Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,646
- 119,250
Wanabodi,
Kwenye Jukwaa la Siasa humu JF, ukizungumzia Zanzibar, mind za wengi zinakwenda straight kwenye dhana potofu na uongo kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa!. Kiukweli Zanzibar hakuna mgogoro wowote wa kisiasa, uchaguzi mwingine ni 2020,
Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ...
hivyo nashauri wana JF, tujikite kwenye kuzungumzia maendeleo ya Zanzibar.
Leo asubuhi, nimeamkia kwenye taarifa hii kutoka MFA kuihusu Zanzibar.
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation: Zanzibar ...
Kwenye taarifa kuhusu Zanzibar kusaidiwa na TMEA, nimekuta paragraph hizi mbili
"Aidha, kwenye miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar haijasahaulika. Zanzibar inanufaika na miradi inayofadhiliwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya kukuza biashara na kupunguza umasikini katika nchi za EAC inayoitwa "East Africa Trademark" (TMEA). TMEA ambayo ni mdau mkubwa wa EAC inafadhili mradi ambao unawawezesha Wazanzibari kufanya maombi kwa njia ya mtandao ili kupata cheti cha uasili wa bidhaa. Cheti hicho ni muhimu kwa wafanyabiashara kwani kinatambulisha bidhaa yako ilipotengenezwa na kupata msamaha wa kodi ya forodha inapoingia nchi nyingine za EAC".
"Mradi mwingine unaofadhiliwa na TMEA huko Zanzibar ni ule wa kuwasilisha malamiko kwa njia ya mtandao au ujumbe mfupi wa simu pale inapotokea mfanyabiashara amekumbana na vikwazo visivyo vya forodha katika kusafirisha bidhaa zake ndani ya Jumuiya. Ujumbe huo utakapopokelewa, kikwazo kilicholalamikiwa kitafanyiwa kazi na taasisi husika mara moja".
Hii ni habari njema sana kwa maendeleo ya Zanzibar, kwa sababu nilipata kuhudhuria tukio fulani, ambapo Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipofunga safari kutoka Zanzibar na kuja hadi TMEA. Naomba kwanza ushuhudie, Balozi Amina alikuja kufanya nini TMEA.
Na kweli baada ya muda, juhudi hizi zikazaa matunda. Angalia baada ya ziara hiyo, TMEA walifanya nini Zanzibar...
TradeMark East Africa Yawezesha Zanzibar kutumia SMS Kuripoti ...
Habari kama hizi, ndizo habari za kimaendeleo, wana JF tujikite zaidi kwenye kujadili habari za kiuchumi na za kimaendeleo zenye manufaa kwa taifa, badala ya kutwa kuchwa kujadili habari za kisiasa tuu, na tena habari nyingine, hazina hata manufaa yoyote kwa taifa letu!.
Hongera sana Balozi Amina Salum Ali, juhudi zako zimeanza kuzaa matunda. Hongera TradeMark East Afrika, juhudi zenu na michango yenu yaanza kuthaminiwa na serikali ya JMT.
Hongera pia MFA kwa kutambua juhudi za TMEA.
Paskali