Habari Njema na Mbaya: Takribani 80% ya visa vya COVID19 haviambatani na dalili kali au za kutishia maisha

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Katika visa vilivyobainika duniani vya #CoronaVirus, asilimia 15 tu huambatana na dalili ya ugonjwa hatari wa mapafu “pneumonia”, kushindwa kupumua, oksijeni kupungua kwenye damu na matatizo mengine ya mapafu

Asilimia takribani 5 huambatana na dalili hatarishi zaidi zinazoweza pelekea kifo kama kufeli kwa mfumo wa upumuaji au kufeli kwa viungo kadhaa vya mwili

Asilimia takribani 80 ya visa vyote viliambatana na dalili za wastani kama homa, kikohozi na mafua

Wakati hii ikiwa ni habari njema kwani dalili husika ni rahisi kutibiwa, ni habari mbaya kwani kuna wengi wasio na dalili za kutilia shaka ambao ni rahisi kuambukiza wengine

Wasio na dalili kali ni rahisi kuendelea na shughuli zao za kila siku, kwenda kwenye mikusanyiko wakihisi wako salama

Kumbuka kuendelea kuchukua tahadhari hususani kipindi hiki ambapo shughuli zinaelekea kurejea katika hali ya awali

===
From WHO Website:

For COVID-19, data to date suggest that 80% of infections are mild or asymptomatic, 15% are severe infection, requiring oxygen and 5% are critical infections, requiring ventilation.
 
Covid19 tutaizoea tu kama tulivyozoea malaria, UTI, cholera, mafua nk. Hatuwezi kuendelea na lockdowns, shutdowns, isolation, curfews na vitu vya namna hiyo. Maisha lazima yaendelee.

Maisha yetu na jinsi ya kuinteract itabadilika sana though. Kubeba sanitizer na kuepuka mikusanyiko isiyo lazima ndio itakuwa mpango mzima moving forward
 
Katika visa vilivyobainika duniani vya #CoronaVirus, asilimia 15 tu huambatana na dalili ya ugonjwa hatari wa mapafu “pneumonia”, kushindwa kupumua, oksijeni kupungua kwenye damu na matatizo mengine ya mapafu

Asilimia takribani 5 huambatana na dalili hatarishi zaidi zinazoweza pelekea kifo kama kufeli kwa mfumo wa upumuaji au kufeli kwa viungo kadhaa vya mwili

Asilimia takribani 80 ya visa vyote viliambatana na dalili za wastani kama homa, kikohozi na mafua

Wakati hii ikiwa ni habari njema kwani dalili husika ni rahisi kutibiwa, ni habari mbaya kwani kuna wengi wasio na dalili za kutilia shaka ambao ni rahisi kuambukiza wengine

Wasio na dalili kali ni rahisi kuendelea na shughuli zao za kila siku, kwenda kwenye mikusanyiko wakihisi wako salama

Kumbuka kuendelea kuchukua tahadhari hususani kipindi hiki ambapo shughuli zinaelekea kurejea katika hali ya awali

===
From WHO Website:

For COVID-19, data to date suggest that 80% of infections are mild or asymptomatic, 15% are severe infection, requiring oxygen and 5% are critical infections, requiring ventilation.

Ukweli mchungu at least 12% wanakufa.

Tofauti inakuja kwa sababu ya kutokufahamu fika kwa kila mgonjwa nini kimemwua e.g. kibongo bongo kukataa kupima wafu au wagonjwa, kuficha takwimu kwa manufaa binafsi, kutokuwa na miundo mbinu wezeshi ya upimaji nk.

Wanaokufa si wachache kihivyo.

Wengi wanaofia majumbani hasa katika nchi zinazoendelea hawawi account for kwa huu ugonjwa hata kama ndiyo uliowauwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom