Habari njema mahakamani kwa Karamagi, Muhongo, Ngeleja na Yona ni Magufuli na Ndugai

Laiti kama jf ingekuwa accessed na watanzania 5m,hii nchi isingetawalika...maana nondo za humu ni noma sanaaa...
 
Kelele za nini si msubiri tu.. Mbona kesi ile ya Yona na Mramba mbona JK au MKAPA hawakuenda mahakamani
Hawakwenda kisiasa.

Hoja hapa hawa wa Magu watapambana na wajuaji kina Chenge. Halafu mashtaka haya yana utetezi wa Magu mwenyewe; maana hajui atafungua mashtaka kwa sheria ipi yenye kunyooka. Halafu mawakili akina jesca.
 
Tangu walioanza kuweka uzio wa wastaafu hakuna atakayestakiwa na in fact atakayeshtakiwa atashinda kesi na ana haki ya kudai fidia kubwa sana

Mwanasheria mkuu AG ana kazi ya kuishauri serikali kuhusu masuala ya kisheria ikiwemo mikataba.
AG hasaini mikataba bali serikali baada ya kupitia Cabinet inayoongozwa na Rais.
Hivyo AG hana uhusiano na Acacia au kampuni ingine isipokuwa kuishauri serikali

Waziri hasaini mikataba kama ndoa ya binti au kijana wake. Ni lazima ipitie Cabinet na kupata Ridhaa. Mkuu wa Cabinet ni Rais au mwingine anayefuata kwa utaratibu. Utamshtaki vipi Rais?

Kinachoendelea ni kutaka kutafuta watu wawili, watatu kuwavunjia heshima kama kafara la kisiasa.

Hili linakumbusha yule waziri na katibu mkuu waliofungwa kwasababu ya mikataba mibovu , leo tunajua ilikuwa kisasi cha kisiasa tu kwasababu wakati wa kampeni waziri yule alimpinga bw fulani kwa kusema ni ''mswahili swahili tu ''
 
Ndiyo ugumu. Leo watu wanaitwa mashujaa lakini mazingira yamejengwa ni rafiki kwa watuhumiwa

Nilivyosikia kuwa mahakama ya mafisadi tiyari nikaamini kuwa June haifiki bila hata Jela yao maalum haijawa tiyari. Hadi leo, hata yule Jaji aliyetajwa //////escrow yupo uraiani.
Sometimes sipendi hata kuyasikia matamko ya viongozi wetu wakuu kwani huwa wanajidhalilisha wenyewe na kutuamuru kuwa tusiwaelewe
 
Ni uchambuzi mzuri. Maziwa hayawi matamu yakinywewa na wakubwa tu ila wadogo wakiyanywa yanakuwa machungu. Kama kuna utamu uwe kwa wote, kama kuna uchungu uwe kwa wote.
 
We Piga kelele na u bush lawyer wako. Hao wanapigwa uhujumu uchumi kesi inasikilizwa miaka ishirini na mali tunataifisha.
swali. Je! Watuhumiwa wakisema walikua wanatekeleza sera na maagizo ya Bosi wao! Je! Mabosi wao watabeba msalaba uo au Rais aliye madarakani atakubali watangulizi wake waende Segerea?

Maana mahakama ni chombo huru na kinacho msikiliza mtu na kutenda haki bila upendeleo.
 
Siasa za maj chooo izo, tamshangaa sna baba jesca akimuacha JK na BM akang'ang'ana na hao njemba, tatzo baba jesca anapenda sifa sana ad anaarbu
 
Rais Magufuli japo umesimamia ipasavyo hili sakata la madini na kutaka wahusika wachukuliwe hatua basi ni vema hawa marais (Mkapa, JK) kushitakiwa na ni lazima kwani hawa ndio wahusika wakuu. Kinyume cha hicho utakuwa hujatenda haki ya watanzania ambao wengi tunataka hawa watu (marais) wanyongwe. Ogopa Mungu wako na uache unafki, watanzania tuko nyuma yako TUNATAKA kina Mkapa na Kikwete kunyongwa! Hawa wamedhulumu taifa letu matrilioni leo iweje wawe huru?
 
