Habari njema mahakamani kwa Karamagi, Muhongo, Ngeleja na Yona ni Magufuli na Ndugai

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mahakama huendeshwa na doctrine au itikadi ya haki bila upendeleo.

Kauli tata za Magufuli na Ndugai za kuwakingia watuhumiwa nambari moja ufisadi wa Madini akina Mkapa na JK ni utetezi tosha kwa Muhongo, Karamagi, Yona na Ngeleja.

Watakapowapeleka mahakamani mawaziri wa zamani wa Madini watakuwa na utetezi wa aina tano:-

1) Moja, "collective responsibility" yaani uwajibikaji wa pamoja katika baraza la mawaziri kwa hiyo hawawezi kutolewa kafara kwa kutekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri.

Mahakama itawaachia huru kwa sababu tu wamebaguliwa na haki zao za kikatiba za kutendewa sawa na wajumbe wote wa baraza la mawaziri hususani wenyeviti wa vikao hivyo ambao ni Mkapa na JK. Utetezi huu unaitwa "misjoinder of the accused".

2) Kutomshtaki JK wakati alipokuwa waziri wa Mambo ya Nje miaka ya 1997-2000 wakati mikataba ya Bulyanhulu na mingineo ilisainiwa baada ya kupitishwa na baraza la mawaziri na hakuwa na kinga ya Urais kwenye vipindi tajwa na kutomshtaki ni kuwabagua mawaziri walioshtakiwa na utetezi wa " misjoinder of the accused" ni haki yao na lazima wapewe kwa kuachiwa huru.

3) Sheria ya wawekezaji ya mwaka 1997, sheria ya madini ya 1998 na hata ya 2010, sheria za kodi kuanzia 1998-2004 zilirandana na sera ya CCM ya kuvutia wawekezaji. Wao kwa kusaini mikataba husika walikuwa wakitekeleza sheria na misamaha walioitoa ni kuharakisha kasi ya kuwavutia wawekezaji.

Utetezi hapo ni kuwa hakuna jinai katika kutekeleza sera na sheria za nchi. Hakuna mahakama itawatia hatiani kwa hili.

4) Kauli zembe za Magufuli na Ndugai zinaingilia uhuru wa DCI, DPP, TAKUKURU na Mahakama kwa kuwasafisha watuhumiwa wakuu wa ufisadi ambao ni Mkapa na JK huku watuhumiwa Muhongo na wenzie wakitajwa na taarifa za kamati zilizoundwa na Rais kukidhi kiu za kisiasa na kuwatoa watuhumiwa tajwa kama makafara ya kisiasa haiwezekani vyombo vya utoaji haki kama mahakama viwatendee haki.

Kwa kuhukumiwa kwenye majukwaa ya kisiasa ni dhahiri tayari wamedhulumiwa haki zao za kujitetea kwa sababu Rais Magufuli na Spika Ndugai wameingilia uhuru wa mahakama.

Utetezi huu ni mzito wa watuhumiwa haki zao za kikatiba zimekiukwa pale mihimili miwili ya dola ambayo ni serikali na Bunge imeingilia uhuru wa muhimili mwingine wa mahakama katika kutoa haki.

Huu ni utetezi tosha wa kuwafutia mashitaka feki yenye msukumo wa kumjenga Magufuli na CCM yake kwa kupitia migongo dhaifu ya watuhumiwa.

Mahakama haitachelea kulinda uhuru wake kwa kufuta mashitaka ya kubambikiziwa.

5) Hakuna makosa yoyote ya kupokea rushwa ambayo wametuhumiwa kwa hiyo Mahakama haina jinsi bali kuwaachia tu. Makosa tajwa yangelidhoofisha utetezi wao kwenye namba 1-4 hapo juu kwa kubainika wajumbe wa baraza la mawaziri ambao hawajashtakiwa hawana makosa binafsi ya jinai. Hivyo, hawajabaguliwa.

USHAURI

Kama Mkapa na JK ni "untouchables" then their sidekicks are also the "untouchables"
 
Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji na sisimizi hajawai kumuacha tembo salama
 
Watakuuliza kwa nini unatabiri kushindwa kabla ya kesi? Lakini ni wao hao hao ukiwaambia Mbao United ya Mwanza itacheza na Real Madrid ya Hispania hawachelewi kusema kwamba mbao itachezea kichapo cha mbwa mwizi!

Dunia ya wajinga waache waishi wenyewe!
 
..at least Mkapa yeye ana kinga ya Raisi.

..lakini JK yeye tuhuma zake ni ktk majukumu yake alipokuwa Waziri.

..JK akiachwa na mawaziri wengine wakaburutwa mahakamani huo utakuwa ni uonevu.
 
Mahakama huendeshwa na doctrine au itikadi ya haki bila upendeleo.

Kauli tata za Magufuli na Ndugai za kuwakingia watuhumiwa nambari moja ufisadi wa Madini akina Mkapa na JK ni utetezi tosha kwa Muhongo, Karamagi, Yona na Ngeleja.

Watakapowapeleka mahakamani mawaziri wa zamani wa Madini watakuwa na utetezi wa aina tano:-

1) Moja, "collective responsibility" yaani uwajibikaji wa pamoja katika baraza la mawaziri kwa hiyo hawawezi kutolewa kafara kwa kutekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri.

