Habari wadau nimeathirika na tramadol yani niko tramadol dependant

tiku

JF-Expert Member
Oct 31, 2015
441
242
Habari viongozi mimi ni mwanamke wa miaka 40 hivi kuna kipindi niliugua sana kiuno nikawa napewa tramadol nikawa nasikia nafuu kubwa sana.

Sasa nimekuwa deoendant siwezi kumeza tramado saivi nameza hadi vidonge vinne kwa pamoja ndo zinafanya kazi. Bila hivo siwezi kufanya chochote bila kumeza tramadol japo kiuno nilipona tangu mwaka juzi lkn nimeendelea kutumia hadi leo
 
Naomba msaada mwenye kujua jinsi ya kujitoa nisiendelee kutumia tramadol
 
Naomba msaada nisaidiwe jinsi ya kujitoa kutumia tramadol. Yani nisimeze tena na niwe mzima
 
Pole sana, mke wangu pia Amekuwa na hilo tatizo yeye bila Hedex hawezi kufanya chochote
 
Kwanini unatumia kama kiuno kilipona tangu mwaka juzi?unatumia kama starehe/unaenjoy ama?sijaelewa

Angekuwa mwanaume ningeelewa kuwa anatumia ili achelewe kufika nyumbani. Maana tramadol nayo ina maajabu yake.
 
Pole sana mkuu.Hiyo hali iliwahi mkuta baba angu mzazi kwa miaka 4 alikua lazima achome sindano kila siku na kama hajaichoma basi anakua teja...Tramadol yenyewe ni miongoni mwa dawa za maumivu zina effect kubwa kwenye ubongo huleta utegemezi mzee wangu alikua akichoma kwa kua alikua na maumivu ya risasi.

Siku moja tulikaa kama familia tukaona tutampoteza hapo tukaamuru aiche lakini taratibu basi tulifanya yafuatayo.

1. Tulianza kumcheleweshea muda wa kuchoma hapa inahitaji roho ngumu maana kuna muda unaona kabisa huyu mzee anakata moto muda wowote, pia ilikua anachoma bila kueleweka yeye alikua anachoma saa 3 ila tukawa tunamuacha labda mpaka saa 7 au 8 kutegemea na hali yake au mara anachoma leo kesho achomi tukiona kazidiwa sana ndo tunamchoma tulienda hivyo hivyo kwa muda wa miezi mitatu ,akawa anapata tatizo la ganzi vidonge vya Neurotone ikawa mbadala mpaka sasa mwaka wa 5 amepona kabisa.

2. Mazoezi mepesi na mlo kamili matunda kwa wingi.

3. Tulimpa ushauri yeye mwenyewe aanze kuikataa yaani aseme mimi na tramadol basi na ikawa hivyo japo haikua rahisi...nakumbuka ilikua tabu.

Hatukutumia njia tofauti na hiyo.
 
Halafu pia hiyo dawa haitolewi hovyo hovyo na inatolewa kwa kiasi kwa ajili ya huo utegemezi wake.
Habari viongozi mimi ni mwanamke wa miaka 40 hivi kuna kipindi niliugua sana kiuno nikawa napewa tramadol nikawa nasikia nafuu kubwa sana.

Sasa nimekuwa deoendant siwezi kumeza tramado saivi nameza hadi vidonge vinne kwa pamoja ndo zinafanya kazi. Bila hivo siwezi kufanya chochote bila kumeza tramadol japo kiuno nilipona tangu mwaka juzi lkn nimeendelea kutumia hadi leo
 
Habari viongozi mimi ni mwanamke wa miaka 40 hivi kuna kipindi niliugua sana kiuno nikawa napewa tramadol nikawa nasikia nafuu kubwa sana.

Sasa nimekuwa deoendant siwezi kumeza tramado saivi nameza hadi vidonge vinne kwa pamoja ndo zinafanya kazi. Bila hivo siwezi kufanya chochote bila kumeza tramadol japo kiuno nilipona tangu mwaka juzi lkn nimeendelea kutumia hadi leo
Dawa ni sumu, pata ushauri wa daktari
 
Pole mkuu kwa changamoto lakini your problem it's more of psychology na ulichopata ni drug dependency kwa sababu tramadol ni opioid analgesic pia na mara nyingi hushauriw kutumia muda mrefu sababu huwa zinaleta msisimko flani..

ushauri wangu keep yourself busy and exercise regularly and keep yourself from drugs unaelkea kwenye tolerance which is too bad na dawa zote huwa zina limiting dose so ukizid hapo per 24hrs unakua kwenye high risk ya kupata adverse drug reactions... Be safe na jitahidi
 
Kwanini unatumia kama kiuno kilipona tangu mwaka juzi?unatumia kama starehe/unaenjoy ama?sijaelewa
Nilikuwa natumia kwajili ya maumivu ya kiuno sasa nikatumia muda mrefu kumbe haitakiwi mtu kutumia zaidi ya siku 7.

Sasa mimi nilitumia muda mrefu wakati natibiwa kiuno, kilivyo pona nikajaribu kuacha nikashindwa kila nikiacha maumivu ya mwili yanakuwa makubwa nilipoenda hospital nikaelezea dr akanambia ni tramadol dependat hiyo umeshaathirika.

kunasiku nilijitahidi sana kutokuimeza ila ilifika saa 10 jioni nilishindwa kabisa yani. Nikameza maana walidhani naumwa malaria wakataka kunipeleka hosp ndonikameza nikapona wakashangaa
 
Nilikuwa natumia kwajili ya maumivu ya kiuno sasa nikatumia muda mrefu kumbe haitakiwi mtu kutumia zaidi ya siku 7.

Sasa mimi nilitumia muda mrefu wakati natibiwa .kiuno kilivyo pona nikajaribu kuacha nikashindwa kila nikiacha maumivu ya mwili yanakuwa makubwa nilipoenda hospital nikaelezea dr akanambia ni tramadol dependat hiyo umeshaathirika.

kunasiku nilijitahidi sana kutokuimeza ila ilifika saa 10 jioni nilishindwa kabisa yani. Nikameza maana walidhani naumwa malaria wakataka kunipeleka hosp ndonikameza nikapona wakashangaa

Nimefatilia kwa madaktari wengi nimeambiwa hiyo ni addiction ya tramadol na inapona kwa dawa ya Naloxone sasa hapa Tanzania haipo hadi Kenya au Uganda.
 
nimefatilia kwa madaktari wengi nimeambiwa hiyo ni adiction ya tramadol na inapona kwa dawa ya naloxone sasa hapa tanzania haipo hadi kenya au uganda.
Naomba madaktari wanaojua waweze kunisaidia maana nahisi naweza kuharibu figo au ini
 
Dah,nilikunywa tramadol 6 kwa siku niliandikiwa na dr 2×3 ilkuwa mwaka2014, usiku nilizidiwa sana kidogo nipate stroke.

Kilichonisaidia ni maji, nilikunywa zaid ya Lita nne. Nilitoboa ila mpaka leo hii toka siku hyo huwa kuna kipindi mwili huwa unachoka sana, mpaka ninywe maji mengi sana na kukojoa sana. Baada ya nusu saa huwa narudi normal.
 
nimefatilia kwa madaktari wengi nimeambiwa hiyo ni adiction ya tramadol na inapona kwa dawa ya naloxone sasa hapa tanzania haipo hadi kenya au uganda.
Inawezekana kuiagiza? Why not try that?

Mbona Daktari anakuacha njia panda bado hujapata suluhu ya tatizo lako, sijapenda kwakweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom