Pascal Mayalla,
Huyu Dr. Shika ana dalili zote za ugonjwa na mgonjwa hatakiwi kudhihakiwa bali anahitaji huruma ya kutafutiwa matibabu stahiki.
Tanzania ya awamu hii ya CCM imekosa utu na ndiyo tunaona vyombo vya habari kushabikia ugonjwa au maumivu ya majeraha ya mgonjwa.
Hili la Daily News badala ya kumtafutia msaada wa kitabibu uwe kumpeleka kwa wataalamu wa afya ya ubongo, counselling / ushauri nasaha n.k wao wanashangilia mgonjwa kuwa homeless n.k
Hili saga la Dr. Louis Shika mpaka sasa mbali ya kuhojiwa na vyombo kibao vya habari sijapata kuona wakitafuta positive side ya vitu alivyopata kufanikiwa kufanya zaidi ya mahojiano ya kumdhalilisha mtu anayehitaji msaada.
Naamini kuna wakati mwingine Dk. Shika hali yake inakuwa murua kiafya ya ubongo na hapo vyombo hivi vya habari wangetuletea habari chanya za mapito yake kielimu n.k badala ya kuvizia akiwa hana utimamu wa afya ndiyo wanafanya mahojiano naye.
Hii inaonesha kuna mapungufu katika weledi wa wanahabari na sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania kuhusu magonjwa na vipi au wakati gani wamhoji mgeni wao ili wapate upande chanya wa mapito ya watu kama kina Dr. Shika.
Bora haya mahojiano yana chembe ya utu kujua matatizo ya Dr. Shika kiafya:
Balozi Patrich Chokala juu ya Dr. Louis Shika