Mahakama itawaachia huru kwa sababu tu wamebaguliwa na haki zao za kikatiba za kutendewa sawa na wajumbe wote wa baraza la mawaziri hususani wenyeviti wa vikao hivyo ambao ni Mkapa na JK. Utetezi huu unaitwa "misjoinder of the accused".

2) Kutomshtaki JK wakati alipokuwa waziri wa Madini miaka ya 1997-2000 wakati mikataba ya Bulyanhulu na mengineo alisaini na hana kinga ya Urais kwenye vipindi tajwa na kutomshtaki ni kuwabagua mawaziri wa madini walioshtakiwa na utetezi wa " misjoinder of the accused" ni haki yao na lazima wapewe kwa kuachiwa huru.

3) Sheria ya wawekezaji ya mwaka 1997, sheria ya madini ya 1998 na hata ya 2010, sheria za kodi kuanzia 1998-2004 zilirandana na sera ya CCM ya kuvutia wawekezaji. Wao kwa kusaini mikataba husika walikuwa wakitekeleza sheria na misamaha walioitoa ni kuharakisha kasi ya kuwavutia wawekezaji.

Utetezi hapo ni kuwa hakuna jinai katika kutekeleza sera na sheria za nchi. Hakuna mahakama itawatia hatiani kwa hili.

4) Kauli zembe za Magufuli na Ndugai zinaingilia uhuru wa DCI, DPP, TAKUKURU na Mahakama kwa kuwasafisha watuhumiwa wakuu wa ufisadi ambao ni Mkapa na JK huku watuhumiwa wakitajwa na taarifa za kamati zilizoundwa na Rais kukidhi kiu za kisiasa na kuwatoa watuhumiwa tajwa kama makafara ya kisiasa haiwezekani vyombo vya utoaji haki kama mahakama viwatendee haki.

Kwa kuhukumiwa kwenye majukwaa ya kisiasa ni dhahiri tayari wamedhulumiwa haki zao za kujitetea kwa sababu Rais Magufuli na Spika Ndugai wameingilia uhuru wa mahakama.

Utetezi huu ni mzito wa watuhumiwa haki zao za kikatiba zimekiukwa pale mihimili miwili ya dola imeingilia uhuru wa muhimili mwingine wa mahakama katika kutoa haki.

Huu ni utetezi tosha wa kuwafutia mashitaka feki yenye msukumo wa kumjenga Magufuli na CCM yake kwa kupitia migongo dhaifu ya watuhumiwa.

Mahakama haitachelea kulinda uhuru wake kwa kufuta mashitaka ya kubambikiziwa.

5) Hakuna makosa yoyote ya kupokea rushwa ambayo wametuhumiwa kwa hiyo Mahakama haina jinsi bali kuwaachia tu. Makosa tajwa yangelidhoofisha utetezi wao kwenye namba 1-4 hapo juu kwa kubainika wajumbe wa baraza la mawaziri ambao hawajashtakiwa hawana makosa binafsi ya jinai. Hivyo, hawajabaguliwa.

USHAURI

Kama Mkapa na JK ni "untouchables" then their sidekicks are also the "untouchables"
Mkuu siyo kila kitu unajua!!! Waachie na wengine wanaojua waongee..... wewe hujui kitu kwenye sheria wewe ongea siasa mkuu!!
 
Mzee wa Law tumekuelewa
Kumbuka pia matumizi mabaya ya ofis,uhujumi uchumii n.k
Sheria zetu ni mbovu kwenye suala la ufisadi ndiyo maana mafisadi hawaogopi kitu
Wote walifanya kazi kwa kupokea Amri toka kwa mkapa na kikwete wenye Hatia ni kikwete na mkapa wengine wote watahojiwa na kuachiwa.
 
hamna kesi hapo na wabunge watakaoongea washughulikiwa na wakitoka nje wakaongea watakutana na rungu, kila kitu kitakuwa siri kama kawaida
 
Haya mambo magumu kweli sijui hata nachangiaje. Anyway tuzidi kumuomba Mungu
Hakuna ugumu hapo jiongeze tu Tambua kuwa Kipindi hicho Amri zote zilitoka juu kwa mkapa na kikwete watuhumiwa wote walitekeleza Amri toka juu hakuna jinsi mkapa na kikwete wanakwepa jinai.
 
hamna kesi hapo na wabunge watakaoongea washughulikiwa na wakitoka nje wakaongea watakutana na rungu, kila kitu kitakuwa siri kama kawaida
hata mkapa na kikwete nao binafsi wameanza kuwapiga vipapai wale wabunge wanaowaandama bungeni wapo kwa kamati zao za Ufundi kuhakikisha kuwa wanaacha kuwachana live.
 
umekosea, JK hakuwa waziri wa madini miaka ya 1997-2000 kama ulivyoweka hapo, bali alikuwa waziri wa mambo ya nje!! kuna faida yoyote mtu akipost kila Siku? nataka na mm nianze
 
We Piga kelele na u bush lawyer wako. Hao wanapigwa uhujumu uchumi kesi inasikilizwa miaka ishirini na mali tunataifisha.
 
Back
Top Bottom