The Conquerer
Member
- Aug 16, 2012
- 79
- 94
Haya picha mlizotaka hizo hapo. Nilikuwa busy sikuweza ku - upload mwanzoni.
Mambo aliyozungumzia ni kama ifuatavyo:
1. Serikali isizime tv za analogia kwani wananchi masikini hawataweza kununua ving'amuzi kwa ajili ya kuangalia tv za mfumo wa digitali. Kuwe na uhuru wa kutumia mifumo yote.
2. Waziri mkuu aweke hadharani bajeti ya mwenge (kiasi cha fedha kinachokusanywa na matumizi yake)
3. Rais kikwete aache propaganda za kusema anasifika kimataifa na badala yake ashughulikie kero za wananchi kwa kuwa kero hizo haziondolewi na umaarufu wake kimataifa.
4. Polisi waache kuwanyanyasa wananchi kwani kwa kufanya hivyo wanajitengenezea mazingira ya kuwa wafungwa katika nchi yao pindi serikali ya ccm itakapoangushwa
5. Waziri wa mali asili na utalii arudishe wanyama pori waliouzwa nje kwa kuwa kitendo cha kuuza wanyama pori wetu nje kutafanya watalii wasije tena nchini mwetu na hivyo kuendelea kupoteza mapato na kuwa wategemezi zaidi
6. Serikali iache kukopa kopa nje kwa miradi ya maendeleo na badala yake itumie mapato ya rasilimali zetu kuendesha miradi ya maendeleo