Habari wakuu, tunaambiwa Kuna umoja wa Africa unaoziunganisha nchi zote kuwa kitu kimoja

Luther760

JF-Expert Member
Feb 17, 2019
316
240
Habari wakuu, tunaambiwa Kuna umoja wa Africa unaoziunganisha nchi zote kuwa kitu kimoja. Hii kitu imekaaje kwa wenzetu kukamatwa kila siku wakielekea SA kwa madiba?
Je hii organization inasimamia nini.?Halafu kama watu wanapita kwenye nchi yenu hamuezi kuwasindikiza mpaka mpakani mkawaacha waende zao?
Naomba kujuzwa wajuvi wa haya mambo.
 
We mwenyewe ukiondoka unaenda Africa kusini pasipo uhalali watakaoanza na wewe ni wazambia au Msumbiji, bila kujali kuwa unateseka.

Wafuate sheria ndo watapita bila kuteseka wala kukamatwa.

Kwani unafikiri wanakamatwa Tanzania tu, hata huko Kenya wengine wanakamatwa na wakipita hapa kwetu salama Zambia wanakamatwa.
 
Tatizo South nako kwa hapa Africa ni kama Marekani kwa wenzetu waamerika, nako kule watu wa mataifa jirani wanahangaika kweli kukimbilia huko, wankufa lakini hawakomi, kama leo hii kuna jamaa kafa na katoto kake wakati akivuka mto wa mpaka wa Mexco na Marekani, mke wake alivoona maji yanazidi akaamua kurudi na kumwacha mumewe akiendelea kuvuka huku akiwa amembeba mtoto.

Inasikitisha kweli lakini Trump amekomaa wengine kuendelea kuwarudisha makwao.
 
Ukitaka uone umoja unafanya kazi uwe na documents muhimu alafu nenda kama hautafurahia, AU.
 
Tatizo South nako kwa hapa Africa ni kama Marekani kwa wenzetu waamerika, nako kule watu wa mataifa jirani wanahangaika kweli kukimbilia huko, wankufa lakini hawakomi, kama leo hii kuna jamaa kafa na katoto kake wakati akivuka mto wa mpaka wa Mexco na Marekani, mke wake alivoona maji yanazidi akaamua kurudi na kumwacha mumewe akiendelea kuvuka huku akiwa amembeba mtoto.

Inasikitisha kweli lakini Trump amekomaa wengine kuendelea kuwarudisha makwao.
Hapo nimeelewa
 
Back
Top Bottom