kama hizi basi Mh. Rais au Waziri Mkuu wawe na sehemu ya wazi ya kupokelea habari kama hizi ili wazifanyie kazi wao moja kwa moja, ila kuzificha hakutaisaidia serikali na raia wake
 
Kwa hali hii naona kazi ya uandishi inakosa mashiko na uimara kiutendaji, huwezi kupata habari nzuri kwa kuomba muhusika ajiandaye au akaandaye eneo la habari, jamani waandishi wa bongoland akili ya ziada iongeze na yako.
 
Back
Top Bottom