Habari Njema Kutoka Barrick Gold kwa Watanzania, Tunaanza Kufaidi Rasilimali Zetu, Donge Nono la Dola Milioni 100 zalipwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Hatimaye Tanzania sasa tunaanza kufaidi rasilimali zetu za madini, ambapo leo, donge nono la dola za Marekani milioni 100, zimelipwa kwenye kile kibubu chetu pale kwenye ule mfuko Mkuu wa hazina ya serikali kama advance payment ya kile kishika Uchumba cha dola milioni 300, ambacho baadae tulikigeuza kuwa ndio mahari kamili ya yule binti yetu makinikia.

Kiasi kilichobaki cha dola milioni 200, kitalipwa kwa mikupuo mitano ya dola milioni 40 kila mkupuo ambacho kitalipwa ndani ya miaka 5, kwa kila mkupuo kulipwa ndani ya mwaka mmoja mmoja.

Habari njema hii ni kwa mujibu wa Barrick,
Karibu ujisomee
Barrick Partnership with Tanzanian Government Delivers First Major Outcomes

Japo deni letu la makinikia ya Barrick lilikuwa Dola bilioni 190 ambazo zingetosha kumnunulia Noah kila Mtanzania, tukaahidiwa kishika Uchumba cha dola milioni 300!, lakini kufuatia majadiliano marefu, tulisamehe deni lote, na kile kishika Uchumba cha dola milioni 300, tulikikubali kuwa sasa ndio mahari kamili, hivyo hili donge nono la dola milioni 100, ndio mwanzo wa utekelezaji wa makubaliano na Barrick.

Donge nono hili la dola milioni 100 ni nje ya gawio la hisa asilimia 16% za bure bure, ambayo Tanzania tumepewa kwenye kampuni mpya ya ubia wa Tanzania na Barrick, kampuni ya Twiga, na manufaa makubwa kabisa, manene na manono kabisa yanayosubiriwa kwa hamu, ni mgawo wa 50/50, yaani pasu kwa pasu ya manufaa ya Kiuchumi ya kila kinachopatikana kwenye madini yetu.

Huu ni ukombozi mkubwa sana kwa taifa letu. Hongera sana JPM.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Update.
Bunge letu ndio limetangaziwa rasmi fedha hizi mchana huu, sasa hivi, hivyo wewe as mwana jf, you were the first to know, na kwenye magazeti ni kesho!.
Viva if
Mungu Ibariki JF
Mungu Ibariki Tanzania
P
Update 2
Kampuni ya Barrick imeilipa Tanzania dola milioni 100, sawa na takriban sh. bilioni 250, ikiwa ni sehemu ya malipo ya dola milioni 300 ambazo Kampuni hiyo ya Madini ilikubali kulipa kama fidia ya kodi.

Mfano wa Hundi ya kiasi hicho cha fedha imekabidhiwa na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Barrick, Bw. Hilaire Diarra kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, kwa niaba ya Serikali, Jijini Dodoma tarehe 26 Mei, 2020.

Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mwenyekiti wa Timu ya Serikali ya Majadiliano na Barrick ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Kamati yake, Dkt. Mpango alisema tukio hilo ni mwanzo wa makubaliano ya mkataba wa msingi kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni hiyo yaliyofikiwa Disemba 19, 2019 na kusainiwa rasmi Januari 24, 2020.

Dkt. Mpango aliyataja makubaliano mengine yaliyofikiwa kati ya Serikali na kampuni hiyo kuwa ni kuundwa kwa Shirika la Madini la Twiga lenye umiliki wa pamoja likalofanya kazi nchini katika kusimamia uendeshaji wa migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara pamoja na migodi mingine nchini ambapo Serikali ya Tanzania itashiriki katika utoaji wa maamuzi kuhusu uendeshaji wa migodi, mipango, manunuzi pamoja na masoko ya madini.

“Tulikubaliana kuhakikisha kuwa faida za kiuchumi zinazotokana na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi pamoja na North Mara zigawanywe kwa msingi wa usawa wa asilimia 50 kwa 50 kati ya washirikania ambapo hisa za Serikali zinazotokana na faida za kiuchumi zitatolewa katika mfumo wa mrabaha, kodi pamoja na kupata asilimia 16 ya faida kutokana na makampuni hayo kufanya kazi nchini” alisema Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema mbali na makubaliano hayo, kampuni ya Barrick imekubali kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 5 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Mtambo wa kuchakata madini nchini (smelter).

“Kampuni ya Barrick pia imekubali kuanzisha ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuahidi kutoa hadi dola milioni 10 kwa kipindi cha miaka kumi kwa ajili ya utoaji wa mafunzo yanayohusu sekta ya madini”, aliongeza Dkt. Mpango.

Alisema Kampuni ya Barrick ilikubali kutoa dola 6 kwa kila ounce ya madini itakayouzwa (ikijumuisha mchango kwenye Mfuko wa Mandeleo ulioanzishwa na Kampuni ya Barrick Tanzania) ili kusaidia jamii zinazozunguka maeneo ya migodi pamoja na kutoa kiasi cha dola milioni 40 kwa ajili ya kuboresha kipande cha barabara kati ya Bulyanhulu na Mwanza na kujenga nyumba na miundombinu yake.

“Naipongeza Kampuni ya Barrick kwa kuanza kutekeleza makubaliano haya na natoa wito kwa kampuni nyingine za madini na wawekezaji wengine katika sekta hiyo kuiga mfano mzuri uliooneshwa na Kampuni hii katika kuhakikisha kunakuwa na hali ya usawa katika uendeshaji wa shughuli za madini nchini kwa faida ya pande zote mbili” alisisitiza Dkt. Mpango.
P
 
Ni kweli makinikia yaendelea kusafirishwa nje?

Pascal Mayala nimekuwa nikijua wewe ni msomi kumbe ni wale wale.

Barrick wamelipa $100million kati ya $300m waliohaidi kulipa.

$100million imetokana na mauzo ya kwanza ya container 1600 za makinikia zilizokuwa zimezuiwa na serikali.

$200million zilizobaki wamehsidi kulipa ndani ya miaka 5. Yani kila mwaka ni $40mln.

Kupigwa kupo pale pale.

Kama safari moja ya container 1600 wamefanya mauzo nakupata faida ya zaid ya $100million. Jiulize kwa mwaka wanapeleke contsiner ngapi? Na kila mwaka tunaambulia $40m only!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal,

Haya ni mauzo ya makinikia bwana. Hawa jamaa wajanja sana,mie nilijua watatoa mzigo kule walipoiba,kumbe humu humu.

Bora tungeyapiga mnada wenyewe tu yale makontena.

Sent using iphone pro max

Je kabla ya magufuli.. hayo mauzo ya makinikia tulikuwa tunalipwa bei gani?
Magufuli ni jembe.. mbona awamu za 3 na 4 hatukulipwa na makinikia yalikuwa yanasafiri
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom