Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,873
Baadhi yetu tumekuwa na matatizo sana na ofisi ya DPP kwani kwa muda mrefu tumeamini imekuwa ni kikwazo katika vita dhidi ya ufisadi. Mimi (kama wengine) nimeamini kwa muda mrefu kuwa kama DPP atashindwa kutumia madaraka yake vizuri basi vita dhidi ya ufisadi haiwezi kupiganwa vizuri na Mahakama, Polisi, TISS, CAG na wengine. DPP katika vita hii ni kama kapteni wa mapambano; akizembea wengine watazembea, akisita wengine watasita.
Lengo la mabadiliko ya Sheria ya ofisi yake yaliyofanyika 2007 yalikuwa na lengo kubwa sana la kumpatia na kumhakikishia uhuru zaidi lakini pia kumsukuma (promt) yeye mwenyewe kufanya mambo bila kusubiri "wakubwa" waamue. Bahati mbaya Eliezer Feleshi alituangusha sana na kuliangusha taifa na ni matumaini yangu huyu wa sasa ataweza kutumia madaraka ya vizuri kwani tayari ameona mwendo uliopo.
Hivyo, kuitwa kwake Ikulu kwenda kuonana na Rais Magufuli kuna lengo moja -kumpatia baraka zote za kutumia ofisi yake bila upendeleo, woga, kusita au kusubiri kuuliza kwa mtu mwingine kama "fulani akamatwe au la". Watanzania watarajia hati za watu kukamatwa au kushikiliwa mali zao kuanza kutolewa mapema zaidi na kuna watu watakamatwa na taifa litashtuka. Kama watu kubanwa kodi tu wameenda kulia kwa yule mwingine ngoja kamata kamata ianze.
DPP Mganga (Pichani juu na Rais Magufuli Ikulu jana) huyu akishindwa kufuata mwendo atasukumwa nje; Hosea hakuwa peke yake katika kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi. Tunasubiri tuone na RO naye watamuambia nini (kama siyo kustaafu kama alivyotakiwa).
MMM
Last edited by a moderator: