Habari Njema:Timu ya Taifa Brazil kufanya mazoezi Uwanja wa Taifa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari Njema:Timu ya Taifa Brazil kufanya mazoezi Uwanja wa Taifa Dar

Discussion in 'Sports' started by Shadow, Apr 18, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Na Vicky Kimaro  TIMU ya taifa ya Brazil ikiwa na wachezaji wake mashuhuri Kaka, Robinho na Ronadinho wanategemewa kuja nchini kuweka kambi kwa wiki moja kabla ya safari yake ya Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia 2010.


  Hayo yalisemwa na kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo siku chache baada ya rais wa TFF, Leodegar Tenga kukaririwa akisema kuwa hivi karibuni shirikisho lake kwa kushirikiana na serikali watazindua kampeni ya kuhamasisha timu zinazoshiriki kombe la dunia kuja kuweka kambi hapa nchini.


  Marcio Maximo alisema tayari ameshaanza mazungumzo na mkurugenzi wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) ili timu hiyo iweke kambi ya wiki moja hapa nchini.


  ìNimetumia muda mwingi wa mapumziko yangu kuitangaza Tanzania, nimeongea na mkurugenzi wa CBF ameniahidi kumwalika Tenga rasmi Brazil kuzungumzia suala hili,î Tenga ataenda kama rais wa TFF na mwenyekiti wa CECAFAî.


  ìMsumbiji na Angola nao wanafukuzia nafasi hii kwa vile wao wanaongea Kireno hivyo si kazi rahisi kushawishi kuja hapa, ila tutajaribu natumaini mambo yatakuwa mazuri,î alisema Maximo.


  Maximo ambaye alikuwa mapumziko nchini kwao Brazil alisema wakati akiwa huko alipata fursa pia ya kuzungumza na wachezaji Robinho na Kaka ambao walikuwa waje nchini kama mabalozi wa UNICEF, lakini hivi sasa wanashiriki ligi kuu zinazoendelea barani ulaya hivyo itakuwa vigumu kuja huku kwani ziara itawachukua wiki moja kitu ambacho hakitakuwa rahisi kwao kwa hivi sasa.


  Alisema wachezaji hao wamempongeza na kumsifia kwa kuipandisha chati Tanzania katika medani ya soka.

  Wakati huo huo, pia Maximo alisema yupo kwenye mchakato wa kusaka makocha watakaomrithi Itamar Amorin na Marcus Ticono na jukumu la kuwasaka makocha hao amelikabidhi kwa mkurugenzi wa Shirikisho la Soka la Brazil ambaye atamuunganisha na rais Tenga katika kufanikisha zoezi hilo.

  Source:Mwananchi Read News
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mhhh! nahisi kama ndoto vile...sijui kama si tetesi ngoja tusubili.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Nsumbiji na Angola wana nafasi kubwa pia sisi tujipendekeze kwa usa,uk au germany....au hata japan au holland
   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 857
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Huu ni usanii wa Maksimo, eti Kina Kaka na Robinho wanaizimia sana Taifa Staz, hiyo inatusaidia nini bila kushinda vikombe au kwenda kwenye fainali kubwa?
   
Loading...