Habari njema - Arsenal yaanza mazungumzo na Massimiliano Allegri

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,735
239,358
Hatimaye ile timu mbovu na yenye mwenendo wa kuaibisha Arsenal , imepata maono mapya na taratibu imeanza kulivua limbwata ililopewa na kocha aliyechoka Arsene Wenger.

Vyombo mbalimbali vya habari za michezo vimeripoti kuanza mazungumzo ya kumpata kocha wa Juve , Allegri ambaye kwa Italy ni kama ameshinda kila kitu , huku akielekea kuivusha UEFA CHAMPIONS LEAGUE Juve dhidi ya Timu ya marefa ya Barcelona .

Kila la heri Arsenal .
 
Juve lazima achapwe wiki ijayo-watatoka 3-0 kisha kwenda dakika za nyongeza
Naiona nusu fainali ya barca na altetico madrid
 
Unakosea sana kusema Arsenal ni mbovu! Sasa Sunderland itakuaje??
Nakuhakikishia Sunderland itaitandika Arsenal gemu ya marudio , Arsenal sasa hivi ni sawa na shamba la kijiji , wala si shamba la bibi tena , maana shamba la bibi ni la ukoo tu .
 
hizi habari za kuanza mazungumzo zipo kila leo ..wamiliki watakapo ona hata makombe yanumuhimu pia pamoja na faida wanayoipata watafanya maamuzi.
Gunnerz till i die
 
Back
Top Bottom