Habari Njema Zenji: Juhudi za Mhe. Balozi Amina S. Ali zazaa matunda, TradeMark yamwaga madola! | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari Njema Zenji: Juhudi za Mhe. Balozi Amina S. Ali zazaa matunda, TradeMark yamwaga madola!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, May 19, 2017.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,710
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kwenye Jukwaa la Siasa humu JF, ukizungumzia Zanzibar, mind za wengi zinakwenda straight kwenye dhana potofu na uongo kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa!. Kiukweli Zanzibar hakuna mgogoro wowote wa kisiasa, uchaguzi mwingine ni 2020,
  Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ...
  hivyo nashauri wana JF, tujikite kwenye kuzungumzia maendeleo ya Zanzibar.

  Leo asubuhi, nimeamkia kwenye taarifa hii kutoka MFA kuihusu Zanzibar.
  Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation: Zanzibar ...

  Kwenye taarifa kuhusu Zanzibar kusaidiwa na TMEA, nimekuta paragraph hizi mbili

  "Aidha, kwenye miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar haijasahaulika. Zanzibar inanufaika na miradi inayofadhiliwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya kukuza biashara na kupunguza umasikini katika nchi za EAC inayoitwa "East Africa Trademark" (TMEA). TMEA ambayo ni mdau mkubwa wa EAC inafadhili mradi ambao unawawezesha Wazanzibari kufanya maombi kwa njia ya mtandao ili kupata cheti cha uasili wa bidhaa. Cheti hicho ni muhimu kwa wafanyabiashara kwani kinatambulisha bidhaa yako ilipotengenezwa na kupata msamaha wa kodi ya forodha inapoingia nchi nyingine za EAC".

  "Mradi mwingine unaofadhiliwa na TMEA huko Zanzibar ni ule wa kuwasilisha malamiko kwa njia ya mtandao au ujumbe mfupi wa simu pale inapotokea mfanyabiashara amekumbana na vikwazo visivyo vya forodha katika kusafirisha bidhaa zake ndani ya Jumuiya. Ujumbe huo utakapopokelewa, kikwazo kilicholalamikiwa kitafanyiwa kazi na taasisi husika mara moja".

  Hii ni habari njema sana kwa maendeleo ya Zanzibar, kwa sababu nilipata kuhudhuria tukio fulani, ambapo Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipofunga safari kutoka Zanzibar na kuja hadi TMEA. Naomba kwanza ushuhudie, Balozi Amina alikuja kufanya nini TMEA.  Na kweli baada ya muda, juhudi hizi zikazaa matunda. Angalia baada ya ziara hiyo, TMEA walifanya nini Zanzibar...

  TradeMark East Africa Yawezesha Zanzibar kutumia SMS Kuripoti ...


  Habari kama hizi, ndizo habari za kimaendeleo, wana JF tujikite zaidi kwenye kujadili habari za kiuchumi na za kimaendeleo zenye manufaa kwa taifa, badala ya kutwa kuchwa kujadili habari za kisiasa tuu, na tena habari nyingine, hazina hata manufaa yoyote kwa taifa letu!.

  Hongera sana Balozi Amina Salum Ali, juhudi zako zimeanza kuzaa matunda. Hongera TradeMark East Afrika, juhudi zenu na michango yenu yaanza kuthaminiwa na serikali ya JMT.

  Hongera pia MFA kwa kutambua juhudi za TMEA.

  Paskali
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #21
  May 19, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu Retired, sijasema tusijadili matukio, bali nimeshauri tusikalie kutwa kutwakujadili siasa ambazo hazina manufaa.

  Mimi ni mwandishi wa kujitegemea ambaye nimejikita kwenye kuandika habari za kimaendeleo tuu zenye manufaa kwa taifa.

  Nakiri udhaifu wangu, kuwa nina udhaifu mmoja mkubwa ambao umeisha ni cost sana sio kimaisha tuu hadi kwenye familia. Udhaifu wangu ni kuwa mkweli tuu much!. Mimi ni mkweli daima. Kuanzia kwenye familia, society, kazini na hadi humu jf.

  Wife anaishi US mpaka kesho, hivyo distance relationships, wanaziweza baadhi ya wenzetu wakiwemo Wachagga. Wife ni Mchagga anaishi US mimi naishi Bongo!. Visitation ni once a year!, mimi ni mtu wa Kanda ya Ziwa, kusubiri mwaka hadi mwaka hatuwezi, hivyo akasikia ni nilipokwenda nikawa mkweli!, this costed me!.

  Nilipokuwa TBC niliendesha vipindi vya siasa na kutoa haki sawa kwa vyama vyote wakati wa uchaguzi wa 2000. Nikatuhumiwa kuwa mimi ni pro opposition, nikatumiwa watu wa GSU kunichunguzana nikaitwa kuhojiwa mbele ya mkurugenzi wangu wa TBC ya wakati huo, na nikatoa ukweli kabisa wa ndani ya nafsi yangu kuwa mimi sio pro opposition ila sio pro CCM, sina chama!. This costed me my job at TBC!.

  Mpaka sasa nasimama kwenye ukweli kuwa sina chama, sijikombi kwa yoyote, simtegemei yoyote kwa favours zozote!.

  Kwenye hili la Zanzibar, nimelizungumza sana humu, ukweli halisi ni the end that justify the means kuwa hsakuna chochote kitakachofanyika ksabla ya 2020!, tuukubali ukweli mchungu huu
  Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
  ,
  tujikite kwenye kujadili maendeleo!.

  Hii Mayalla ya njaa, ni jina tuu, lakini mtu mwenyewe ni masikini jeuri!, hanunuliki kwa bei yoyote!.

  Paskali
   
 3. g

  gromiko Member

  #22
  May 19, 2017
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 25
  Maneno yako yamefanya niukubali ule utani unaosema, Mlevi mmoja wa kipemba akili na uwezo wake wa kufikiri ni sawasawa na msomi mmoja mwenye PHD wa kibara.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #23
  May 19, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,710
  Trophy Points: 280
  Miss Natafuta, jirani wasiotembeleana, long time?!.
  Karibu uwatembelee
  Tanzania | TradeMark East Africa

  Paskali
   
 5. Miss Natafuta

  Miss Natafuta JF-Expert Member

  #24
  May 19, 2017
  Joined: Sep 16, 2015
  Messages: 19,051
  Likes Received: 31,557
  Trophy Points: 280
  nitakutafuta leo mkuu jioni ila umezeeka sana pascal why? nasikia unapelekwa moshi kuwa rc
   
 6. R

  Retired JF-Expert Member

  #25
  May 19, 2017
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 11,678
  Likes Received: 14,127
  Trophy Points: 280
  Paskali, kwa weledi wako, nilitegemea uandike kuwa pamoja na matatizo yetu say ya akina Ben Saanane, Ney wa Mitego, Clouds, matukio ya polisi, Zanzibar politics etc, uwahimize waandishi wasiache kuandika habari za maendeleo na si kusema kwa ushujaa kabisa kuwa Zanzibar hakuna shida. I am quoting your sentense iliyonipa ukakasi "Kwenye Jukwaa la Siasa humu JF, ukizungumzia Zanzibar, mind za wengi zinakwenda straight kwenye dhana potofu na uongo kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa!. Kiukweli Zanzibar hakuna mgogoro wowote wa kisiasa, uchaguzi mwingine ni 2020," This is the most disturbing part of your post! Otherwise, kuandika maendeleo ni part ya mwandishi mzuri!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #26
  May 19, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu Khamisiya, yote haya usemayo hapa ni kweli tupu, kitu ambacho hukukisema kwa kutokujua, ni sii wewe tuu bali Wanzanzibari wengi hawajui asili ya Zanzibar ni bara!.

