Habari Njema: Kuchimba dawa kwa abiria sasa ni dakika 20

Lalamiko kwa abiria sio muda wa kuchimba dawa huo dk 10 .Sasa dk 20 zote za nn? unatutosha Kabisa uliopo..yaani Hawa LATRA mgonjwa anaumwa kichwa unamtibu miguu...lalamiko letu Ni chakula Bei ghali..watu hatufanani vipato.unashushwa hotel hamna hata chakula Cha Bei nafuu..kweli lunch Nile 8,000 au elfu 10 etc? Haya ndio Mambo yakufanyia kazi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hoteli zenyewe ziko porni kiasi kwamba tuna kosa alternative ya kupata chakula cha bei rahisi, ,inaumiza sana kwa kweli
 
Bado ni kizungumkuti tu, ukiacha dharula, wangesema kila baada ya kilomita ngapi gari inapaswa kusimama kwaajili ya kuchimba dawa, wasafiri wana afya tofauti tofauti.

Kama ni muda wa safari, barabara ndio changamoto kubwa sana, ikifuatiwa na askari, dereva ni changamoto ya mwisho. Barabara pana na zenye viwango, basi inasifiri kwa 100kph bila tatizo, sasa mara shimo, mara tuta, mara askari anarukia barabarani kutokea kichakani na speed gun yake n.k

Hapa mpaka Chalinze, inapaswa kuwa lisaa tu kwa miundombinu bora, 600km zimalizwe kwa masaa 7.5 tu
Naunga mkono, yaani safari inakuwa kama adhabu
 
Wadili na ishu ya kushushwa NANGURUKURU chakula cha chini kabisa kinagharimu sh.5k wakati hakuna (ni marufuku kuwa na) mgahawa mwingine eneo hilo wala huruhusiwi kuuza "cha-kula" chochote kama hujaingia humo

Hilo ndilo tunalolipigia kelele kila siku na wala si vinginevyo, swala la muda m'bongo hata dakika moja tu inamtosha kabisa atakula atakunya na atapata muda wa kupumzika ndani ya dakika hiyohiyo moja!
kama umazungumzia ile hotel mpya ya wife wake remote controller sahau kabisa
 
Dak 2 kama unakata gogo inabd ulisukuma chap chap litoke usije ukabaki na kipisi cha nnya
Dah Hatari sana aseh; ilikuwa kama wanyama, halafu kujisaidia kunahitaji utulivu sana angalau dakika 10 hivi ndiyo inakuwa murua. Dakika 10 zilizobaki unapiga msosi.

Heko kwa LATRA
 
sina hamu nao wamenigeuza kiboyogoyo na mifupa yao wanazani sie mbwa
Alafu ili kukukosha ukilalamika wanakwambia ongeza elfu tatu tukuongozee nyama bila chipisi! Ukishatoa elfu tatu kiteki away kinawekwa kwa mkwara mbele yako! Sasa fika kwenye meza anza kula! Unaishia kwenye upembuzi yakinifu ya vimfupa tudogotudooogo vilivyocharangwa mix na nyama yaani usipokuwa makini unapaliwa na vimfupa! Mimi huwa nakasirikaga naishia zangu kaunta!
 
Back
Top Bottom