Habari njema kwa mkoa wa Njombe na wana CCM wote !!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari njema kwa mkoa wa Njombe na wana CCM wote !!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by greenstar, May 5, 2012.

 1. g

  greenstar JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nifuraha ya kipekee kuona Mkoa Mpya wa NJOMBE ni unapaa katika medali za kisiasa na kiuchumi baada yakuwa na WABUNGE MAKINI kutoka CCM wenye taaluma na uzoefu uliotukuka katika kuhamasisha maendeleo.Ukizingatia tuna MKUU wa MKOA mchapakazi asiyependa porojo hakika NJOMBE itapaa sana katika ukanda wa KUSINI nakuwa kitovu cha UCHUMI kutokana na rasilimali zilizopo kama MCHUCHUMA na LIGANGA,MISITU ya MBAO,CHAI,PARETO,ALIZETI na MAHARAGE yanatosha kugeuza mkoa huu kuwa kitovu cha uchumi.

  Pongezi za dhati kwa wabunge hawa;

  Mh.Deo Filikunjombe
  Mh.Anne Makinda
  Mh.Eng.Gerson Lwenge(NW UJENZI)
  Mh.Dkt.Binilith Mahenge(NW MAJI)
  Mh.Jah People

  Hawa viongozi pamoja na MKUU wa MKOA Mh.Msangi wataleta mapinduzi ya maendeleo kwa kutumia taaluma zao na uzoefu katika kazi,Rai yangu kwa WANANJOMBE wote,tuwape ushirikiano katika kuharakisha maendeleo ya MKOA wetu.

  Pia tuache kuyumbishwa na propaganda za wanasiasa UCHWARA kama NYIMBO eti ataleta maendeleo? Wananjombe si VIPOFU wala si VIZIWI wala si ZEZETA kana kwamba NYIMBO ni mgeni katika siasa za NJOMBE,alipata nafasi miaka 10 huko nyuma akasahau wajibu wake wakuwatumikia wananchi akawa nachumia TUMBO,wanaCCM wamegundua JANJA yake anakimbilia CHADEMA,salamu zake,ASAHAU kurudi kutawala tena na NJOMBE ina watu makini na WASOMI wanaojua ukweli wa mambo.

  Kisa cha kweli ninachokikumbuka,alinunua PIKIPIKI 25 ili awape VIJANA wake wakati wa kampeni akiamini atashinda UBUNGE,kwa bahati mbaya alishagawa chache kwa viongozi kadhaa,lakini aliposhindwa aliwaiita wote NYUMBANI KWAKE akiwadanganya anafanya SHEREHE ya KUJILIWAZA na kujipanga UPYA kwa uchaguzi UJAO...wale watu wakaenda na mbwembwe zao na PIKIPIKI za HONGO walipofika akawageuzia KIBAO na KUWANYANG'ANYA Pikipiki zote !
  Huyu ndiyo NYIMBO yule mjanja mjanja ambaye anahangaika kurudi kwenye SIASA,pole sana bw.NYIMBO kwa kufulia hadi unaamua kunyang'anya pikipiki za MCHINA zenye thani ya Mil.25.

  Kama wewe mjanja fufua chama chako cha PONA ili uone siasa siyo poroja bali UTENDAJI.....tunafahamu unavizia kuwa Mnykt.wa CHADEMA kwa vile huna kazi ya kufanya....sasa hivi umewajengea kibanda cha OFISI pale WANGING'OMBE na kukibatiza ofisi za CHADEMA mkoa wa NJOMBE,imekula kwako kwani hutaweza kunyang'anya pale watakapo kupiga chini kama ulivyotupwa na CHIKU ABWAO katika MKOA wa IRINGA.
  \
  Nakushauri nunua trekta ulime KARANGA na alizeti ili tudumishwe UCHUMI wetu badala ya kuzunguka vijijini ukifungua matawi hewa na kutumia mitandao ya KIJAMII na magazeti wakusifie kwa habari za kufikirika.

  Wananjombe msidanganyike na huyu NYIMBO,ameshahujumu shule za WAZAZi za WANGING'OMBE na MTWANGO hadi zikashuka kitaaluma kwa ulafi wake,barabara hazipitiki,na miradi ya umeme ilikwamishwa na yeye baada ya YONO kumshinda katika UCHAGUZI...kwa ufupi anataka kuwatapeli tena...basio msipoteze muda wenu kuhudhuria mikutano yake...Ukisikia anakuja basi wewe wahi shambani au kazini kwako ukijitafutie riziki yako....Tufanye kazi kwa bidii ili tupate maendeleo yetu na familia zetu.Kuwa MBUNGE siyo suluhisho kama hakuna nia ya dhati kuwatumikia wananchi.

  SIASA za NJOMBE si za kishabiki kama mikoa mingine,tunahitaji watendaji makini ambao tayari tunao wakutosha ambao wapo tayari kushirikia na WABUNGE wao !!!!!!!!