  Paskali.
  Kama una muda na unapenda kujielimisha karibu pande hizi...
  Wazanzibar wote ni wageni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
  Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa ...
  Swali: Je Unafaham Hili Juu Ya Zanzibar? | JamiiForums | The Home ...
  Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...
  Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi ...
  Balozi Karume: 'CCM pekee iwe inasimamisha mgombea urais Zanzibar ...
  Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano ...
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #27
  May 19, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu Retired, pole sana, huo ndio ukweli halisi, ndio ukweli wenyewe kuwa kuwepo kwa mgogoro ni dhana tuu ndani ya mawazo na vichwa vya watu, lakini in reality hakuna mgogoro wowote!. Huu ndio ukweli wenyewe japo mchungu.

  Pole.

  Paskali
   
 9. Miss Natafuta

  Miss Natafuta JF-Expert Member

  #28
  May 19, 2017
  Joined: Sep 16, 2015
  Messages: 19,051
  Likes Received: 31,557
  Trophy Points: 280
  nasikia mafuriko ya pemba yanashughulikiwa kisiasa .kwanini ? kwa vile wengi ni CUF AU VIPI MKUU ?.
   
 10. u

  usemwe JF-Expert Member

  #29
  May 19, 2017
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 205
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Hakuna mgogoro ? Really ?
   
 11. t

  treborx JF-Expert Member

  #30
  May 19, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 4,442
  Likes Received: 2,031
  Trophy Points: 280
  Kinacho-trend huko Zanzibar kwa sasa ni Mafuriko ya mvua Pemba.
   
 12. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #31
  May 19, 2017
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 11,249
  Likes Received: 12,178
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo ukimjadili Ben Saa nane ndio bibi yako atakuwa masikini. Mpaka leo bibi, baba yako na ww mwenyewe bado ni masikini, hiyo ilisababishwa na ww kumjadili au kutomhadili Ben Saanane? Acha hoja za kitoto dogo.
   
 13. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #32
  May 19, 2017
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 30,611
  Likes Received: 4,264
  Trophy Points: 280
  pongezi....
   
 14. R

  Retired JF-Expert Member

  #33
  May 19, 2017
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 11,678
  Likes Received: 14,127
  Trophy Points: 280
  Paskali, let us argue philosophically. Let first define the word "mgogoro" . Tukikubaliana kwenye definition moja, then tutakuja kuona kama kuna mgogoro au hakuna.
  Mfano: Is a whale a Fish? Kujibu swali hilo lazima kwanza tukubaliane definition ya Fish ie characteristics of a fish. Tukikubalina hapo kuwa fish ana characteristics hizi, then tunaangalia kama Whale ana hizo characteristics.
  Let me do something else, then If you do not mind I will revert to this controversy later! ( To define is to say what a thing is and what it is not)
  Paskali huwa nakuheshimu sana ninapokuonaga unahoji watu uwanja wa Taifa sabasaba! Clever. Swali la JPM lilikuwa swali of the Century. nadhani katika maswali yaliyowahi kuulizwa hapa tangu tupate uhuru kwa weledi linaingia kwenye rekodi. Lakini kwa mwendo unaokwenda nao, tutakuwa na mashaka kama lile swali hukupewa na mtu uulize. It was a very challenging question!
   