We Piga kelele na u bush lawyer wako. Hao wanapigwa uhujumu uchumi kesi inasikilizwa miaka ishirini na mali tunataifisha.
Hapo umenena bila ya ushabiki WOWOTE
POINT NI NINI? NI KWAMBA
DEGE LIMETUA BONGO MAJORITY SHARE HOLDER MUHUSIKA MKUU YUKO TAYARI KWA MAZUNGUMZO N.A. GOVER

We Mara hili mara lile nyumba mara.NI.BALAAH
 
Wangeweka kifungu katika katiba kuwa marais wastaafu wanaweza kuhojiwa lakini wasifungwe.

Uzuri wa kutoa nafasi wastaafu kuhojiwa ni kutoa nafasi taasisi ya Urais na wananchi kupata ufahamu wa makosa ambayo Rais mstaafu anaweza kutenda yeye mwenyewe au washauri wake.

Na huu ufahamu kuhusu matendo / maamuzi ya Rais Mstaafu au Taasisi ya Urais aliyemaliza muhula wake itatoa funzo na kuingia katika kumbukumbu muhimu kuzuia maamuzi yasiyo makini , ukiukwaji wa katiba au uonevu kwa mihimili mingine ya dola.
 
..at least Mkapa yeye ana kinga ya Raisi.

..lakini JK yeye tuhuma zake ni ktk majukumu yake alipokuwa Waziri.

..JK akiachwa na mawaziri wengine wakaburutwa mahakamani huo utakuwa ni uonevu.
Magu amelifungulia "dude" kwa ajili ya kuwalaghai wadanganyika tu.

Magu anaonekana (anaigiza?) kusonononeka kwamba "tunaibiwa" na "tumeibiwa vya kutosha"

Baada ya kuzungumza na "Mwizi" ameibuka mbele ya Camera na kusema (kupiga sound kwa kauli hewa) kwamba "mwizi" ametubia na amesema wamekubaliana " atalipa".

Magu amejisahau kwamba maigizo yake yanaangaliwa na wote, anaowatumu kuiba , wadanganyika anaowalenga kuwapa matumaini hewa , wachambuzi, wakosoaji. Kama ukiangalia ile video baada ya mazungumzo yao baina ya "mwizi" na "muibiwa" ,utamwona Prof. Kabudi akishindwa kushangaa Boss wake anavyopiga sound.

Hivi kweli "mwizi" amekubali kulipa?

Kwa nini "mwizi" alipohojiwa yeye alisema amekuja kuweka mambo sawa na kusaidia kufikia suluhu. Aliongeza kusema kwamba suluhu au maelewano yatatokana baada ya kukaa pamoja kwenye meza ya kupiga sound "round 2).

Magu kwa kuelezea kile anachotamani kitokee, "tulipwe kutoka kile tulichoibiwa" tayari amemwaamsha "mwizi" kutengeneza timu inayoweza kupiga chenga ya mwili na kupiga sound ya hifi. Tunaelewa kwamba timu atakayoiunda Magu haitokuwa tofauti na zile timu za watangulizi wake, timu ya kudai 10%.

Hili dili la Magu tayari limeshapiga U-turn baada ya kuwafanya na kuwatangaza JK na Mkapa kuwa ni "kifaru cha jeshi".

Tunajiuliza, Uzalendo wa CCM kwa maliasili za nchi hii na masilahi ya nchi na umma wa nchi hii yameanza lini?

Kama kuibiwa si jambo zuri, ni kwa nini CCM inaiba kura na kukwapua ushindi wa CUF?

Kwa masikitiko niseme tu kwamba hali ya kitaa kiuchumi ni mbaya. Wale wanaotembelea Ikulu hupata juisi na pipi, huku kitaa ni vumbi na mifuko kutoboka tu.

Magu wacha kupiga sound, muda wa "hapana kazi tu" unapita kwa kasi. Tumeshapigwa sound za kutosha kwa miaka 40+ na tumeshatumbuliwa vya kutosha, tumemstahamilieni CCM vya kutosha lakini bado hatuoni matunda, ni maumivu mbele kwa mbele.

CCM imebadilika au ni ilel ile?
 
Hawana kesi hao na nitashangaa sana wakifikishwa mahakamani. Labda kwa makosa mengine lakini si ya mikataba ya madini.

Silioni tatizo kwenye mikataba.
 
Back
Top Bottom