Habari njema za scholarship (India) kwa course za Diploma / Degree

kityentyee

Member
Mar 9, 2021
72
338
Habari zenu wakuu, Kwanza kabisa ninayo furaha kuwatangazia nafasi za masomo nchini India (Scholarship) kwa wale wenye ndoto ya kwenda kusoma nje ya nchi.

Utaratibu upo hivi, kwa yeyote mwenye nia ya kwenda kusoma nchini India kwa course yoyote hasa Afya, Uhandisi,na cousre nyinginezo za Science kwa ngazi ya Diploma au Degree basi jibu la ndoto yake ya kwenda kusoma huko limeshapatikana.

JAIN UNIVERSITY, MARWAD UNIVERSITY pamoja na LPU wanatoa scholarship hizo kwa kwa budget ya USD 2500 kwa mwaka. Sambamba na hilo vyuo vitagharamia Nauli ya ndege ya mwanafunzi, chakula, malazi pamoja na huduma zote muhimu za mwanafunzi katika kipindi chote atakachokua masomoni.

Deadline ya hizi nafasi ni mwisho wa mwezi huu november 2022.

AHSANTE
 
Link ?
 
Mimi ni agent ambae nimeingia Ubia na hivyo vyuo kutafuta wanafunzi, so yeyote atakayekua yupo interested atahitajika kunitumia or kunipatia details zifuatazo;
20221105_164423.jpg
 
Je, kuna malipo yoyote natakiwa kukulipa wewe au kulipia gharama zozote kipindi tupo kwenye mchakato wa kufanya application au baada ya application?
 
Hiyo application form mie ndio nitakayeishughulikia, then baada ya hapo kutafanyika proofchecking ya kuthibitisha kama mtu amequalify then kuna test fupi itafanywa ONLINE halafu baada ya hapo atapewa go ahead ya yeye kuanza process za kutafuta passport (kwa wale ambao hawana), then atafuatilia VISA, akishapata Visa yake mie nitatoa report kwamba yeye kapata visa then baada ya hapo Ticket inatumwa anaondoka zake, akifika huko akipokelewa namie napewa changu then maisha yanaendelea ndugu zangu Tupeane support tu japo hata kwa kuwasambazia na wengine.

NOTE
Kuhusu deadline wala mtu isimpe tabu kuna namna huwa natoa Excuse kwa wanafunzi watakao chelewa then Chuo husika kinaandaa Batch ya wachelewaji wanaandaliwa kama revision session flani ya kuweza kuwaboost ili waweze kwenda sambamba na wenzao waliowatangulia
 
Hiyo achana nayo mkuu ,,deal na hizo details zingine tu kushuka chini
Masters na phd hakuna? Na hizo details mtu anakutumia kwa njia gani? Unaonaje ungeandaa form then ukashare hapa watu waijaze hizo details then wakutumie kwa email, kuliko hivi ulivyofanya
 
Masters na phd hakuna? Na hizo details mtu anakutumia kwa njia gani? Unaonaje ungeandaa form then ukashare hapa watu waijaze hizo details then wakutumie kwa email, kuliko hivi ulivyofanya
Ukiwa interested unazama tu inbox nakutumia whatsapp no. then maisha yanaendelea bro, but thanks for your genuine Idea mkuu
 
Hizi zinakuwa kama fursa baadae inakuwa fursana, mtu anakula za uso huko.. Kuna haja gani aje pm sijui whatsapp, hakuna link, why kila kitu ufanye wewe, ndio mwishoni utaanza kusema inahitajika 250k sijui ya nini nini, mtu anakula za kichwa.
 
Masters na phd hakuna? Na hizo details mtu anakutumia kwa njia gani? Unaonaje ungeandaa form then ukashare hapa watu waijaze hizo details then wakutumie kwa email, kuliko hivi ulivyofanya
kuhusu masters na phd pia zipo mkuu ila zenyewe zina vary from $2500 ~ $3000, ni wewe tu boss, japo kuna time huwa wananipa pia tender ya kutafuta wanafunzi wa FULL FUNDED SCHOLARSHIP mfano last month nimepeleka India wanafunzi 23 wa full funded 14 wa degree, 7 wa diploma na 2 wa masters
 
Mtalizwa sio muda mrefu bahati mbaya Jamii forum nayo siku hizi great thinkers hakuna so hawatahoji mambo ya msingi!!
 
Naona wasiwasi flani Kwa sababu hizi hapa chache:
1. Kwa nini wewe ndo ufanye process za documents
2. Kuna ubayq gani ukitoa link/website husika watu waperuzi kujiridhisha.
3. Gharama halisi zakufanya mchakato mzima?
 
Hizi zinakuwa kama fursa baadae inakuwa fursana, mtu anakula za uso huko.. Kuna haja gani aje pm sijui whatsapp, hakuna link, why kila kitu ufanye wewe, ndio mwishoni utaanza kusema inahitajika 250k sijui ya nini nini, mtu anakula za kichwa.
Mkuu kama utakua na passport yako ,,ukafight mwenyewe kupata visa then mie nikakupatia tu ticket yako ukaenda halafu ukifika huko mie napewa changu na chuo husika ,,wapi ambapo unahisi mie nitakupiga za kichwa kama usemavyo boss, maamuzi ni yako tu boss, maana I've been doing these things since last september of last year 2021 kwa vyuo vya Turkey, Cyprus na India. so Maamuzi ni yako tu boss ila sijakuzuia pia kunishauri namna bora ya kufanya biashara yangu iwe more profession maana Ajira zenyewe hamna ndugu yangu ila tunajitahidi kutumia fursa zilizopo kupata rizki katika namna ya uhalali boss bila dhulma
 
Hizi zinakuwa kama fursa baadae inakuwa fursana, mtu anakula za uso huko.. Kuna haja gani aje pm sijui whatsapp, hakuna link, why kila kitu ufanye wewe, ndio mwishoni utaanza kusema inahitajika 250k sijui ya nini nini, mtu anakula za kichwa.
Mkuu
Acha Vijana Wakasomee Fursa Baadaye Fursana
 
Mtalizwa sio muda mrefu bahati mbaya Jamii forum nayo siku hizi great thinkers hakuna so hawatahoji mambo ya msingi!!
As long as I am a muslim, In the name of Allah aliyeniumba mie, I swear that Wallah, wabillah watallah bro mikono yangu haina harufu ya aina yoyote ya dhulma katika hili ndugu yangu, ila tu ni vile watu wameshapigwa na vitu vizito sana kiasi kwamba hawana imani kabisa na hizi mambo, anyway to make it short wakuu ni kwamba huwa natoa nafsi ya mtu kunijua physically ikiwa ni pamoja na kumuonesha vibali vyangu vyote vya kisheria vinavyoniruhusu mie kufanya hizi mishe
 
Mtalizwa sio muda mrefu bahati mbaya Jamii forum nayo siku hizi great thinkers hakuna so hawatahoji mambo ya msingi!!
Tanzania Hatuna Tabia Hizo
Pesa Watu Wanazo Ni Kutengeneza Mazingira Mazuri Unajipigia Kama Ngoma Unatembea Kifua Mbele Tu
 
Back
Top Bottom