  Nawassilisha
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Utaacha lini porojo na majungu?
   
 3. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Sasa Chadema inaingiaje hapa?Unawasifia hao unaowaita hawana majungu Ila wanachapa kazi,maneno Kama haya yameshasemwa na viongozi Wa ngazi za juu miaka 50 iliyopita zaidi wametuachia manyoya tu.Acha majungu mara pikipiki mara vile haueleweki Kama popo unazunguka zunguka tu kichaka hapa.Hii sio sehemu ya kupeana pongezi kwa nini usingewatumia pongezi hizi ktk simu zao?Hichi ulichoandika hapa kina faida gani kwa wananchi?
   
 4. J

  Jadi JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  huyu katumwa?mtu wa kawaida hawezi kuandika kwa muda mrefu hivi
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wANGEKUWA WACHAGGA KWELI WANGELETA MAENDELAO KWAO LKN HAO ULIOWATAJA, HUYO MAKINDA YUPO HUKO BUNGENI MIAKA NENDA MIAKA RUDI USHAONA TOFAUTI HUKO NJOMBE?
   
 6. S

  Small Master Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe yeye ndo kipofu maana sehemu hii ni ya watanzania wote kwa mstakabali wa nchi nzima, huyu anadhani maendeleo ya nchi hupimwa kwa mkoa mmoja tu? Je anasemaje kuhusu maliasili, madini je?, mazao mengine kama kahawa maana mkuu wa wilaya ya mbozi amejiuzuru kutokana na wananchi kuibiwa kahawa zao kwa kulipwa Tshs 1,000 kwa kilo wakati kwenye mnada wa Moshi kilo moja ni Tshs 7,000, Yupo hapo?
   
 7. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna tofauti gani hapo kwenye RED???
   
 8. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mbwa sharti abweke ili kumdhihirishia mwenye mbwa kuwa anafanya kazi.
  Kwa taarifa yako wananjombe hatisikilizi upuuzi huu.
   
 9. L

  Lamusumo JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa haijui njombe na pengine thread ameandika ofisi za ccm chini usimamizi wa viongoz wa ccm..hapa njombe mjini pamoja na kwamba cdm haikusimamisha mgombea ubunge wala udiwani dr. Slaa aliongoza kwa kura za urais,nguvu ilotumika kumshinda nyimbo ni hazielezeki, ccm wenyewe wanakiri kuwa walikuwa wanarushiwa mawe wakienda kwenye kampeni.kwa taarifa mkoa wa njombe hasa majimbo matatu ya njombe operations za cdm zimerahisishwa na radio njombe kwa hyo mwanzisha hoja atoe porojo zake humu jf
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mbona umeandika maelezo marefu sana!? Halafu hueleweki
   
 11. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nani alikuteua kuwa msemaji wa mkoa wa njombe na wananchi wake?
   
 12. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Unanmzungumzia msangi huyu aliyetoka iringa?sahau kama makinda hajawaletea maendeleo imekula kwenu na mdaraja yenu ya mbao!kalime viazi na numbu acha kupoteza muda jf,ukiendelea na porojo nakuitia Sagasaga sasa hivi
   
 13. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  una akili inayofanana na ya 'maiti'
   
 14. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika maelezo yako nimegundua kitu: (tuelezee ni kwa kiwango gan NYIMBO anakukosesha usingz ww na magamba wenzio) maelezo yakijtosheleza tutawabadilishia operation kamanda, wa ukanda huo, ili angalau tuwapatie wa level zenu.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jitahidi Nape leo lazima atakulipa Allowance kwa hii thread yako iliyowabagua wanaCCM wenyewe kwa wenyewe
   
 16. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,922
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Greenstar(nyota ya kijani) jina lako la ni la alama ya ccm nyota ya kijani ILA HAMJUI uzazi wa mpango. MNAZAA HOVYO HOVYO, mmezaa richmond, mmezaa dowans, kagoda, mnazaa tu, kiwira, sasa na wewe eti greenstar unazaa uzushi utamdanganya nani? Ngoma tuachie Chadema tukupangie mambo.
   
 17. m

  moma2k JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Hao wabunge wanne poa! Mkinda hovyo Amekuwa Mbunge kwa miaka mingi huko Njombe lakini hakuna maendeleo, hakuna alichofanya. sasa tuna hitaji damu mpya kama kama za akina Filikunjombe. Vinginevyo CDM itachukua jimbo.
   
 18. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hivi we umesöma kweli au una brain concussion!?
   
 19. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mimi niwanjombe ila namshangaa huyu jamaa!
  hatuna akili za kijinga kama wewe!
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kumbe unaugonvi na mtu!
  kama kawaida wanaccm kugombana na watu!
  mtamuua kama wa arumeru!?
   
Loading...