#Habari: SEHEMU ZA SIRI ZAYEYUKA BAADA YA KUMUIBIA MWANAUME ALIYELALA NAE!

Jereman

Senior Member
Jun 29, 2016
140
124
Dada mmoja mjini Bukoba akiwa hajielewi kwa kile kilichompata, ajikuta hana sehemu zake za siri (Nyeti Zake) baada ya kulala na mwanaume msukuma katika nyumba ya wageni ya Super star hamugembe na kutoweka na pesa za mwanaume huyo ambae inasemekana ni mkazi wa Misungwi Mkoani Mwanza ambae hufanya biashara ya Ndizi toka Bukoba kwenda Mwanza.

Baada ya kuondoka na pesa za jamaa, muda wa masaa kadhaa hadi anapoishi alihisi kubanwa na haja ndogo ndipo alipoenda chooni kwa lengo la kukojoa.

Lakini Dada huyu alijikuta katika hali ya Mshangao mkubwa na mshituko baada ya kuona hana sehemu zake za siri za kukojolea hali iliyomfanya aonekane kama mtu aliyechanganyikiwa na kupiga mayowe ghafla na kupelekea umati mkubwa wa watu kujaa wakimshangaa pasipokumuelewa. Ndipo akaeleza mwenyewe kuwa kachukua pesa za mwanaume aliyekuwa nae Guest usiku na sasa haoni kitumbua chake.

Baadae Police walifika eneo la tukio na kupata maelezo hivyo kumchukua Binti huyo hadi mahali Guest Ilipo.

Bahati Nzuri Walimkuta Msukuma Huyu Akiwa Bado Yupo Hapo Guest Akiwazia Pesa Zake, Na Binti Alipomuona Alimkimbilia Na Kupiga Magoti Huku Akilia Machozi Akimuomba Chonde Chonde Achukue Pesa Zake Amrudishie Nyeti Zake.

Ndipo Ngosha Huyo Akatoa Kikopo Kidogo Katika Mfuko Wake Wa Suruali Kilichokuwa Na Dawa Za Kiasili Akachanganya Na Maji Na Kumumwagia Mwilini mwake Kisha Akamuambia Atazame Kama Nyeti Zake Zimerudi.

Binti Bila Kujali Umati Wa Watu Alifunua Sketi Yake Na Kujipapasa takribani mara tatu akiwa haamini amini Na Kukuta Imerudi Kama Ilivyokuwa Mwanzo na kupaza sauti ""Ipoo Ipoo Imerudiiiii" Binti Alilia Sana Na Kumuomba Jamaa Amsamehe Sana Na Kuahidi Hatorudia Tena Mchezo Huo Wa Kuwaibia Wanaume Hasa Wageni Asiowajuwa.

Jamaa Akamwambia Nishakusamehe Ila Kuwa Makini Watu Wengine Huwa Hatuibiwi Ovyo Ovyo.! Kesi Ikaishia Pale Na Watu Wakatawanyika japo Ngosha Katoa Fundisho.
 
Back
Top Bottom