 15. Masanyiwa Mabula

  Masanyiwa Mabula JF-Expert Member

  #34
  May 19, 2017
  Joined: Jan 24, 2017
  Messages: 963
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 180
  USHANUNULIWA WW SIYO BURE. HAUFANANI NA MTANGAZAJI KBSA BALI MTU ANAYETUMIWA.
  Una safari ndefu sana Pascal ya kuufikia utangazaji bora ila kwasasa umekuwa mtangazaji Kasuku.
  Najua kila mtu anapenda siasa, lkn kuna baadhi ya taaluma hazitaki mambo ya siasa kbsa. Ktk taaluma yako haipaswi kuchanganywa na siasa kbs. Inabid ukae mbali na siasa ni sawa na maji na mafuta.
  "UNAPASWA KURIPOTI HABARI NA KUHARIRI BILA KUEGEMEA UPANDE WWTE WA VYAMA VYA SIASA HATA KM UNA MAHABA NA CHAMA FULANI"
  Tangu siku ile ulipomuuliza mkulu swali na watu wakakupongeza ushakuwa mjinga wa mwisho. TAALUMA YAKO UMEACHA KULIA NA WW UNAPITA KUSHOTO. Sasa hiv ushachuja hauna tofauti na wale wa buku 7.
  Kaa kweny taaluma yako, utulie na ufanye vitu vyako pasipo kuegemea kweny chama fulan hata km una mahaba nacho. Nilikuwa nakuamini sana lkn sasa hiv nikikuta uzi wako hauna tofauti na walumumba buku 7
  Sasa hiv sikufagiliii wala nn, naona km mshenzy fulani tu anayeabisha taaluma ya uandishi wa habari.
  Nilitegemea ww utakuwa unareport habari humu na kuleta mijadala fikirishi bila kuegemea upande wwte. Hizo buku 7 zako zikiisha utakuwa sawa na Ray wa bongo movie
   
 16. Masanyiwa Mabula

  Masanyiwa Mabula JF-Expert Member

  #35
  May 19, 2017
  Joined: Jan 24, 2017
  Messages: 963
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 180
  Kiukweli mgogoro wa kisiasa upo tena mkubwa ni sawa na mto. Juu maji yametulia ila ndani yanaenda kwa kasi. Hii ilisabibishwa na Jecha. Iliathiri sana ila kwass ni mto.
  Ukifika kweny uchaguzi(kipind cha masika) ndiyo utaona hali halisi ya mto.
  Huyu keshanunuliwa, mada zake nying sasa hiv hazieleweki kbsa. Na hii asipoingalia itamcost sana.
  Awangalie wenzake km Millard Ayo
   
 17. R

  Retired JF-Expert Member

  #36
  May 19, 2017
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 11,678
  Likes Received: 14,127
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wewe usipomjadili bibi yako anafaidika? ndiyo maana nasema hujaenda shule! Huwezi toa reasoning kama hiyo! Tunajadili kwa faida ya wengi, wasipotezwe kwa kuhoji ukweli wa mambo, wasipotezwe kwa kuuutaka ukweli! and the like siyo ya issue ya bibi kufaidika. Akina mandela waliteseka kwa kuutetea ukweli na si kufaidika bibi zao!
   
 18. R

  Retired JF-Expert Member

  #37
  May 19, 2017
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 11,678
  Likes Received: 14,127
  Trophy Points: 280
  Paskali, unaona, tulikuwa na tegemeo kubwa kwako kama mwandishi fikirishi. Angalia alivyokuandika vizuri huyu Mabula?? kama swali lako lilivyokuwa fikirishi, kila mmoja alikupongeza kwa weledi wa hali ya juu. Najua uko hivyo. Au labda ulitishwa, ukatishiwa kupotezwa kama Ben, na sasa unaweka mambo sawa!
  Paskali, unaona, tulikuwa na tegemeo kubwa kwako kama mwandishi fikirishi. Angalia alivyokuandika vizuri na huyu Mabula, **** swali lako lilivyokuwa fikirishi, kila mmoja alikupongeza kwa weledi wa hali ya juu. Najua uko hivyo, una weledi mkubwa tu!. Au labda uliitwa, ulitishwa, ukatishiwa kupotezwa kama Ben, na sasa unaweka mambo sawa!
   
 19. B

  Babati JF-Expert Member

  #38
  May 19, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,845
  Likes Received: 25,105
  Trophy Points: 280
  Hongera zao Wazanzibar
   
 20. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #39
  May 19, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 17,503
  Likes Received: 19,318
  Trophy Points: 280
  hapana du!
   
 21. ISIS

  ISIS JF-Expert Member

  #40
  May 19, 2017
  Joined: Apr 20, 2016
  Messages: 68,640
  Likes Received: 412,190
  Trophy Points: 280
  Well said
   
Loading...